DOKEZO Mbeya: Kemikali za kuivisha Ndizi zimehamia katika matunda mengine, Wataalam wa Afya watueleze kama ni salama

DOKEZO Mbeya: Kemikali za kuivisha Ndizi zimehamia katika matunda mengine, Wataalam wa Afya watueleze kama ni salama

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Vipi yale machungwa na mananasi pale segere mbona ni machachu vile wakati yanaonekana yameiva? Naambiwa nisinunue pale nikanunue korogwe ndiyo yameiva kihalisia, ya segere yanaivishwa kwa moto! Kumbe wengine nao huivisha matunda kwa kemikali? Ndio maana kuna matunda yameiva lakini ladha yake si ya kawaida!
Hahahahahaha
 
Wafundishwe tu njia salama ya kutumia. Kawaida matunda yanapoiva hutoa kemikali ambayo huchochea matunda mengine kuiva. Sasa waivishaji hutafuta kemikali kama hiyo ya kutengenezwa. Wenzetu wanafanya hivyo miaka na miaka.
 
Wanasubiri chadema watangaze maandamano waonyeshe uhodari wao.
Kifupi hiki chombo kimejisiwa sana, huwa nashindwa kuelewa hiyo ulipo tupo yao ina lenga nini hasa wakati kuna mambo ya kuhatarusha uhai wa watanzania yanafanyika nanwao wapo tuu, hivi hawana vitengo ? Au wao ni kua deal mambo ha kiutawala tuu!
 
Calcium Carbide ikiguswa na unyevu wa kwenye hewa na kutoa gesi iitwayo acetylene. Acetylene hii inafanya kama kuiga homoni ya asili ya mimea iitwayo ethylene, ambayo husababisha matunda kuiva.

Kwa tuliosoma chemia tunaelewq madhara ya hii Calcium Carbide ina madhara mengi kwa binadamu ikiwemo kuharibu mfumo wa upumuaji, saratani (kansa), pamoja na kuharibu ini na figo

Kwa sasa naogopa kula hata matunda ni hatari sana
Mkuu uko vizuri. Mimi nilisoma chemistry yenye 'CSEE' na 'ACSE' ila sikumbuki hii reactions. 🙏
 
Huwa najiuliza TISS wanafanya nin cha ziada zaidi ya kulinda maslahi ya wanasiasa ,mwenge,cjui bendera chadema ,badala ya mambo ya msingi kama haya.
Mkuu hao unaowataja wenyewe wanategenea wewe hapo utoe taarifa kwani hawawezi kuwa kila eneo alafu wanaweza kuwa washalinasa jambo Hilo na kuliwasilisha kwa watu wa uchunguzi (polisi) mchakato ukawa mgumu hapo
 
Habari Wana Jamiiforums wenzangu, ndugu yenu Mwanongwa katika pilika zangu nikakutana na Stori za kwamba kuna Wafanyabiashara wa Ndizi pamoja na Maparachichi ndani ya Mkoa wa Mbeya wamekuwa siyo waaminifu katika biashara hiyo.

Kawaida ndizi zinapokomaa huwa zinavunwa na kuvundikwa kwenye sehemu yenye joto ili ziweze kuiva na kuwa tayari kuliwa.

Siku za hivi karibuni Wafanyabiashara wasiyo waaminifu wamebuni mbinu mpya ya kuivisha ndizi kwa njia ya kutuma kemikali.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakituma kemikali hizo ambazo huivisha ndizi Kwa muda mfupi tofauti na utaratibu wa kuzivundika.

Nimefika kwenye Soko Kuu la Ndizi “Kiwira” lililopo Wilayani Rungwe, Mbeya, nikapiga Stori na baadhi ya Wafanyabiashara ambao walidai kutumia kwao kemikali katika kuivisha ndizi kumeongeza kipato chao cha kila siku.

Wanadai kemikali hizo husaidia kuivisha ndizi kwa muda mfupi, wakiziweka kwenye matunda baada ya siku moja tu yanaiva vizuri kabisa, hivyo kuwafanya kuwa na Matunda yaliyoiva kila siku.

Matumizi hayo yanaendelea hadi kwenye Maparachichi pamoja na maembe ambayo bado hayajakomaa vizuri.

Mchezo huo umehamia kwenye masoko mbalimbali hapa nchini kama vile Soko la Matunda Soweto - Mbeya, Soko la Mabatini - Mbeya, Soko la Uyole na Soko la Sabasaba - Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga.

Mwamba sikuishia hapo nikataka kujua kemikali hiyo wanaipata wapi na inauzwaje, hapo ndiyo nikapatwa na mshangao baada ya kuambiwa kuwa hiyo dawa haipatikani madukani ila huwa wanainunua kwa njia ya magendo na inatoka katika nchi za Malawi na Zambia.

