Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na bado mnaletewa GMOCalcium Carbide ikiguswa na unyevu wa kwenye hewa na kutoa gesi iitwayo acetylene. Acetylene hii inafanya kama kuiga homoni ya asili ya mimea iitwayo ethylene, ambayo husababisha matunda kuiva.
Kwa tuliosoma chemia tunaelewq madhara ya hii Calcium Carbide ina madhara mengi kwa binadamu ikiwemo kuharibu mfumo wa upumuaji, saratani (kansa), pamoja na kuharibu ini na figo
Kwa sasa naogopa kula hata matunda ni hatari sana
Hatari sanaNa bado mnaletewa GMO
Tupo kwenye nyakati ambazo mimi, wewe na yule tukiwa na uhakika wa sisi na familia zetu kwenda chooni na kulipa ada basi nothing else matters even if it means keeping lives of our fellow Tanzanians at stake.Siku kadhaa zilizopita kulitokea madai kama hayo ya wafanya biashara ya ndizi soko la Mabibo, Dar kutumia gas maalumu iitwayo Ethylene ili kuivisha ndizi kwenye makontena. Baadae TBS wakatoa taarifa kuwa hiyo Ethylene haina madhara kiafya. Kitu cha kujiuliza kama ni kweli hiyo Ethylene haina madhara hao wanaoitumia watashindwaje kutumia hiyo kemikali ya etefon? Au TBS watatoa ufafanuzi mpya kuhusiana na hii etefon kuonyesha kuwa au kutokuwa na madhara kiafya?
Habari Wana Jamiiforums wenzangu, ndugu yenu Mwanongwa katika pilika zangu nikakutana na Stori za kwamba kuna Wafanyabiashara wa Ndizi pamoja na Maparachichi ndani ya Mkoa wa Mbeya wamekuwa siyo waaminifu katika biashara hiyo.
Kawaida ndizi zinapokomaa huwa zinavunwa na kuvundikwa kwenye sehemu yenye joto ili ziweze kuiva na kuwa tayari kuliwa.
Siku za hivi karibuni Wafanyabiashara wasiyo waaminifu wamebuni mbinu mpya ya kuivisha ndizi kwa njia ya kutuma kemikali.
Wafanyabiashara hao wamekuwa wakituma kemikali hizo ambazo huivisha ndizi Kwa muda mfupi tofauti na utaratibu wa kuzivundika.
Nimefika kwenye Soko Kuu la Ndizi “Kiwira” lililopo Wilayani Rungwe, Mbeya, nikapiga Stori na baadhi ya Wafanyabiashara ambao walidai kutumia kwao kemikali katika kuivisha ndizi kumeongeza kipato chao cha kila siku.
Wanadai kemikali hizo husaidia kuivisha ndizi kwa muda mfupi, wakiziweka kwenye matunda baada ya siku moja tu yanaiva vizuri kabisa, hivyo kuwafanya kuwa na Matunda yaliyoiva kila siku.
Matumizi hayo yanaendelea hadi kwenye Maparachichi pamoja na maembe ambayo bado hayajakomaa vizuri.
Mchezo huo umehamia kwenye masoko mbalimbali hapa nchini kama vile Soko la Matunda Soweto - Mbeya, Soko la Mabatini - Mbeya, Soko la Uyole na Soko la Sabasaba - Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga.
Mwamba sikuishia hapo nikataka kujua kemikali hiyo wanaipata wapi na inauzwaje, hapo ndiyo nikapatwa na mshangao baada ya kuambiwa kuwa hiyo dawa haipatikani madukani ila huwa wanainunua kwa njia ya magendo na inatoka katika nchi za Malawi na Zambia.
Swali linakuja kama hii kemikali inauzwa kwa njia za panya, Je, inausalama kwa Watumiaji wa hizo ndizi ambazo zinaivishwa?
Jibu ni hapana, Kemikali hiyo ni hatari kwa afya ya walaji wa Matunda hayo ambayo yameivishwa Kwa kemikali hiyo.
