Mbinu mpya wanayotumia matapeli wanaotuma meseji

Mbinu mpya wanayotumia matapeli wanaotuma meseji

Hii nayo ikoje mkuu... yaani mfano ungefanya vile atakavyo ungeibiwaje?
ni cheusi chekundu alitaka kucheza,
nilikuwa na pesa kwenye simu laki420 alivyotuma hiyo elf50 ikawa 470..!

wakati ananipigia kunipush nimtumie katika ile namba ya dogo wake alieko shule huku nyuma alikuwa anataka awahi kunipiga pini,nikishatuma kwenye ile namba ya dogo palepale anapiga huduma ya wateja kisha wana reverse kwake ile hamsini!!
kumbuka hapo nilishatuma 50 yake kwa dogo ambaye ni yee
 
Aina za utapeli zipo nyingi ila mimi napokeaga sms tu mara nyingi, ya kupigiwa simu imetokea mara moja tu eti mtu kapiga simu anasema yeye ni makao makuu ya tigo huku namba aliyotumia ni voda sasa nilichojichanganya na mimi ni kumuuliza kwamba je hapo makao makuu mnatumia voda siku hizi- huu ushirikiano wa tigo na voda umeanza lini?" Matusi niliporomoshewa hapo ni mvua halafu nikasikiliza mpaka alipochoka kutukana akakata simu mwenyewe

Ilikuwa tigo ila sasa naona ni ttcl...
Kila meseji inayoingia ni wao kama sio basi voda

Zantel ni wa kwanza (nadhani) kuanzisha utaratibu wa kuripoti utapeli ila cha ajabu hiyo Zantel nimetumiwa mara moja tu ujumbe tangu nisajili

Airtel ndo namba yangu inayoongoza kwa kutumiwa hizo mambo halafu cha ajabu huku nilipo mtandao haushiki ila hata kama ni wiki sijawa hewani siku nikiwa hewani tu sms yao kuna uwezekano mkubwa kuingia
 
mimi alinitumia ela 50000 halafu hapohapo akanipigia kwamba amekosea hivyo ananitumia namba ya dogo aliye skuli nimrushie...
nikampotezea maana janja ya nyani kwishajua!!
hadi mwisho ikaomba msamaha kwamba nirudishe haitarudia tena...
hapo mimi iko kwa mama muuza piga moja moto moja baridiiiii..
iko fikiri kila mtu ni MAKU MAKU

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Habarini za asubuhi,

Wale jamaa zetu wa "tuma kwenye namba hii" kisha wakaja na kauli mbiu yao ya "Mimi mwalimu mtoto wako ameanguka ghafla tunaomba utume pesa kidogo ya kusaidia matibabu ya haraka huku ukijiandaa kuja" wamekuja na kauli nyingine isemayo: "
Habari yako? Mimi mwenye nyumba wako naomba hiyo kodi ya nyumba irushie kwenye hii ttcl 0734 693 419 maana na shida nayo, halafu mbona umekaa kimnya bila taarifa?

Namba ya mtumaji 0734 457 719

Chukueni tahadhari wale mliopanga
Apo kama ulimblock mwenye nyumba utazani ni yeye tena unamchapa block nyingne
 
Hili suala ni kweli, wazazi wangu walitaka kutapeliwa kwa mtindo huo, nina mdogo wangu kamaliza 4m 6 mwaka huu, sasa wakati yuko shule ilikua mwezi wa pili,

Siku hiyo majira ya mchana baba akiwa kazini kwake, akapokea sms kwa cm yake ikisomeka hivi, "habari mzazi, mwanao ameanguka darasani ghafla na kupoteza fahamu, tumefanya jitihada za haraka kumfikisha hospital ambapo anapatiwa matibabu, ila bado hajapata fahamu hivyo unatakiwa utume gharama za matibabu kwa no hii (huku ikiambatanishwa namba husika)".

