JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata bastola na mkasi mkubwa zilizotelekezwa na watu wawili ambao bado wanaendelea kutafutwa na jeshi hilo.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya, Ulrich O. Matei amesema leo Machi 28., 2022 majira ya saa 06:30 asubuhi maeneo ya Uhindini, Kata na Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya lilikamata silaha aina ya Pistol - Liger M80, CAL.9x9 yenye Maker namba B.94554 rangi nyeusi ikiwa na risasi kumi ndani ya magazine na mkasi mmoja mkubwa.
Amesema silaha hiyo ilikamatwa wakati askari wakirudi nyumbani kutokea kazini ndipo walipofika maeneo ya uhindini jirani na duka la wakala mkuu wa M-PESA aitwaye IRENE KAHEMELE waliwaona watu wawili huku mmoja akiwa amebeba begi dogo jeusi mgongoni na kuwatilia mashaka.
Walipojaribu kuwasogelea walianza kukimbia hali iliyosababisha askari kuanza kuwakimbiza huku akipuliza filimbi kuomba msaada ndipo watu hao walitupa begi hilo na kutokomea.
Katika upekuzi ndani ya begi hilo ndipo ilikutwa silaha moja na risasi 10 ndani ya magazine na mkasi mkubwa mmoja.
Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea.