Mzazi Daniel Kapangala amemzawadia mwanae sungura wawili ambao ni jike na dume katika mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Tembela iliyopo Kata ya Itewe, Halmashauri ya Mbeya, Shule hiyo inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kapangala amesema ameamua kumpa mwanae zawadi hiyo ikiwa ni sehemu ya kumhamasisha kujifunza na kuingia katika shughuli za ufugaji, akiamini kuwa ufugaji unaweza kuwa fursa ya kujiajiri na kujipatia kipato.
Amesema zawadi hiyo inalenga kumjengea mwanae utamaduni wa kujifunza shughuli za uzalishaji, huku akimtaka kuitunza na kuendeleza ufugaji huo.