Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Tawi la Machinjioni, Kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya, Michael Kalinga amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, Desemba 3, 2024 na mwili wake kukutwa Kata ya Mkola.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa amesema wamepata taarifa za mauaji ya Kalinga na wanaendelea kuzifanyia kazi.
Katibu wa CCM Wilaya Chunga, Charles Jockel akizungumza na Mwananchi amesema amepokea taarifa hizo leo Jumanne asubuhi kutoka kwa uongozi wa CCM Kata ya Makongorosi.
"Haijulikani alikuwa anakwenda au kurudi Makongorosi maana mwili wake umekutwa eneo la kuelekea Kata ya Mkola," amesema Jockel.