Upinzani Tanzania bado sana kwa maana ya capacity. Serikali haiundwi kwa mtu mmoja mmoja eti Sugu sijui nani. Inahitajika taasisi na watu wenye weledi. Sasa wapinzani wakipewa nchi wataitisha ajira ambapo wanaCCM wanaomba au watachukua expatriates? Sielewi hata wanawezaje kuongoza nchi like legit. Natafuta sentensi inayoonyesha wanaweza katika kichwa changu na sioni kabisa. Napenda mabadiliko lakini hatuwezi kumwondoa pilot kisha tukamweka mkulima na safari iendelee. Nafikiri wenye uwezo wa tathimini watakubaliana nami kuwa ni fact. Tunahitaji mabadiliko ila je tuna watu wa kutosha kuongoza na kuunda serikali madhubuti? Ondoa hawa viongozi wote wa upinzani halafu tafuta chini yake kuna kina nani? Waendesha bodaboda, mama lishe etc. Kwa ujumla utaona ukitoka kwa viongozi ni moja kwa moja wanachama. Chama kitaweza kuongoza na kuunda serikali ikiwa chini ya viongozi kuna tabaka la kutosha la wataalamu na kisha baadae wanachama wa kawaida. Shame, shame Tanzanian politics! CCM jengeeni uwezo upinzani jamani! Sasa hata hawa wapinzani tena wanarudi kulekule tena. Wameona nini? Think broadest! Mawazo yangu tu anyhow.