Nilipo soma ule uzi wako wa mwanzo ukielezea vitu 6 ambavyo si viumbe vya Mungu binafsi nilikupuuza niliona umekurupuka tu, maana hoja zako zote hazikua na mashiko, lakini naona bado unaendelea kupotosha watu.
Qur'an 21-33 inasema, Nae ndie ambae ameumba usiku na mchana na Jua na Mwezi vyote vinaelea angani. unajua kwa nini Allah kataja usiku na mchana kisha akataja Jua na Mwezi?
Pia ukisoma ktk Surat Mulk aya ya pili, Allah anasema yeye ndie alie umba umauti na uhai, kwa maana hiyo mauti imeumbwa na uhai pia umeumbwa,
ningekua na muda wa kutosha kwa sasa ningekujibu hoja zako zote, ila nakusihi pendelea sana kuuliza kwa jambo usilokua na elim nalo, na sio kukurupuka kuhukumia mambo wakati huna elim nayo.