KERO Mbeya: Kabwe hapafai kuwa Soko Jioni, ni pachafu kupindukia, tunakaribisha Kipindupindu

KERO Mbeya: Kabwe hapafai kuwa Soko Jioni, ni pachafu kupindukia, tunakaribisha Kipindupindu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Masoko mengi Tanzania ni machafu, wanachojua ni kukusanya ushuru tu.
Mara ya mwisho nilikwenda soko la Ilala mwaka jana, nimeapa sikanyangi tena. Soko hata choo kina afadhali.
Hatari
 

Attachments

  • DSC_0480.JPG
    DSC_0480.JPG
    1.1 MB · Views: 4
Sio mbeya tu
Nenda mabibo wanapaita mahakama ya ndizi
Bila jombo jomba huingii
Mbeya, Ilala, Mabibo.

Kwahiyo, sio tatizo la wananchi ni wanaowasimamia wananchi
 
Hivi ni nani alitoa wazo la kupafanya Stendi ya Daladala ya Kabwe kila ikifika jioni kupageuza Soko?

Moja hili eneo ni chafu kupita maelezo na Wafanyabiashara wamejianzishia Dampo hapohapo.

Yaani huku taka zimejaa lakini pembeni yake unaona mama anaendelea na kuuza Samaki, Matunda, Mboga Mboga n.k.

Maafisa wa Afya wale 'Mabwana Afya' mmetulia kimya kana kwamba hamuoni kinachoendelea maeneo hayo au mpaka Watu waugue kipindupindu ndiyo mtapazuia.

Ukiachana na uchafu pia ikifika jioni Daladala zinapata shida sababu stendi inakuwa imebanwa na Wafanyabiashara, hivyo kusababisha kero isiyokuwa na msingi.

Nao vibaka hawako nyuma kila ikifika jioni wanaingia kazini ukizubaa tu imekula kwako.

Jamhuri ya wachuzi, majiji na miji imejaaa masoko na kila mwaka wanaongeza masoko
 
Wahusika watu wa afya walifanyie KAZI.
Mbeya Kwa sasa kipindupindu kinazidi kushika Kasi.
 
Back
Top Bottom