Mbeya: Mahakama imeahirisha kusoma hukumu ya Mdude Nyagali hadi Juni 28, 2021

Kwa muda huu saa10:30 asubuhi msafara wa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe umewasili hapa katika viwanja vya Mahakama Kuu Mbeya kusikiliza hukumu ya mwanachama wao Mdude, ambaye alishitakiwa kwa makosa ya madawa ya kulevya, uhujumu uchumi nk...
Mambo mawili makubwa nayaona hapa.Jambo la kwanza mahakamnai ni mahali pa heshima kuu kwa maana ya kuwa watu wanakwenda kuitafuta haki.

Hakimu ni mtu mkubwa sana kwani uamuzi wake unaweza ukaamua hatma ya binadamu mwingine.Kitendo cha HAKIMU kusema hukumu haitasomwa kwa sababu zilizo NJE ya uwezo wake ni cha kutiliwa mashaka ukiangalia hayo mawili yaliyotangulia.

Jambo la pili linahusu waandishi wa habari na hata Chama chenyewe cha Chadema.Hapakuwa na ripoti ya usikilizwaji wa kesi kama wale wa zamani tulivyoshudia wakati wa kesi ya kutaka kupindua nchi 1983 ambapo kila siku maendeleo ya kesi,mahojiano kati ya mawakili angalau yalitupa mwanga wa kujua kinachoendelea.

Humu ndani JF kesi ya mwanzilishi wa JF ilikuwa ikiripotiwa kila siku.Jambo hili linatupa shida ya kuhisi kuwa ni nani mkweli,Nyagali au serikali?
 
Mungu wa Ibrahim na Yakob na amsimamie - tunajua kosa lake ilikuwa ni kumkosoa mtukufu ndiyo kupewa haya makosa makubwa ili kumnyamazisha ili iwe funzo kwake yeye na wengine.
Amen
 
Amen.
Ubarikiwe mkuu.
 
Watu wameingia gharama kutoka mbali halafu wana ahirisha kirahisi hivyo jamani?

Bongo aisee duh
 

hahaha chadema wakianza reality tv itanoga sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…