JE, VIONGOZI WA MASOKO WANAJUA JAMBO HILI?
Baadhi yao wanadai wanasikia tu taarifa hizo mtaani ila hawajafanikiwa kuwaona Wafanyabiashara wakituma kemikali hizo.
Hivyo, wanafanya upelelezi ili kujua ni Wafanyabiashara gani ambao wanatumia kemikali hizo ambazo zimekuwa hatarishi kwa afya ya Binadamu.
KIAFYA HII KEMIKALI INA ATHARI GANI?
Nimefanikiwa kupata Kemikali yenyewe kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara ambaye aliniuzia kimfuniko kimoja cha kopo la maji la Lita moja Kwa kiasi cha Tsh. 2,000 tu, na akaniambia natakiwa kuchanganya na maji kiasi cha lita 20.
Kemikali hizo ni Calcium Carbide na Etefon 480 zinachanganywa na maji ambapo zinatoa gesi inayotumiwa kuivisha matunda.
Basi ikanibidi nimtafute bwana afya na kumuonesha kopo la kemikali hiyo na kutaka kujua hiyo ina athari gani kwa binadamu, majibu niliyopewa ni kwamba kemikali hizo hutumika katika utengenezaji wa Mbolea na zinaweza kusabisha magonjwa mengi yakiwemo Saratani.
Afisa na Mtaalamu wa Afya anashauri tuwe makini tunaponunua ndizi, anazotaja kuwa zimeathirika kwa kiasi kikubwa.
Anasema kwa kawaida, ndizi zinapaswa kuiva kati ya siku tatu hadi nne, zinapovunwa zinakuwa za kijani lakini ukiona ndani ya muda wa siku moja tu unakuta zimeiva unapaswa kuwa na wasiwasi.
Ndizi zilizoivishwa kwa njia ya kuzivundika huwa zinakuwa na rangi ya njano na ukijani kwa mbali lakini zilizoivishwa kwa Kemikali huwa zinakuwa za njano kabisa, hivyo, tunapaswa kuwa makini pindi tununu hapo ndizi.
Mwanongwa nawakumbusha tu viongozi wa Serikali hasa katika Mamlaka za Afya kupita Kwenye maghala ya Matunda na kufanya ukaguzi maana huko ndiko mchezo wa kuivisha Kwa kemikali unafanyika.
Siku kadhaa zilizopita kulitokea madai kama hayo ya wafanya biashara ya ndizi soko la Mabibo, Dar kutumia gas maalumu iitwayo Ethylene ili kuivisha ndizi kwenye makontena. Baadae TBS wakatoa taarifa kuwa hiyo Ethylene haina madhara kiafya. Kitu cha kujiuliza kama ni kweli hiyo Ethylene haina madhara hao wanaoitumia watashindwaje kutumia hiyo kemikali ya etefon? Au TBS watatoa ufafanuzi mpya kuhusiana na hii etefon kuonyesha kuwa au kutokuwa na madhara kiafya?
Dadek 🤔Maziwa mgando wanaiweka Amira ili kidumu kijae chap...Lita Tatu kinafull Lita tano
HahahahahahaVipi yale machungwa na mananasi pale segere mbona ni machachu vile wakati yanaonekana yameiva? Naambiwa nisinunue pale nikanunue korogwe ndiyo yameiva kihalisia, ya segere yanaivishwa kwa moto! Kumbe wengine nao huivisha matunda kwa kemikali? Ndio maana kuna matunda yameiva lakini ladha yake si ya kawaida!
Lucas Mwashambwa ChoiceVariable TlaatlaahIngewekana tupate majibu kwa Luca,Choice,na babu Tlaatlaah
Duuh,Kemikali za kuivisha Ndizi zimehamia katika matunda mengine, Wataalam wa Afya watueleze kama ni salama
Wa tag TBS ambao walisema kwamba Hazina shida
Lazima tuwatag na wajuaji wetu wa humu.Wa tag TBS ambao walisema kwamba Hazina shida