TozzyMay
JF-Expert Member
- Dec 30, 2023
- 482
- 1,787
Wewe ni mwehu kweli sasa tangu lini watu wa jinsia tofauti wakabakana?
Nini maana ya kubakana?
Ikiwa KUBAKA ni kitendo ya kushika mtu kwa nguvu na kuzini naye?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mwehu kweli sasa tangu lini watu wa jinsia tofauti wakabakana?
Hiyo 50/50 huwa iko applicable kwenye kugawana Mali tu basi baada ya talaka.17/17 application ya 50/50 imegoma.
Wapi hii 50/50 itatenda haki?
Au hakuna 50/50 ni rumours tu?
Sahihi kabisa, maana kwa kuangalia tu hapo Hiyo kesi imepelekwa kwa assumptions Zaid kwamba wa kiume ndio alibaka, Kwanin wasingefanya reversal assumptions???Kama wote ni "watoto" kwanini tusiseme huyo wa kike ndiye amembaka huyo wa kiume na kujisababishia mimba?
Tuwe serious kwenye mambo mengine.
Mkuu kosa la ubakaji lina dhamana.Nijuavyo kosa la ubakaji halina dhamana achilia mbali kifungo cha nje halafu mwanafunzi
Mkuu kwa sheria zetu ni mwanaume tu ndo anaweza kubaka! Hata shangazi la miaka 40 nilibemenda mtoto wa miaka 16 huwezi sema mwanamke amebaka.Kama wote ni "watoto" kwanini tusiseme huyo wa kike ndiye amembaka huyo wa kiume na kujisababishia mimba?
Tuwe serious kwenye mambo mengine.
Ungemfunga nani sasa kati ya hao. Haki ilikuwa kuwafunga wote.Mkuu kosa la ubakaji lina dhamana.
Kuhusu kifungo imetokana na mbakaji kuwa " under age". Yaani mtoto kabaka mtoto. Ijapokua ningekua hakimu ningemfunga hata miaka miwili jela ya watoto!
Huyo kijana wa miaka 17.Ungemfunga nani sasa kati ya hao. Haki ilikuwa kuwafunga wote.
Nani alitengeneza hizo sheria na kwa makusudio gani? Kuwaruhusu wanawake kuwafanyia ubaki(child molestation) watoto wadogo au?Mkuu kwa sheria zetu ni mwanaume tu ndo anaweza kubaka! Hata shangazi la miaka 40 nilibemenda mtoto wa miaka 16 huwezi sema mwanamke amebaka.
Sheria za jamhuri zinatafsiri vipi neno kubaka?View attachment 3147731
Nini maana ya kubakana?
Ikiwa KUBAKA ni kitendo ya kushika mtu kwa nguvu na kuzini naye?
Nawaza tu hapa huyo mtiaji mimba angekuwa ni mwalimu!! Watu wangevurugwa kweli kweli!
Inaweza kuwa kosa lingine kisheria lakini sio "ubakaji". Sheria za zamani hizi zinatambua ubakaji wa upande mmoja....Nani alitengeneza hizo sheria na kwa makusudio gani? Kuwaruhusu wanawake kuwafanyia ubaki(child molestation) watoto wadogo au?
Kwa hizo perceptions zako HUFAI KUWA HATA WAKILI WEWE.Huyo kijana wa miaka 17.
Ni wakili zamani.Kwa hizo perceptions zako HUFAI KUWA HATA WAKILI WEWE.
Aisee 🙌🙌🙌Ni wakili zamani.
Mzaha huuKijana wa Miaka 17 ahukumiwa kifungo cha nje Miezi miwili kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi
Halikadhalika, Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 17 Mkazi wa Kijiji cha Kilambo, mwanafunzi wa kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Ikimba amehukumiwa kifungo cha nje miezi 12 pamoja na kumlipa fidia mhanga kiasi cha shilingi laki mbili [200,000/=] kwa makosa mawili kubaka na kumpa mimba mwanafunzi alilolifanya kwa binti mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Ikimba.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela na Mhe.Hakimu Paul Barnabas - SRM Oktoba 24 2024 na Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi Bihemo Mayangela Dawa. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (e) na kifungu cha 131 kifungu kidogo Cha pili (a) vyote vya sheria ya kanuni ya Adhabu pamoja na kifungu cha 60A kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya elimu mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 15, 2024 baada ya kumlaghai mwanafunzi mwenzie kuwa atamuoa baada tu ya kumaliza masomo yake.
