KERO Mbeya: Vyoo vya Uwanja wa Sokoine ni vichafu sana, wahusika hamjali afya za Wateja wenu

KERO Mbeya: Vyoo vya Uwanja wa Sokoine ni vichafu sana, wahusika hamjali afya za Wateja wenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Waungwana hivi ni viwanja vyote ambavyo vina changamoto ya vyoo au ni Sokoine Stadium tu hapa Mbeya.

Maana huu uwanja vyoo vyake ni changamoto kubwa, ni vichafu balaa na hakuna maji kabisa.

Wamiliki wa uwanja embu jitahidini basi kurekebisha vyoo kama mnavyo pambana kurekebisha sehemu ya kuchezea.

Tumeona Meneja wa Uwanja, Modestus Mwaluka akipata Tuzo za kutosha Kwa kuutunza uwanja lakini ukienda chooni ni balaa tupu.

Ombi kwenu Bodi ya Ligi mnavyokagua viwanja waambieni wamiliki wawapitishe na vyooni mjionee.

Soma Pia: Uwanja wa Sokoine Mbeya hauna msimamizi, mbona mchafu sana?

Muwe mnatujali na sisi watazamaji maana ndiyo wateja wenu,Sasa kama sehemu za kujistili zinakuwa chafu mnatufanya tushindwe kuja viwanjani.

Tunakumbushana tu kuwa Afya ndiyo mtaji muhimu kwa mwanadamu.

Mwaluka, safisha vyoo ili kuepukana na Magonjwa kwa watumiaji wa Uwanja wa Sokoine.

View attachment 3182678View attachment 3182685View attachment 3182687
Mitano Tena Kwa saa100 na Tulia
 
Back
Top Bottom