Mbinu 10 za kumdhibiti mke/GF jeuri.......(FOR REAL MEN ONLY)

Mbinu 10 za kumdhibiti mke/GF jeuri.......(FOR REAL MEN ONLY)

mhh mikono ya mwanamke ndo imekaa kupika na kufua?
kuwa realistc kwa maisha ya sasa wote twaenda porini kusaka maua mazuri ssa iweje tena utake mkeo aawe mjakaz?ITAKUWA AUJAMPENDA BALI UMEOA ILI AWE MTUMWA...

Kwali Rose1980,

Mke wangu mie ni my best friend, siyo beki 3, kibarua wala mjakazi...kama nilimbwata basi mimi nimekuwa overdosed!!

Babu DC!!
 
Tiger hao wageni unajua walikuwa akina nani.............hao ni mkewe sarah? be serious next time bro........... Tiger

Mkuu,
walikuwa malaika, ila kazi ya mwanamke inawezaje kuwa ya mwanaume?
Kwani kutafuta kwa jasho au kuzaa kwa uchungu kunaangalia wageni wako au tamko la mungu?
Huyo mungu anayebadili sheria zake kwa kuangalia matukio mbona simuelewi?
 
Last edited by a moderator:
Cha mhimu hapa kila mmoja na atende kwa makusudi Mungu alivyo muumba, haya mambo ya kutaka usawa mwisho huleta muvutano usio sababu na kuishia majuto.
 
Mengi ya ukweli mkuu hasa kwenye kuendesha gari. Siku moja nilizidiwa night wife akaendesha kwenda hospital, ilibidi nifunge macho nisione kinachoendelea. (labda ni udhaifu wake tu, sijasema wote ni madereva wabaya)
kwenye kupika sawa lakini kwenye kuchoma nyama nikialika marafiki hilo langu, yeye atasaplai vifaa vya kazi tu. Kuna raha ya kuchoma nyama mkononi na glass ya scotch
 
Wana wake wengi wa siku izi ukitumia ivyo vigezo wako belowa 50%
Unakuta mtu kaolewa ata haelewi kwa nini kaolewa kichwani kwake anajua ni FASHION TUU!

na wanaume wanokidhi vigezo ni % ngapi?? Truth be told kwa taarifa tu japo wababa walikuwepo lakini wanawake (mama zetu) ndio waliowezesha wengi wengi wetu hapa tukasoma kwa kuuza mama ntilie na vitumbua na sasa tuna maisha bora na hata tunaweza kubofya hizi Qwerty keybord , na hata sasa bado mwanamke ndiye anayehudumia familia kwa sehemu kubwa. hizo role za wanaume wanawake ndio wanaziplay big time..why? b'se more and more men are becoming irresponsible and some one has to take charge I don't mind mind even if is a woman!!
 
Mengi ya ukweli mkuu hasa kwenye kuendesha gari. Siku moja nilizidiwa night wife akaendesha kwenda hospital, ilibidi nifunge macho nisione kinachoendelea. (labda ni udhaifu wake tu, sijasema wote ni madereva wabaya)
kwenye kupika sawa lakini kwenye kuchoma nyama nikialika marafiki hilo langu, yeye atasaplai vifaa vya kazi tu. Kuna raha ya kuchoma nyama mkononi na glass ya scotch

Just listen to yourself..yani vitu vinavyokupa raha ndo ufanye ww visivyokupa mkeo afanye..na yeye visivyompa raha ?? selfishness huua upendo kabisa!
 
mi nafikiri kwa kukazana kufanya hayo uliyoyaorodhesha hapo ili kuprove u-real men ndio yanayoweza kusogeza kifo karib kwa magonjwa ya moyo,coz mwanaume atajipinda hata kwa kuiba na kukopa ili amuonyeshe mkewe kuwa ye kidume, jaman imeandikwa kuwa mkioana mnakuwa kitu kimoja. bible inasema tunaangamia kwa kukosa maarifa, tafakari chukua hatua, mkeo si adui yako anapaswa kuwa rafiki, ndugu na ndiyo mwandani na msiri wako mkubwa. huo mtazamo wa long sana, utawaumiza tu jaman, kha
 
Katika dini yangu ya kiislam, imenifundisha kuwa mwanamke ni mtu wa kupewa heshima siku zote.