Hukumu/Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu, wanafunzi wengine na vijana wengine wenye tabia na wanaofikiria kufanya vitendo kama hivyo kwa watu wengine, wanafunzi na mabinti wadogo.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana hasa katika utoaji ushahidi mahakamani ili kesi ziweze kupata mafanikio. Pia linatoa shukrani kwa vyombo vyote vya haki jinai kwa ushirikiano mkubwa unaotolewa ili kuhakikisha haki inatendeka dhidi ya washitakiwa/watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai.
Mbeya: Kesi 1072 zimefikishwa Mahakamani ndani ya Oktoba 2024
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na jitihada mbalimbali za kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hali inayopelekea kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali na kuwafikisha mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 jumla ya kesi 1072 zilifikishwa mahakamani ambapo kesi 195 zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kukutwa na hatia na kuhukumiwa vifungo jela huku kesi 751 bado zipo mahakamani zikiendelea katika hatua mbalimbali.
Miongoni mwa kesi zilizopata mafanikio mahakamani kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 ni pamoja na ile ya shambulio la aibu, kubaka na kumpa mimba mwanafunzi na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mbeya: Vitus Thadeo ahukumiwa kifungo cha Maisha Jela kwa kumbaka binti wa Miaka 8
Vitus Thadeo [26] Mkazi wa Mwasanga Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 08 mwanafunzi wa Shule ya Msingi na mkazi wa Mwasanga Jijini Mbeya.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Mhe.Scout Novemba 03, 2024 na Mwendesha mashtaka Augustino. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 130 na 131 cha sheria ya kanuni za adhabu, mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni, 2024 baada ya kumvizia na kumbaka mlalamikaji akiwa chumbani kwake.
Vile vile, Christopher Kidumba @ Shumita [55] Mkazi wa Kijiji cha Kanioga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumbaka binti mwenye umri wa miaka 08, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Kanioga.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbarali na Mhe.Hakimu Mwandumbya – SRM chini ya Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi Kombe Oktoba 25, 2024. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza vyote vya sheria ya kanuni ya adhabu mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 01, 2024 baada ya kumkamata kwa nguvu mlalamikaji na kisha kumbaka na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Sambamba na hayo, Pascal Aron [28] Mkazi wa Ilomba, Asajile Isack [30] Mkazi wa Sae na Anord Gaspa [27] Mkazi wa Ituha kwa pamoja wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha walilolifanya kwa Philipo Mwasomola [29] tingo wa gari, mkazi wa Soweto Jijini Mbeya.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Mhe.Hakimu Chuwa Novemba 01, 2024 chini ya Mwendesha mashtaka Emanuel. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 287 A cha sheria ya kanuni ya adhabu, ambapo washitakiwa walitenda kosa hilo Desemba 20, 2022 baada ya kumvamia Philipo Mwasomola [29] na kumkata kwa panga mikononi na miguuni na kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali mwilini na kuiba simu zake mbili pamoja na pesa kiasi cha shilingi 16,000/=.
Mbeya: Jela Miaka 20 kwa shambulio la aibu dhidi ya Mtoto wa Miaka Minne
Pia, Michael John Mwaisaka [42] Mkazi wa Kijiji cha Mwaya amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kumlipa fidia mhanga kiasi cha shilingi laki tatu [300,000/=] kwa kosa la shambulio la aibu alilolifanya kwa mtoto mwenye umri wa miaka 04 mwanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela na Hakimu Paul Barnabas - SRM Novemba 04, 2024 na Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi Bihemo Mayangela Dawa. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 138C kifungu kidogo cha kwanza (a) na kifungu kidogo cha pili (b) cha sheria ya kanuni za adhabu, mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 19, 2024 baada ya kumjengea mazoea mhanga na alitumia nafasi hiyo kumchukua kutoka kwa bibi yake aliyekuwa anauza ndizi karibu na kilabu bila bibi yake kujua kisha kwenda naye kwenye kichaka na hatimaye kumvua nguo na kumfanyia vitendo vya kingono.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Mkuu hatutumii hisia kufanya maamuzi, ni sheria ndo zilivyo. Mtoto wa miaka 17 ni "criminally liable". Yaani unataka kusema vitoto vya miaka 15-17 vifanye makosa ya jinai halafu viachwe tu!!!Aisee 🙌🙌🙌