Mbinu mbalimbali wanazotumia matapeli kutapeli watu

The Lost Boy

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2020
Posts
248
Reaction score
311
Mwaka 2012 saa tatu usiku hivi, nikitembea pale Zakhem nikitafuta daladala za Chamazi. Na ule uharaka wa kutembea ghafla nikajikuta kama nimemkanyaga bwana mmoja (alijikanyagisha sikujua).

Basi akanishika begani huku akitweta kwa ghadhabu kuu "kwanini unanikanyaga bro, wajikuta nani labda... " muda huo ajifanya kama kulipiza kisa kwa kunikanyaga mguuni mwangu.
Nikaona mambo yasiwe mengi nikawa namuomba radhi yaishe kiuungwana.

Lol, sikujua ni matapeli, muda ule natafuta suluhu, kwa nyuma alikwepo mwingine ambaye ndiye alochomoa kiswasadu changu hali sina habari
Alokabwa ndio kaiba
Ulitapeliwaje mjini?
 
Nilitapeliwa ukweni😢
 
Skuizi ukipokea pesa tu kuanzia elfu 50 tu wanakuja kama wote we utaskia mmoja anakuja anasema yeye mganga kutoka kigamboni anatibu nyota na mapenzi tuma kwa namba hii nikutibu Cc ephen_
 
Umechelewa sana kugundua me siku ya kwanza walinifanyia hivyo... Ile mmoja kanichomoa tu nyuma nikamdaka. Nikaandaa ngumi mkononi. Nikamwambia naomba ulichochukua kabla sijakuwasha. Alirudisha fasta.
 
Nilishapigwa elfu 10 yangu pale Kariakoo kwa mbinu hii hii 2010.

Nilikuwa natoka NMB kariakoo nikiwa na mafumba kibao kwenye Bag, nikachukua pesa kama elfu 50 nikaweza mfuko wa sharti kwa kutumia muda ule.

Aisee sijui walinionaje, akajifanya kama tumegongana kwenye msongamano....huku najikwamua kumbe mwingine anavuta mkwanja. Ikatoka buku teni tu
 
Ulitapeliwa kiboya sana. Nilikuona hiyo jana, na jinsi ulivyokuwa umevaa siulizi, utakuwa umetokea Njombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…