Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Majaji wamerahisisha rufaa sana.Kuwa mvumilivu Mwabukusi na wenzie watashinda rufaa mzee wangu.Shangilia kwa machale
Kawadanganye wajinga wenzio.

Rufaa haijawahi kuwa kikwazo cha kesi yoyote Tanzania.

Hao mawakili wenu uchwara wanataka michango yenu tu, wanaelewa wazi kuwa IGA haiwezi kuamuliwa wala kutenguliwa na mahakama yoyote ya Tanzania, pia wanaelewa kuwa hawawezi kubatilisha tamko lolote la bungeni, watunga sheria wao.

Waambieni waende ICSID, nawashangaa mnajihangaisha na mahakama ambayo haiwezi kuamua mambo ya IGA.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Hukumu ya kisanii, majaji wanataka vifungu vyenye makosa virekebishwe, badala ya kutoa amri waseme ule mkataba wa IGA ni batili, hii ngoma lazima iende mbele zaidi, wajinga wacha waendelee kushangilia wasichokijua.
Mnapoteza muda tu, wawekezaji wanaanza kufunga mitambo bandarini, waambie wapenda magumashi waliokutuma kwamba chuki imeangukia pua.
 
Hiki kitu bado mbichi sana. Serikali lazima ikubali maoni ya wananchi.
 
Mwabukusi kapiga makelele na mapovu yamemtoka kwa wingi hatimaye kafika mwisho wake.
 
Wamuombe radhi Rostam Aziz kutoka na waraka wao.
 
Watu tunaanza bishara za kunenepesha kondoo tuchinje tupeleke kondoo kwa container Dubai, Muscat na Jeddah, wao waanatuletea kauzibe. Akili zao finyu sana. ni wakuchapwa viboko hadharani hao.

Wanafikiri bandari ni kushusha mizigo tu? Ina mlolongo wa mambo yaliyofunguka. Mie nasema reli zote zilizokufa zitafufuliwa na zitafanya kazi na hazitoshi.

Kuna container million mbili kwa mwezi zinatakiwa zitoke congo na Zambia kwenda nje kuwa refined.

Zambia na Congo walikuwa wajinga miaka yote wanayayusha shaba yao na kuvitengeneza vinoo vinaenda China, kumbe shaba ile ina madini mengine kibao, walilala. Sasa wameingia mikataba na Japan, ipelekwe kule makinikia na wao wenyewe wasimamie, inachenjuliwa kila aiana ya madini yanauzwa kivyake. Sasa unafikir makinikia yote hayo yatapita wapi?

Mie nakwambia reli zetu zote na malori yote hayatoshi. Hawaelewi kuwa hii hatujamakiza tushaanza reli nyingine ya kutokea Mtwara kwenda mpaka Zambia huko.

Mama ni kichwa tofauti kabisa kile, wamuone vilevile mkimya kimya. Ma shaa Allah anaona miaka 100 mbele.

Mama kishamkubalia Ulega kuweka Guest za mifugo yetu ya kusafirisha.
 
Hii kauli inaonesha namna mioyo ya majaji wetu ilivyohangaika na hili jambo. Wakafika kiwango cha kuchoka, kushindwa kufanya lolote.
Mapunziko mema Majaji. Mmefanya mlichoweza katika ubinadamu wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…