Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

mnao pinga huu uwekezaji ni kwamba mmezoea wizi ukwepaji kodi na kila ana ya hujuma zifanywazo bandarini hivyi mnaona kabisa kiama chenu kinakuja mtakosa ulaaji kaeni kimya dawa iwaingieeeeeeeeeeeee

Kwamba huo uwekezaji ukija wizi na ukwepaji kodi utapungua? Dream on
 
Kuna mdau mmoja anaitwa kalamu, anahangaika mno kupambana na serikali na leo ameangukia pua kwa mara nyingine.

Kupambana na adui usiyemuona ni kazi ngumu sana, hujui lini atakupa mapigo na yatakuja kwa njia zipi.
 
Ningeshangaa sana kama hii kesi isingetupiliwa mbali. Nilishawahi kuandika humu humu JF kuwa hakuna kesi hapom, ni kuitupilia mbali.

majaji waametumia hekima sana kuwasikiliza, lakini mimi nilisema kwa madai yao yale, siku ya kwanza ingetupiliwa mbali.

Ningeshangaa sana, ningewaona majaji wa ajbu duniani. Lakini ni vyema kabisa, ni majaji wenye hekima na wanafahamu wanachokifanya.
 
Kuna mtu anaitwa kalamu yumo humu JF kapambana mpaka akawaalika wanasheria kutoka Kenya kujaribu kujenga hoja kwamba serikali ya TZ imekosea kuingia ubia na Dubai katika suala la DP World!, yaani kwa akili yake anashindana na serikali ya JMT halafu anatagemea kupata ushindi!.

Kuna mali nyingi sana huko Congo, Rwanda, Zambia zote hizo zinasubiri bandari yetu na reli ya kisasa pamoja na bandari yenye huduma za teknolojia za hali ya juu.

Yaani tupoteze fursa zote hizo kwa akili za kipuuzi tu za wachache kati yetu!. Rais Samia analo lengo zuri la kuendeleza pale alipoishia hayati JPM. Ndio maana ya maneno KAZI IENDELEE.
 
Kwamba huo uwekezaji ukija wizi na ukwepaji kodi utapungua? Dream on
Utpunguwa kwa asilimia kubwa sana, utashangaa.

Mifumo ambayo serikali inataka iwekwe hapo ni ya udhubiti live 24 hours.

Container toka linapotoka huko linajulikana limepakia nini na mpaka litapofika vilivyomo ndani vitajulikana kwa remote, bila hata xray.


Unajuwa maana ya DP Worls kuwa (logistics chain) wanaanzia kuanzia mzigo unapofungwa, unapopakiwa mpaka njia nzima unapopita upo chini yao mpaka destination?

Ukiielewa maana yake utaelewa kwanini kanisa ni mstari wa mbele kupiga kelele.

DP World ukiwapa go ahead na ukiwapa kazi hiyo, mpaka kazi ya TRA wanaifanyia ukaguzi wa mzigo hukohuko kabla haujateremshwa hapa na hakuna longolongo. Hapa mwenye mzigo unaambiwa uoneshe anwani yako tu, mzigo unafikishwa mpaka kwako.

Itategemea na tutawapa kazi ipi na ipi?
 
Bilashaka majaji wamekula mpunga toka DPW ndiyo maana
 
Kwa hitimisho la kuona Sheria zimevunjwa Ila hawezi kusema lolote kwa kua waliofanya hayo makosa nao ni mhimili!
 
Kama mahakama inashindwa kutoa haki inayoonekana kilichobaki ni kufanya kama Niger, Mali, Burkina Faso na kwingineko ni suala la muda tu
 
Majaji tuliokuwa nao walishatangulia mbele za haki wote sasa hivi hatuna majaji hawa waliopo ni waajiriwa wa rais na lazima walipe fadhila kwa kesi yoyote inayomuhusu mtoa fadhila.

Hawa majaji wa sasa mbona kula rushwa hata kwenye vyesi vingine visivyo ihusu serikali ni jambo la kawaida sana kwao tofauti kabisa na majaji wa zamani waliokufa maskini kwa kutetea msimamo wao wa kuzingatia sheria na haki.
 
Kama mahakama inashindwa kutoa haki inayoonekana kilichobaki ni kufanya kama Niger, Mali, Burkina Faso na kwingineko ni suala la muda tu
Kwa jeshi gani, unajua mfumo au muundo wa jeshi la Tanzania ulivyo lakini. Katika Tanzania afisa yeyote wa jeshi wakati wowote anaweza akapewa uteuzi kuwa waziri, mkuu wa mkoa au wa wilaya nk.

Sasa je unaweza kupewa moja ya nyadhifa hizo kama wewe sio mwanachama wa ccm? Jiulize hilo swali kisha ujijibu mwenyewe.

Wakati mfumo wa vyama vingi unarejeshwa Tanzania kwenye mwaka 1992 watu walidanganywa kwamba vyombo vya usalama havitakuwa na mafungamano na chama chochote cha siasa na kwa kuwa kwenye nchi wajinga ni wengi basi wakaamini kumbe ilikuwa ni uongo wa mchana kabisa.

Sasa huyo afisa wa kupanga njama eti ya kuipindua serikali ya ccm atatoka kikosi gani cha jeshi katika nchi hii...????
 
Mahakama ni muhimili mwingine kama serikali na bunge. Kama serikali na bunge wamekubaliana uwekezaji huo, je mahakama ni kitu gani kipingane na wenzake ndani nchi moja iliyoamua kuingia mkataba huo? Anyway, huo mkataba haukubaliki hata kama mihimili hiyo imeamua kuungana dhidi ya wazalendo wanaopinga mkataba huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…