KERO Mbeya: Vyoo vya Uwanja wa Sokoine ni vichafu sana, wahusika hamjali afya za Wateja wenu

KERO Mbeya: Vyoo vya Uwanja wa Sokoine ni vichafu sana, wahusika hamjali afya za Wateja wenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Waungwana hivi ni viwanja vyote ambavyo vina changamoto ya vyoo au ni Sokoine Stadium tu hapa Mbeya.

Maana huu uwanja vyoo vyake ni changamoto kubwa, ni vichafu balaa na hakuna maji kabisa.

Wamiliki wa uwanja embu jitahidini basi kurekebisha vyoo kama mnavyo pambana kurekebisha sehemu ya kuchezea.

Tumeona Meneja wa Uwanja, Modestus Mwaluka akipata Tuzo za kutosha Kwa kuutunza uwanja lakini ukienda chooni ni balaa tupu.

Ombi kwenu Bodi ya Ligi mnavyokagua viwanja waambieni wamiliki wawapitishe na vyooni mjionee.

Soma Pia: Uwanja wa Sokoine Mbeya hauna msimamizi, mbona mchafu sana?

Muwe mnatujali na sisi watazamaji maana ndiyo wateja wenu,Sasa kama sehemu za kujistili zinakuwa chafu mnatufanya tushindwe kuja viwanjani.

Tunakumbushana tu kuwa Afya ndiyo mtaji muhimu kwa mwanadamu.

Mwaluka, safisha vyoo ili kuepukana na Magonjwa kwa watumiaji wa Uwanja wa Sokoine.

DSC_0269.JPG
DSC_0271.JPG
DSC_0267.JPG
 

Attachments

  • DSC_0265.JPG
    DSC_0265.JPG
    541.9 KB · Views: 4
  • DSC_0270.JPG
    DSC_0270.JPG
    457.1 KB · Views: 4
  • DSC_0266.JPG
    DSC_0266.JPG
    554.5 KB · Views: 4
Bodi ya ligi huwa hata mm nashanga
a unatoa tuzo ya meneja Bora wa uwanja ila vyoo,vichafu balaaa
 
Picha moja nimeona mtu kashusha mzigo hajasukuma kaamsha zake!
Hiyo ndo Mbeya niijuayo, ustaarabu 0
 
Back
Top Bottom