Mbeya si Green City, ni Dark City; kwa sehemu kubwa mji haujapangika vizuri

Mimi natoka mbeya lakini nimeishi sana Arusha nimeona nyumba za tope Arusha mpaka nikaona Kumbe home Kwetu mbeya ni ulaya tupu, kama huamini nenda kule Arusha Daraja mbili mitaa ya Bongonyoo, Daraja mbili nenda kule sinoni mitaa ya Mombasa raha utaona maajabu.... Dar es salaam nimesoma na kuishi sijaona Cha ajabu, mitaa ya msewe, ukonga Mombasa, siju,lmalamba mawili kote ni ujinga mtupu...


Km unataka unyama wa mjini nenda USA au baadhi ya nchi za ulaya... Wewe ni mmama charii angu. Imeisha iyo.
 
Wapumbavu wa sisiemu watabisha siyo mbeya tu ni nchi nzima miji ipo hovyo
 
Mbeya huwezi linganisha na mji kama Arusha au mwanza, mji kama Arusha unaweza kuwa mdogo na population ndogo lakini barabara, mahoteli makubwa yenye hadhi ya nyota tano, utalii, ma- supermarket makubwa, ofisi za kimataifa zinaifanya Arusha kuwa juu zaidi ya mbeya, sasa mji gani hauna hata barabara hata Moja ya njia nne? nao unaita jiji, kweli??
 
ni kweli uliyosema lakini ni nyumbani kwetu

nimetembea mikoa kadhaa naonaga afadhali mbeya yetu tukiweza kuboresha bara bara tu na mipango miji miji tutakuwa tumetisha sana

mbeya huwezi fananisha na singida,tabora,kigoma,lindi,mara,mtwara,songea,na maeneo mengine kiufupi sisi nchi yetu ni maskini kwa ujumla full stop
 
Ulivyocomment Kwa hasira inaonesha jinsi gani umegundua ukweli sema tu umeamua kukaza fuvu
 
Kwahyo kutoka ulikotoka ukaona bora kitu kingine ni kuiongelea mbeya vibaya? Hovyo kabisa
 
Shida kubwa ya mbeya ni mipamgo miji na kwa Sasa lazima wakubali gharama kubwa itumike kuwahamisha watu wenye nyumba za hovyo katikati ya mji ili kuongeza Barabara za mitaa na mpangilio na eneo la Kilimo libadilishwe maana saiz mbeya imejaa ndo maana watu wanavamia milima na hii ishu imetoa fursa kwa mkoa wa njombe kuanza kutengeneza mji mkubwa wa viwanda na biashara nyanda za juu kUsini mkoa wa njombe umepata SoMo flan kutoka dodoma kuwa wanauwezo wa kuwa na mji mkubwa nyanda za juu kulingana na jiografia ya mikoa ya nyanda za juu kUsini ilivyo mkoa wa njombe una eneo kubwa lenye uwezo wa kuhimili viwanda vingi kutokana na uwingi wa rasilimali na hii imepelekea kujengwa kwa viwanda vya madawa,vyuma ,parachichi nk pia Kuna ujenzi uwanja wa Kanda wa ndege na soko la mazao la Kanda .vilevile ukubwa wa eneo tayari mbeya imesha banwa anzia inyara hadi mbalizi utaligundua Hilo mji hauwez kuruhusu project kubwa kama industrial park pote pameenea makazi nk"tic njombe - YouTube" https://m.youtube.com/results?sp=mAEA&search_query=tic+njombe
 
Huwa mnaitaka nini home city mby?.
Hapo enjoy cheap shopping,landscapes na life la town hapo tu
 
Nenda shangazi pub hapo uyole ukatoe lock kisha nenda kwa white ukapige supu ya utumbo.
 
Kwa sehemu za starehe na hata mipango miji hiyo mikoa yote uliyoitaja hapo imeiacha mbeya mbali tu.
 
Mleta mada akili yako haipo sawa.
Kati ya Mbeya na Dar es Salaam ni jiji lipi lina mipangilio ya hovyo ya miundo mbinu?
Dar yote inanuka vinyesi,umeona wapi Mbeya kuna vinyesi na mama ntilie wanauza chakula juu ya vinyesi?
Niambie jiji moja tu kwa hapa Tanzania ambalo lina miundo mbinu bora.
Mbeya ni jiji la watu wenye akili timamu kitu kinachopelekea wivu mkubwa kwa watu wanaotoka kwenye majiji yanayonuka vinyesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…