Mbeya si Green City, ni Dark City; kwa sehemu kubwa mji haujapangika vizuri

Mbeya si Green City, ni Dark City; kwa sehemu kubwa mji haujapangika vizuri

Mleta mada akili yako haipo sawa.
Kati ya Mbeya na Dar es Salaam ni jiji lipi lina mipangilio ya hovyo ya miundo mbinu?
Dar yote inanuka vinyesi,umeona wapi Mbeya kuna vinyesi na mama ntilie wanauza chakula juu ya vinyesi?
Niambie jiji moja tu kwa hapa Tanzania ambalo lina miundo mbinu bora.
Mbeya ni jiji la watu wenye akili timamu kitu kinachopelekea wivu mkubwa kwa watu wanaotoka kwenye majiji yanayonuka vinyesi.
Ilemi, Ilolo, Isanga, Mwanjelwa, Nzovwe, Simike, Itunga, Kalobe kote hamna mashimo ya maji taka wala miundombinu ya kisafisha maji taka.

Jiji ni uchafu mtupu
 
Mkuu unafahamu kwanini pameitwa green city?

Mbona hujazungumzia maana halisi ya Green City.
 
Huu ni ukweli mchungu ambao wana mbeya wengi hatutaki kuukubali.Mbeya inahitaji transformation kubwa sana kuendana na hadhi kama majiji mengine makubwa kama DSM,Mwanza ,Arusha na Dodoma.Tukiendelea kukaza fuvu nakuamini kua mbeya iko vizuri kama majiji mengine tutaendelea kubaki nyuma milele na vimikoa vidogo vitaibuka na kutupita.Tuache kujiongopea na kujipa moyo wakati ukweli tunauona uko dhahiri.Wenzetu wote wana Malls,mbeya hamna hata moja,Wenzetu wana hotels zenye hadhi na swimming za kutosha ,mbeya hotel zenye hadhi na zenye swimming siju kama zipo na kama zipo zenye swimming hazizidi tatu.Wenzetu wana viwanja ving vikali vya starehe lakini mbeya viwanja vya maana sijui kama vinazidi vitatu.Miundombinu wametuacha mbali sana,Majenngo ya kisasa wametuacha mbali sana.Hata ustaarabu (civilization) wametuacha mbali sana,maana mbeya mpaka leo bado tuko zama za mawe za kale tunajenga nyumba za matofali mabichi tena mjini na wakati wenzetu wameshahama huko.
Tofali bichi la Mbeya ukiliingiza kwenye mashine inayopima tensile strength,litasomeka linaumadhubuti wa hali ya juu kuliko matofali yanayouzwa Dar es salaam yaliyotengenezwa kwa mchanga na cement.
 
Niko Mbeya, nimekuja kutembea mara moja, baada ya kuzisikia sifa nyingi sana za mkoa na jiji hili la Mbeya.

Daima huwa na utamaduni wa kufanya matembezi ya miguu ili niweze kuujua mji vizuri, haswa nikiwa mgeni katika mji huo.

Mbeya ni jiji lililojaa vumbi, barabara za lami ni chache sana. Mipango miji ni sifuri.

Mji uliopangika vizuri ni ule mji uliopangwa na wakoloni, maeneo ya Uzunguni, Uhindini, Soko Matola, Ghana na Majengo, zaidi ya hapo ni uchafu mtupu.

Pia soma: Mwanza City (Lake Zone Economic Powerhouse) vs Mbeya City (S/Highlands Economic Powerhouse)

Miji iliyopangiliwa baada ya hapo haina sifa ya kusema kwamba iko planned.

Majengo ya mji ni ya ajabu kabisa. Jengo la CCM mkoa ni baya sana utadhani jengo la kilabu cha pombe za kienyeji.

Barabara za mji zimejaa vumbi, ukiliingia unajikuta nusu ya ugoko wako imezama kwenye vumbi, sijui hata anachokifanya huyu Dada Tulia.

Mbeya hamna mahoteli, hoteli pekee yenye hadhi ni hotel ya Desderia ya Mr. 2 a.k.a Sugu.

Mbeya kila ni kibaya, lakini anatakiwa kulaumiwa nani?

USHAURI:-
MBEYA JIJI wachukue ramani ya Majengo, Soko Matola na kuihariri kidogo, basi wataweza kuitengeneza Mbeya iliyo bira sana
Kwani mji upi umepangika vizuri Tanzania, labda zaidi ya Dodoma chini ya CDA?
 
Tofali bichi la Mbeya ukiliingiza kwenye mashine inayopima tensile strength,litasomeka linaumadhubuti wa hali ya juu kuliko matofali yanayouzwa Dar es salaam yaliyotengenezwa kwa mchanga na cement.
Duuh punguza ujuaji ndugu yangu..hata kama ina umadhubuti..ndio ziote nyasi..mbona mkoa primitive sana wakuu
 
Ujenzi umejengwa kiholela hakuna mipangilio,na hilo tatizo siyo mbeya liko nchi nzima

Ova
Nilikua naangali mpira wa Yanga na Ken gold kabla ya mechi kuanza Azam TV wakachukua picha ya mjini kusema kweli mji upo hovyo yani kwanza Ardhi yake imekaa Viabaya Nyumba zimejengwa hovyo sana
 
Nilikua naangali mpira wa Yanga na Ken gold kabla ya mechi kuanza Azam TV wakachukua picha ya mjini kusema kweli mji upo hovyo yani kwanza Ardhi yake imekaa Viabaya Nyumba zimejengwa hovyo sana
Hata uwanja wenyewe ukiangalia haupo nadhifu kabisa kama viwanja vya wenzetu..mbeya inapaswa ibadirike ,uwanja mchafu na unajiotea manyasi hovyo hovyo halafu hawajali wala nini.
 
Back
Top Bottom