Mbeya: Mzazi amzawadia mwanae Sungura kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mzazi Daniel Kapangala amemzawadia mwanae sungura wawili ambao ni jike na dume katika mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Tembela iliyopo Kata ya Itewe, Halmashauri ya Mbeya, Shule hiyo inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
WhatsApp Image 2026-10-05 at 18.10.52.jpeg
Kapangala amesema ameamua kumpa mwanae zawadi hiyo ikiwa ni sehemu ya kumhamasisha kujifunza na kuingia katika shughuli za ufugaji, akiamini kuwa ufugaji unaweza kuwa fursa ya kujiajiri na kujipatia kipato.

Amesema zawadi hiyo inalenga kumjengea mwanae utamaduni wa kujifunza shughuli za uzalishaji, huku akimtaka kuitunza na kuendeleza ufugaji huo.
 
Mboga anaenda kuchinjaa tyu tamuu io
 
Sasa si angempa hao sungura nyumbani. Mtoto yuko kwenye mahafari unampelekea sungura badala ya keki na mataji! Halafu jamaa ni kijana ila mambo yake ni ya kizee kunizidi hata mimi.
 
Back
Top Bottom