A
Anonymous
Guest
Ndugu wana JF, wakazi wa Mbeya, Mbalizi na maeneo yake hadi Ifisi, tunapitia changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji majumbani.
Ni takribani wiki tatu sasa maji hayajatoka, lakini cha kushangaza, leo maji yametoka wakati Makamu wa Rais alipowasili Mbeya. Hali hii inazua maswali na kuwafanya wananchi kuhisi kuwa huduma ya maji inatolewa kwa utaratibu usioeleweka.
Ombi langu kwa Makamu wa Rais: Kesho, naomba suala hili lifuatiliwe kwa kina na wahusika wa idara ya maji katika maeneo ya Mbeya na Mbalizi wawajibishwe endapo itabainika kuwa wamezembea au wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Wananchi tunateseka sana kutokana na kukosa huduma hii muhimu.
Hali hii pia inachafua taswira ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwa wananchi wanatarajia serikali na taasisi zake kuhakikisha wanapata huduma muhimu kwa wakati.