Mbeya ilipewa Jiji kwasababu ya uwingi wa watu na mapato, ila ni mji ambao haujapangika vizuri na haujajengwa vizuri. kwa wale wenzangu na mimi wenyeji wa huko, ukiishi mbeya walau miaka miwili haujajenga, unadharauliwa sana, hivyo watu wengi mbeya wamejenga nyumba zao, lakini sasa ujengaji wake kwasababu kila mtu alalazimisha awe na nyumba, regardless na kipato alichonacho, kuna nyumba hazina mpangilio kabisa wala mfanano. nawezasema pamoja na kwamba DODOMA ni padogo, ila pamepangika na ni pazuri kuliko mbeya. mbeya mtu anajenga apendavyo na nyumba ya aina apendayo, ya kudunduliza, ya kitajiri, ya kimasikini twende...alimradi awe na nyumba. na wanyakyusa wanavyodharau mtu anayepanga.....
but kimapato, kuna biashara kubwa sana. business centres kama SIDO/MWANJEWA/KABWE ni chache sana kwenye miji mingi Tanzania ukiondoa DSM. pale utapata kila kitu ambacho ungepata dsm na kwa bei nzuri. kuna watu wanafanya biashara pale ya hali ya juu. population pia ni kubwa inasapoti biashara ndio maana ilipewa hadhi ya jiji.