Mbeya: Watatu wakamatwa kwa kufanya Biashara ya kusafirisha Watoto wakafanye kazi za Majumbani

Mbeya: Watatu wakamatwa kwa kufanya Biashara ya kusafirisha Watoto wakafanye kazi za Majumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuwasafirisha watoto wenye umri wa miaka 10 na kuwapeleka kutumikishwa kazi majumbani, kilimo na ufugaji katika maeneo mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei amesema leo Septemba 7, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana wakati wakiwa kwenye harakati za kuwasafirisha kuwapeleka kwa wakulima na wafugaji wilayani mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumikishwa kazi, ambapo kwa kila mtoto mmoja walikuwa wakilipwa kiasi cha Sh20,000 mpaka Sh25,000.

"Imebainika kuwa watuhumiwa hao, kwa makubaliano yao kila mtoto mmoja aliyekuwa akiafirishwa wanapatiwa ujira wa Sh20,000 mpaka 25,000 bila kutambua kuwa kufanya biashara ya binadamu na kuwatumikisha watoto ni kinyume cha sheria," amesema.

Amesema kuwa polisi bado wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.

Mkurugenzi wa asasi isiyokuwa na kiserikali ya Sauti ya Mama Afrika (Samofa), Thabitha Bughali ameomba Serikali kuchukua hatua kali kwani kitendo hicho ninawanyima haki watoto kupata elimu na kujikuta wakinyanyaliwa kwa jamii.

Mwananchi

PIA, SOMA: - Mbeya: Kisa cha watoto kutoroshwa, baadhi ya wazazi wakiri kuridhia watoto wakafanye kazi za Majumbani
 
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuiba watoto na kuwauza kwa wafugaji.

Watu hao wanadaiwa kuwaiba watoto hao kutoka kwenye familia zao na wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu kisha kuwauza kwa wafugaji kwa kiasi cha kuanzia shilingi elfu ishirini na tano mpaka elfu thelathini.



________________________________________

Hivi binadamu tumekosa utu kiasi hiki kweli? Unawezaje kuiba mtoto wa mwenzako na kumuuza kama mtumwa kwa kiasi kidogo hivyo cha pesa? Na je hao wafugaji wanawezaje kununua watoto kwaajili ya kuwatumikisha kwa kuwachungia mifugo?

Zama hizi kweli mambo haya bado yapo? Hii habari imenishangaza na kunisikitisha sana. Binadamu ni wanyama sana.
 
Kamata Kwanza wanunuzi,.maana hao ndio wahitaji wa bidhaa
 
Back
Top Bottom