Mbeya Kuna Mambo: Hebu Cheki Majina wanayopewa Watoto wa Kisafwa

Kwanza Wasafwa hawana "Mwa"....prefix hii n kwa Wanyakyusa2,we utakuwa upo Intern...ndo mana ata mawazo yako ya kungaunga
 
Mkuu si kweli kwamba wasafwa hatuna majina yanayoanzia na Mwa..... kuna majina kama "mwashadema", "mwandala", "mwaninga", "mwanzala"..etc

Ni kweli kabisa kuna baadhi yetu wasafwa huita majina "eti" kwasababu ya umaarufu...kuna watu huita majina kama "Newton", "Girsanov" etc.... Kwanini wanaita majina ya namna hiyo?.......kwasababu ya hao watu ni maarufu?....Binafsi, I have not researched on this.....
 
Mbeya ni Mkoa wenye Historia tata sana Tanzania, ni Mkoa wenye Makanisa Mengi sana lakini ni Mkoa ambao watu wake wanawindana kama Chui anapowindwa kwa maana Ngozi yake ni dili, lakini vile vile ni Mkoa ambao sasa ikifika saa Kumi na Mbili wakazi wake hujifungia ndani ili kuepuka kushambuliwa kwa Nondo kwa imani za Kishirikina.

Lakini nimekutana na Jambo la Ajabu ajabu sana juu ya hawa ndugu zetu Wasfwa ambao ndio wakazi wa Mbeya, wamekuwa wakiwapa watoto wao Majina mpaka unashangaa sana

Mfano wa Majina ya watoto ambayo niliyowahi kukutana nayo pale nilipokuwa niko zamu kwenye wodi ya watoto Rufaa

1: Frank Lampard Mwambulukutu ( hako ni katoto kadogo)
2. Scania Hundred
3: RPCMorogoro Mwakyoma
4: Rooney

Sasa Mtu unamwita mtoto wako RPCMorogoro kweli haya ni Mapenzi au

Napenda sana kusikia kutoka kwa Wasafwa naamini mko hapa Jukwaani

Kazi kweli, kwa mtindo huu nawashauri wanachama wote wa JF kukaa karibu na maziwa fresh maana sumu/uongo mwingine ni hatari, majina yote hayo uliyotaja ni ya kinyekyusa live hapo hakuna jina la msafwa. kuwa makini ktk kufanya study yako (kuepuka biasness)
 
Mkuu si kweli kwamba wasafwa hatuna majina yanayoanzia na Mwa..... kuna majina kama "mwashadema", "mwandala", "mwaninga", "mwanzala"..etc

Ni kweli kabisa kuna baadhi yetu wasafwa huita majina "eti" kwasababu ya umaarufu...kuna watu huita majina kama "Newton", "Girsanov" etc.... Kwanini wanaita majina ya namna hiyo?.......kwasababu ya hao watu ni maarufu?....Binafsi, I have not researched on this.....

Wewe msafwa wa wapi? unaonekana kutokujua majina yaliyotajwa hapo ni ya kinyaki?
 
kwenye sensa mmakonde ananiambia jina lake ANDIKA NIKUTOROKE, watoto wake Chapati ya Azam na mwingne Ukali wa Panga kinoleo
 
[QUOTE=Katavi;
Iringa ndio funga kazi.
Flatscreen mhagama
Blackberry sanga
Fisadi filikunjombe
 
Kazi kweli, kwa mtindo huu nawashauri wanachama wote wa JF kukaa karibu na maziwa fresh maana sumu/uongo mwingine ni hatari, majina yote hayo uliyotaja ni ya kinyekyusa live hapo hakuna jina la msafwa. kuwa makini ktk kufanya study yako (kuepuka biasness)

Scania Hundred nalo ni jina la Kinyakyusa?!!!
 
Hayo ni majina manne tu kati ya wanyakyusa takribani 1050000.

Rooney peke yake haiashirii unyakyusa kama ilivyo Scania Hundred, hujaweka uthibitisho kuwa hao ni wanyakyusa.

Kulikuwa na kiongozi wa juu jeshi la polisi anaitwa Absolom Mwakyoma isijekuwa umechanganya dawa na mtu akamwita kwa cheo, mkoa wake na jina la ukoo ukadhania ni jina la kuzaliwa.

Frank ni jina kikristo lenye asili ya uingereza vile vile Lampard ni jina kikristo lenye asili ya uingereza na kaikatazwi na wala si ajabu kumpa mtoto majina hayo mawili.

Nadhani jamaa ANAWATANIA Wasafwa kuwa wanaiga sana majina, yawe ya Magari, Watu maarufu wanaowasikia redioni/tv, na mpaka majina ya majirani zao Wanyakyusa...

By the way, uwa namkubali sana Mwanamuziki chipukizi wa Kisafwa aliyepewa na Wazazi wake jina la PETER AWILO, sijui kama jina la kwanza walichukua kutoka kwa PETER Tino ila ni wazi kuwa jina la pili walilichukua kutoka kwa AWILO Longomba, sasa hivi huyu kijana ni almaarufu kama Awilo wa Mbeya...

