Uchaguzi 2020 MBEYA MJINI: Mkimchagua Sugu mtakuwa mmeshamchagua Tulia, mtakuwa na wabunge wawili

Uchaguzi 2020 MBEYA MJINI: Mkimchagua Sugu mtakuwa mmeshamchagua Tulia, mtakuwa na wabunge wawili

KAWETELE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2015
Posts
700
Reaction score
1,674
Huyu Tulia akson Tangu ateuliwe na Magufuli kama "mbunge wa Dar" (Ndipo alipo pigia kura ya meya), alianza maandalizi ya kupata ubunge wa kuchaguliwa, mwanzoni nguvu zote alizielekeza huko kwao alikozaliwa ila baadaye akaona isiwe tabu akahamia Mbeya mjini kujaribu kumtoa Sugu.

Akaanzisha ujenzi maeneo ya Itezi ili aonekane mtoto wa Mbeya mjini. Akaanzisha taasisi nyingi nyingi za kutoa msaada kwa miaka yote mitano alikuwa busy kubomoa ngome ya Sugu akisaidiwa kwa ukaribu na polisiccm.

Hata ziara za jiwe akageuka ndiye msemaji wa wana Mbeya mjini.

Sasa ni mwaka wa uchaguzi. Pale yupo Sugu ambaye ni charismatic " ana bahati ya kupendwa" pamoja na mapungufu yake usela usela.


My take:
Ili taasisi uchwara za mikopo na kugawa T-shirt kwa wapiga debe, ili wana Mbeya muendelee kufaidi vibajaji vya bure, ili muendelee kumuona kwenye vipaimara, ili aendelee kugawa gawa hela kwenye stendi, ili aendelee kuwa mtu wa watu dawa ni moja tu, ni kumpa Sugu tena miaka mingine 5 na hii mtakuwa mmevunja record ya jimbo hilo kuongozwa na mtu kwa miaka 15 tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
 
Tulia alidanganywa sana na mtu aliyemwambia aache kwao anakojulikana Rungwe Tukuyu kijiji cha Bulyaga aende kuhangaika mbeya mjini asipojulikana.
Nani alimdanganaya dada yetu??

Angekuwa huko kwao anakopendwa mno angekuwa ashapita bila kupingwa Kule Tukuyu anakubalika sana.

Hapo mbeya mjini alitumwa kubomoa na kuvunja ngome ya CHADEMA na Sugu kwa kura halali kabisa hawezi kushinda.

Wana mbeya si wajinga wanamlia fedha zake na miradi yake lakini hawampi kura Naona Damu itamwagika sana Mbeya mjini.

Tulia ulidanganywa dadaangu.
 
Sugu tunamsubiri msimu wa fiesta.

Bungeni awaachie watu makini
 
Hapa ndio sugu alipofikia
huyu dada wa watu mataga mmemuingiza chaka [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
20200912_081929.jpg
 
Back
Top Bottom