Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza na waandishi wa habari Mei 15, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa, awali mnamo Aprili 29, 2023 majira ya usiku huko maeneo ya Nzovwe Jijini Mbeya, watuhumiwa walivunja Jengo la Black Microfinance Bank na kuiba silaha hiyo.
Kamanda Kuzaga ameongeza kuwa, kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi kupitia kikosi maalum cha kuzuia na kupambana na uhalifu lilifanya ufuatiliaji na mnamo Mei 11, 2024 huko Kijiji cha Itete kilichopo Kata ya Isuto mkoani Mbeya lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Nerbat Bwiga akiwa na silaha hiyo.
Aidha, Kamanda Kuzaga amesema kuwa mtuhumiwa amekiri kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kushirikiana na mwenzake Isaya Zumba.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kutafuta kazi halali ya kufanya na kuachana na uhalifu kwani hauna nafasi. Pia linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.