Mbeya: Mtu mmoja auawa kwa kukatwa na panga wakigombea goli lilokataliwa uwanjani

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Anyulise Mwamkisu (49) ameuawa kwa kukatwa na mapanga, katika uwanja wa mpira wa miguu wa Kijiji cha Mofwile Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, kulikokuwa na Ligi ya mpira kati ya Nyuki FC na Mofwile FC na kuibuka kwa vurugu baada ya timu moja kushinda goli na kukataliwa, hali iliyoibua vurugu.

Hayo yamebainisha na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyela mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Lwitiko Kibanda wakati akijibu maswali ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Juma Homera huku akiongeza kuwa katika tukio hilo wapo waliojeruhiwa.

Your browser is not able to display this video.
 
Lazima tutambulike,hata kwa kukatana mapanga...dunia itatutambua tu🥴
 
Mpira ni ushetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…