Baada ya kusoma ile sms, akahamaki akampigia cm mama kumfahamisha, hapo mama akaanza kuchanganyikiwa na kumshinikiza baba atume hela haraka iwezekanavyo, sasa baba akatak kujua undani wa tukio hilo, akapiga cm kwa no ilotuma text haipokelew zaid ya mara 3, baadae ile no ilatuma sms "samahani nipo sehemu mbaya siwezi kupokea cm, ila mwanao kazinduka na daktari kasema gharama itakua laki 2".

Hapo baba akaona haelewi chochote, akamtafuta kaka mkubwa kumpa taarifa, sasa mkubwa ana mawasiliano na baadhi ya walimu ktk shule anayosoma dogo, akawacheki kuuliza anambiwa dogo yupo vizur wala hakna tatzo lolote, akapewa dogo cm wakaongea na kaka yaan dogo yupo vizuri kabisa. Ndo hapo ikawa amani kwa wazazi, vinginevyo wangetuma hela kwa matapeli.

Utapeli wa mtandaoni upo na unazidi kukua kwa kasi.
Awa wahuni wanapiga mno pesa
 
Me niliwajibu hivi
Screenshot_20210614-143115_Gallery.jpeg
 
ni cheusi chekundu alitaka kucheza,
nilikuwa na pesa kwenye simu laki420 alivyotuma hiyo elf50 ikawa 470..!

wakati ananipigia kunipush nimtumie katika ile namba ya dogo wake alieko shule huku nyuma alikuwa anataka awahi kunipiga pini,nikishatuma kwenye ile namba ya dogo palepale anapiga huduma ya wateja kisha wana reverse kwake ile hamsini!!
kumbuka hapo nilishatuma 50 yake kwa dogo ambaye ni yee
Sio uongo ningepigwa
 
ni cheusi chekundu alitaka kucheza,
nilikuwa na pesa kwenye simu laki420 alivyotuma hiyo elf50 ikawa 470..!

wakati ananipigia kunipush nimtumie katika ile namba ya dogo wake alieko shule huku nyuma alikuwa anataka awahi kunipiga pini,nikishatuma kwenye ile namba ya dogo palepale anapiga huduma ya wateja kisha wana reverse kwake ile hamsini!!
kumbuka hapo nilishatuma 50 yake kwa dogo ambaye ni yee
Duu mkuu noma.sana, 😁😁
 
Mimi ninachojiuliza wanapataje hizi namba zetu maana dah! Aisee sielewi wanajuaje kuwa namba hii inatumika.

Au wanajuaje kwamba huyu mtu anapesa kwenye simu aana aisee.
Mbona ni rahisi hata wewe unaweza kubuni namba ukatuma meseji, kama ziko hewani zitafika kwa walengwa
 
Watu wanaotapeliwa kwa njia hizo za kiduanzi huwa hawachukui muda kutafakari na ndivyo ilivyo hulka ya wabongo wengi...

Maisha yetu yamekaa na 'short cuts' sana...
 
Napokea meseji kama hii wakati naishi kwangu sijapanga, ila si ajabu kuna watu unakuta wanatuma hata kama wanakaa kwenye nyumba zao walizojenga wenyewe [emoji23] [emoji28] watanzania hawana masihara
Meseji inatumwa kwa yeyote atakayepatikana huyohuyo
 
Sasa hivi wamekuja na mbinu nyingine na hii nimeziona juzi. Jamaa yangu kapoteza simu juzi. Namjua muda mrefu tu kuwa anatumia simu ndogo. Sasa nimeshangaa napokea msg whatsapp kutoka kwenye namba yake nimuazime pesa kidogo. Nimesikitika Sana maana najua kuwa hata jamaa akienda kufunga line yake bado jamaa ataendelea kutapeli WhatsApp tu mpaka apate simu kubwa ya kutumia kufunga account yake
View attachment 1818372
Nyinyi ni wazembe, ina maana wewe mwenye smartphone umeshidwa kabisa kumsaidia jamaa kufuta hiyo acc
 
Back
Top Bottom