DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 4,446
- 8,215
Mimi natoka mbeya lakini nimeishi sana Arusha nimeona nyumba za tope Arusha mpaka nikaona Kumbe home Kwetu mbeya ni ulaya tupu, kama huamini nenda kule Arusha Daraja mbili mitaa ya Bongonyoo, Daraja mbili nenda kule sinoni mitaa ya Mombasa raha utaona maajabu.... Dar es salaam nimesoma na kuishi sijaona Cha ajabu, mitaa ya msewe, ukonga Mombasa, siju,lmalamba mawili kote ni ujinga mtupu...Huu ni ukweli mchungu ambao wana mbeya wengi hatutaki kuukubali.Mbeya inahitaji transformation kubwa sana kuendana na hadhi kama majiji mengine makubwa kama DSM,Mwanza ,Arusha na Dodoma.Tukiendelea kukaza fuvu nakuamini kua mbeya iko vizuri kama majiji mengine tutaendelea kubaki nyuma milele na vimikoa vidogo vitaibuka na kutupita.Tuache kujiongopea na kujipa moyo wakati ukweli tunauona uko dhahiri.Wenzetu wote wana Malls,mbeya hamna hata moja,Wenzetu wana hotels zenye hadhi na swimming za kutosha ,mbeya hotel zenye hadhi na zenye swimming siju kama zipo na kama zipo zenye swimming hazizidi tatu.Wenzetu wana viwanja ving vikali vya starehe lakini mbeya viwanja vya maana sijui kama vinazidi vitatu.Miundombinu wametuacha mbali sana,Majenngo ya kisasa wametuacha mbali sana.Hata ustaarabu (civilization) wametuacha mbali sana,maana mbeya mpaka leo bado tuko zama za mawe za kale tunajenga nyumba za matofali mabichi tena mjini na wakati wenzetu wameshahama huko.
Km unataka unyama wa mjini nenda USA au baadhi ya nchi za ulaya... Wewe ni mmama charii angu. Imeisha iyo.