Kazi ya mke kwa mujibu wa dini yetu ya kiislam ni kumpatia mwanaume haki yake, kulea watoto, kuitunza mali ya mumewe na kumpenda mumewe TU! hayo mambo ya kupika, kufua sio kazi ya mwanamke, mambo hayo mwanamke hufanya kwa mapenzi yake kwa mumewe, halazimishwi wala hapigwi wala hagombwi kwa kutofanya ivo vitu. Ofcourse mke anaekupenda atakuhudumia vitu vyote hivo lakini halazimishwi. Tena mwanamke akakikosea hutakiwi kumpiga na kumuumiza, bali unatakiwa uchukue kitambaa chepesi umpige nacho! Hii ndoa itadumu. Lakini ndoa ya kutumia mabavu, haina furaha ng'o
 
1.Kupika ni Jukumu la Mwanaume
2. Kupika je

Mwanaume kamili hafanyi hayo Mambo hapo.. Hako ni kavulana

We uliumbwa nikuletee Pesa za chakula ukanitafutie Vyakula vinono nile nikupende zaidi. Ukileta Mambo ya Ubeijing. Wanawake wa KITANGA na Zanzibar Wanakuwa Nyumba Ndogo..

Hongera......
 
Hizi mbinu ni muarobaini wa wake/ma-GF korofi na utawashikisha adabu...............nimeifupisha kutoka kwenye hii makala ya
Don’ts for husbands

Haya ni masharti ya kukwepa mwanandni wako kufikiri naye ni kidume ndani ya mahusiano yenu..........ukishindwa haya au kama ukijipima ukaona hupati maksi 80 au maswali nane kati ya kumi basi wewe unatawaliwa na mwanamke na mahusiano yenu yapo hatarini kuvunjika au wewe kuwa huna furaha maisha yako yote na utakufa kwa shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo...................

amka jikomboe kutoka kwenye utumwa wa mwanamke..............

Aisee.....

Leo nimecheka kweli!!! Umecombine issues balaa
 
Sijaona cha maana hapo. Hayo sio maisha ya ndoa/mahusiano yenye mapenzi ndani yake. Mtu unajikomoa wewe ili kumkomesha mwanamke unaejidai unampenda ili iweje?! Ukishaingiza kukomeshana na kukomoana kwenye mahusiano yako jua hamna kitu hapo, yani you might aswell just call it a quit.

WORTHLESS!!!
English, ENGLISH, ENGLISH
 
Haya yaliwezekana kwa bibi na babu zetu..kipindi hicho mwanamke hakua na elimu wala kazi, kila kitu alimtegemea mumewe kazi zake ilikua kulea watoto,mume na kazi za nyumbani...
Kwa dunia ya sasa huo ni unyanyasaji aisee mfn.nina elimu yangu,kazi nzuri na mshahara mzuri tu sawa na mume au labda kanizidi kidogo atapata wapi nafasi ya kunitawala?
Mimi siamini kwenye mapenzi ya kukomoana eti hata siku moja humsaidii mkeo hata akichelewa kutoka kazini wewe ukawahi hakuna utakalo lifanya?
Mapenzi ni kupendana,kuheshimiana na kusaidiana hicho unachojaribu kusema ni mfumo dume uliopitiliza,hata kama gari amenunua mwenyewe asiendeshe??no thank you..
 
Namba moja na mbili sisi tunaoshinda vijiweni tutafanyaje?
Kutoka saa 12 asubuhi ,kuingia 12:30 jioni ..

Ruta wewe mkoloni sana
 
na wanaume wanokidhi vigezo ni % ngapi?? Truth be told kwa taarifa tu japo wababa walikuwepo lakini wanawake (mama zetu) ndio waliowezesha wengi wengi wetu hapa tukasoma kwa kuuza mama ntilie na vitumbua na sasa tuna maisha bora na hata tunaweza kubofya hizi Qwerty keybord , na hata sasa bado mwanamke ndiye anayehudumia familia kwa sehemu kubwa. hizo role za wanaume wanawake ndio wanaziplay big time..why? b'se more and more men are becoming irresponsible and some one has to take charge I don't mind mind even if is a woman!!

Umenikunaaaaaaaa.......tukutane jioni wangu.

Just listen to yourself..yani vitu vinavyokupa raha ndo ufanye ww visivyokupa mkeo afanye..na yeye visivyompa raha ?? selfishness huua upendo kabisa!

Hapo sasa......wabongo hawabebekiii
 
Back
Top Bottom