Swali linakuja kama hii kemikali inauzwa kwa njia za panya, Je, inausalama kwa Watumiaji wa hizo ndizi ambazo zinaivishwa?

Jibu ni hapana, Kemikali hiyo ni hatari kwa afya ya walaji wa Matunda hayo ambayo yameivishwa Kwa kemikali hiyo.

JE, VIONGOZI WA MASOKO WANAJUA JAMBO HILI?
Baadhi yao wanadai wanasikia tu taarifa hizo mtaani ila hawajafanikiwa kuwaona Wafanyabiashara wakituma kemikali hizo.

Hivyo, wanafanya upelelezi ili kujua ni Wafanyabiashara gani ambao wanatumia kemikali hizo ambazo zimekuwa hatarishi kwa afya ya Binadamu.

KIAFYA HII KEMIKALI INA ATHARI GANI?
Nimefanikiwa kupata Kemikali yenyewe kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara ambaye aliniuzia kimfuniko kimoja cha kopo la maji la Lita moja Kwa kiasi cha Tsh. 2,000 tu, na akaniambia natakiwa kuchanganya na maji kiasi cha lita 20.

Kemikali hizo ni Calcium Carbide na Etefon 480 zinachanganywa na maji ambapo zinatoa gesi inayotumiwa kuivisha matunda.

Basi ikanibidi nimtafute bwana afya na kumuonesha kopo la kemikali hiyo na kutaka kujua hiyo ina athari gani kwa binadamu, majibu niliyopewa ni kwamba kemikali hizo hutumika katika utengenezaji wa Mbolea na zinaweza kusabisha magonjwa mengi yakiwemo Saratani.

Afisa na Mtaalamu wa Afya anashauri tuwe makini tunaponunua ndizi, anazotaja kuwa zimeathirika kwa kiasi kikubwa.

Anasema kwa kawaida, ndizi zinapaswa kuiva kati ya siku tatu hadi nne, zinapovunwa zinakuwa za kijani lakini ukiona ndani ya muda wa siku moja tu unakuta zimeiva unapaswa kuwa na wasiwasi.

Ndizi zilizoivishwa kwa njia ya kuzivundika huwa zinakuwa na rangi ya njano na ukijani kwa mbali lakini zilizoivishwa kwa Kemikali huwa zinakuwa za njano kabisa, hivyo, tunapaswa kuwa makini pindi tununu hapo ndizi.

Mwanongwa nawakumbusha tu viongozi wa serikali kupita Kwenye maghara ya Matunda na kufanya ukaguzi maana huko ndiko mchezo wa kuivisha Kwa kemikali unafanyika.
View attachment 3133539
Asante kwa utafiti wako,hapa atakuja mnufaika wa mambo haya atatuambia sii ya kweli na uzushi kwa manufaa yake na genge la biashara hii haramu ya kuangamiza uhai wa watanzania.Halafu atakuambieni kuwa ni upotoshaji.Tafsiriye yangu kwenye hili ni kuwa huu ni ufisadi mpya kama ulivyozoeleka na kuhalslishwa na unalindwa na chawa.
 
Kifupi hiki chombo kimejisiwa sana, huwa nashindwa kuelewa hiyo ulipo tupo yao ina lenga nini hasa wakati kuna mambo ya kuhatarusha uhai wa watanzania yanafanyika nanwao wapo tuu, hivi hawana vitengo ? Au wao ni kua deal mambo ha kiutawala tuu!
Nishida sana
 
umeokoa maisha ya wengi sana ,yaan kwa taarifa hii wewe ni mzalendo haswa na wala sio uzalendo wa kufia chama bali wa kuwajali watanzania wenzio na kuitakia heri Tanzania ,Mungu akubariki sana
Amina
 
Machungwa kanunue muheza pale segera wanaouza barabarani sio waaminifu wanayaunguza na moto ili kuwalaghai wageni wasiojua machungwa
Vipi yale machungwa na mananasi pale segere mbona ni machachu vile wakati yanaonekana yameiva? Naambiwa nisinunue pale nikanunue korogwe ndiyo yameiva kihalisia, ya segere yanaivishwa kwa moto! Kumbe wengine nao huivisha matunda kwa kemikali? Ndio maana kuna matunda yameiva lakini ladha yake si ya kawaida!
 
Vijana wameongeza ubunifu kwenye ajira zao, japo ubunifu huu unaweza igharimu afya ya mlaji.
 
Hatari sana, hii kemikali itakua haijafika MTO WA MBU? kwa wenyeji wa Arusha, Mto wa Mbu njia ya kuelekea Karatu, Ngorongoro ni eneo maarufu kwa uuzaji wa ndizi mbivu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.
 
Back
Top Bottom