Mfano wa Majina ya watoto ambayo niliyowahi kukutana nayo pale nilipokuwa niko zamu kwenye wodi ya watoto Rufaa

1: Frank Lampard Mwambulukutu ( hako ni katoto kadogo)
2. Scania Hundred
3: RPCMorogoro Mwakyoma
4: Rooney

Napenda sana kusikia kutoka kwa Wasafwa naamini mko hapa Jukwaani
 
Mfano wa Majina ya watoto ambayo niliyowahi kukutana nayo pale nilipokuwa niko zamu kwenye wodi ya watoto Rufaa

1: Frank Lampard Mwambulukutu ( hako ni katoto kadogo)
2. Scania Hundred
3: RPCMorogoro Mwakyoma
4: Rooney
Sasa Mtu unamwita mtoto wako RPCMorogoro kweli haya ni Mapenzi au

Napenda sana kusikia kutoka kwa Wasafwa naamini mko hapa Jukwaani
Nimeishi Mbeya kwa muda wa kutosha lakini sijawahi kusikia majina hayo kwa kabila la kisafwa! Majina ya kisafwa yaliyozoeleka ni kama haya;
Mbwiga, Mwandambo, Ndambo, Nzunye, Shungu, Mbozyo, Ilongo, Shali, Tabu, Mwisyo, Shimba, Nzalu, Shogo, Ndele.
 
Hayo ni majina manne tu kati ya wanyakyusa takribani 1050000.

Rooney peke yake haiashirii unyakyusa kama ilivyo Scania Hundred, hujaweka uthibitisho kuwa hao ni wanyakyusa.

Kulikuwa na kiongozi wa juu jeshi la polisi anaitwa Absolom Mwakyoma isijekuwa umechanganya dawa na mtu akamwita kwa cheo, mkoa wake na jina la ukoo ukadhania ni jina la kuzaliwa.

Frank ni jina kikristo lenye asili ya uingereza vile vile Lampard ni jina kikristo lenye asili ya uingereza na kaikatazwi na wala si ajabu kumpa mtoto majina hayo mawili.

Asante mkuu kwa ufafanuzi, Ila marekebisho kidogo. Hakuna jina la kikristo hapa duniani. Frank na Lampard ni jina la kiingereza au ukipenda jina la kimaGharibi na sio la kikristo. Mkristo anaweza kuwa na jina lolote kama vile Mohamed, Asha, Raphael, Elizabeth, Mwakyoma ama Tukupasya. Hapa utakuta kuna majina yenye asili ya Mashariki ya kati, Magharibi, Afrika na kwingineko.

Hakuna jina la kiislam, kikristo wala kipagani. Tusiwe watumwa wa mawazo.
 
Majina yafuatayo ni ya kikristo yenye asili ya kinyakyusa Tupokigwe, Tuntufye, Asajile, Gwandumi, Nkundwe, Lugano, Gwalugano, Nsajigwa, Nsaji etc. Huwezi kukuta Mnyakyusa Muislamu au Mpagani anaitwa majina hayo
 
sikumjjbula polisya mwaiseje,ambumbulwisye mwampondele,ikupilika mwasakifya,NAPITA TU
 
Wewe msafwa wa wapi? unaonekana kutokujua majina yaliyotajwa hapo ni ya kinyaki?

Mkuu Mbugi!
Mimi ni msafwa wa Mbeya mkuu.....Nilichoandika mimi hapo juu ni kutaja majina ya wasafwa yanayoanzia na "mwa" (kumjibu ndugu aliefikiri hakuna majina ya wasafwa yanayoanzia na "mwa"). SIJAZUNGUMZIA majina yaliyotajwa na mtoa maada kama ni ya kinyakyusa au ya kisafwa...Majina niliyoyataja mimi ni ya kisafwa ILA yanaweza kupatikana kwenye kabila jingine. Of course, kuna majina yanayotumika kwa wasafwa pia na wanakyusa; mfano Ambele.
 
Watani zangu Wasafwa taratibu jamani Msije Mkanimeza hayo niliyoandika jamani ndiyo niliyoyaona nadhani ni kawaida ya hii Jamii kuita watoto wao Majina ya Watu Maarufu au hata Majina ya Ofice wazazi walizowahi kufanyia kazi Mfano kuna Mtu amemwita Mtoto wake jina la TAZARA sasa unaweza ukafikiri ni utani ha ha ha
 
Nimeishi Mbeya kwa muda wa kutosha lakini sijawahi kusikia majina hayo kwa kabila la kisafwa! Majina ya kisafwa yaliyozoeleka ni kama haya;
Mbwiga, Mwandambo, Ndambo, Nzunye, Shungu, Mbozyo, Ilongo, Shali, Tabu, Mwisyo, Shimba, Nzalu, Shogo, Ndele.

uko sawa kabisa.
 
Hii inanikumbusha utani niliotumiwa kwenye simu yangu ya mkononi; ambao na unukuu "Umeipata ya Mbeya ya watu Sensa kutoka Dar walivyopata tabu Mbeya? Kwenye familia moja,
Jina lako mtu wa kwanza Mzee: Naitwa Ambanile Mwakipumbu,
Mama naitwa Amfugile Mwakivuzi,
Watoto:
1. Antombile Mwakikuma,
2. Amfilile Mwakikundu
3. Anyonyile Mwakisimi.
Ingekuwa wewe ungefanyaje?
 
Back
Top Bottom