Mbinu hii inaweza kutibu kigugumizi au stammering

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kigugumizi ni tatizo la kushindwa kuongea vizur yaan mtu anakuwa anashindwa kujieleza au kutoa matamshi mpaka ajivute sana,ni changamoto ambayo inawakuta baadhi ya ndugu zetu

Sasa unaweza kuishinda hali hii kwa kufanya mazoezi ya kuongea zaidi,jitahidi kuongea kadri iwezekanavyo na baada ya mda kuna mabadiliko makubwa sana utayaona,tafuta mtu ambaye unaweza kupiga nae mastori ya hapa na pale,na mwisho wa siku utakuwa vizuri

Ntakupitisha kwa mwandishi wa kitabu cha "Thoughts to build on" naye alikuwa ana changamoto ya kigugumizi,lakini kuna njia kadhaa alizitumia ambazo zilimsaidia mpaka baadae akaja kuwa muongeaji mzuri tena wa kimataifa

Anasema kwanza alianza kujiongelesha mwenyewe katika nafsi yake bila kutoa sauati,halafu baadae akaanza kuzungumza kwa sauti ya ndogo na baadae kwa sauti kubwa ya wastani ambayo tunaitumia katika mazungumzo yetu ya kawaida

Aliendelea zaidi kwa kuzungumza na mtu mmoja mmoja baadae kikundi cha watu,baadae na staff members wa bodi ya kampuni yake,baadae na maseneta wa marekani na mwisho wa siku aliongea na ulimwengu kwa kupitia idhaa ya redio ya VOA (voice of Amerika)

Kwakuwa ukitaka kutibu tatizo hili unatakiwa kuongea zaidi na kwa bahati mbaya sana hakuna mtu ambaye anampenda sana mtu muongeaji sana,basi njia pekee ya kufanya ni kujiongelesha mwenyewe,nenda kwenye kioo chako,jiongeleshe kwa namna unayojua wewe kana kwamba unaongea na mtu mwingine

Tembea nyumbani kwako labda kuanzia jikoni mpaka sebuleni,zungumzia kuhusu vyombo vyako,zungumzia kuhusu makochi,kabati,television set na chochote kile,lengo hapa ni kuzungumza,ongea kuhusu hivyo vitu,ikiwezekana kama unakumbukumbu ulinunua wapi basi jikumbushe kumbuka hapa unafanya mazoezi ya kuongea,just talk and talk and talk

Huenda unatembea kwenda sehemu fulani,zungumzia kuhusu uoto wa asili,zungumza kuhusu mazingira yoyote unayayaona kumbuka hapa lengo ni kufanya mazoezi ya kuongea,we ongea na ongea na ongea

Kadri jinsi unavyofanya jitihada za kuzungumza ndivyo unavyozidi kupona tatizo lako,kwahiyo njia pekee ni kujitahidi kadri ya uwezo wako kadri iwezekanavyo na mwisho wa siku utakuwa vizuri

Kwahiyo wapo ambao walikuwa na kigugumizi kama wewe lakini kwa kufuata hataua kadhaa ambazo nimezidodosa hapo walikuja kufanikiwa na kuwa vizur tu,hata wewe unaweza pia

Ni hayo tu!
 
Ahsante sana, hii itawasaidia wenye hiyo changamoto! Wajaribu kufanyia kazi!
 
Back
Top Bottom