Mbinu wanazotumia Matajiri wakubwa wa Kariakoo kuendelea kuwa matajiri na kutoshikika

Mbinu wanazotumia Matajiri wakubwa wa Kariakoo kuendelea kuwa matajiri na kutoshikika

Wewe na huu uzi wako ni sawa na hii picha hapa chini, simply you are an average Joe who trying to be a motivational speaker 😂😂.
Hii post motivational Ni ipi? Why mnapenda Kila mtu aongelee udaku au siasa na mpira? Post ni tofauti kabisa na video uliyokariri. Post inaelezea siri wanazotumia na sio namna ya kuwa tajiri. Mimi ni winga tu pale ambapo hata wewe ukikaa kariakoo au kuwa mnunuaji utazijua na kushare Sio mbaya
 
Ok sawa! Nini kifanyike kwa wenyewe mitaji midogo na wasio kwenye cycle?
 
Wana Wachina/“Washirika” wa Biashara

Wengi wana connection za moja kwa moja na wazalishaji au mawakala China. Wanaweza hata kupewa mzigo kwa mkopo, au kupewa taarifa mapema za bidhaa mpya kabla hazijaingia sokoni.
Hapa wamewin sana.
 
Nikisoma hivi naskia kuchanganyikiwa na kukata tamaa kabisa😔
 
Namba 1 inaweza ndio silaha yao kuu. Pia je hawana connection na watu wa TRA au huko bandarini?
 
DAH mkuu, mchawi Kodi ukicheza vizuri unatoboa haraka sana

Kwishaaaaaa
 
Wewe na huu uzi wako ni sawa na hii picha hapa chini, simply you are an average Joe who trying to be a motivational speaker [emoji23][emoji23].
huyu usikute alikua anauliza sio kufundisha
 
Ukiwa kijijini n biashara gan poa zinaweza kutengeneza circle ya matajiri kama hao,
 
SIRI WANAZOTUMIA MATAJIRI WAKUBWA WA KARIAKOO KUENDELEA KUWA MATAJIRI NA KUTOSHIKIKA

Usipozijua utaendelea kuwashangaa

Ukitaka kujua Tanzania kuna matajiri, Nenda kariakoo. Hizi ni baadhi ya siri tu wanatumia kuendelea kukuza utajiri wao...

1. Group Buying ya Nguvu
wanaungana makundi na kuagiza mzigo mkubwa moja kwa moja kutoka China.

Kwa kuwa wananunua kwa wingi sana (wholesale ya wholesale), wanapata bei ndogo zaidi hata kuliko mtu unayeenda mwenyewe China. Hii huwapa faida kubwa ya bei wanaporudi Kuuza. Wanaungana WATU 10 kila mtu ana 100M _200M wananunua Duvert za 2B wewe unaenda China na 50M mtafanana sokoni?

2. Wanachukua Mikopo Mikubwa kwa Malengo Mahususi

Tofauti na watu wanaokopa kwa dharura au matumizi ya kifamilia, wao hukopa na kununua mzigo mkubwa unaozunguka haraka na kuleta faida kubwa. Wanajua pesa ya benki ni zana, sio mzigo.


3. Wana Channels Imara za Wanunuzi

Wana mtandao wa wanunuzi wakubwa – wauzaji wa jumla kariakoo, mikoani, masoko makubwa, na wafanyabiashara wadogo wanaokuja kuchukua mzigo kila siku. Hata kama hawapo Instagram au TikTok, bidhaa zao huisha kwa kontena, si kwa picha za kupost.


4. Wanabeba Mizigo ya Haraka Tu (Fast Moving Products)

Hawapotezi muda na bidhaa zinazokaa miezi stoo. Wanafuatilia bidhaa zinazotoka kila siku, zinazotumiwa na watu wengi, na haziitaji "kufundisha" soko. huuza sabuni, vyombo, nguo, plastiki, vyombo vya nyumbani n.k.

5. Wanafahamu Timing ya Soko

Wanajua lini mzigo gani unahitajika – mfano, sare za shule Desemba wakati we unaleta week ya wanafunzi kufungua, nguo za sikukuu Machi na November, viatu vya mvua kipindi cha masika n.k. Hawabahatishi. Wanaingia sokoni kabla bidhaa haijaanza kuhitajika. Wanawahi mahitaji


6. Wana Wachina/“Washirika” wa Biashara

Wengi wana connection za moja kwa moja na wazalishaji au mawakala China. Wanaweza hata kupewa mzigo kwa mkopo, au kupewa taarifa mapema za bidhaa mpya kabla hazijaingia sokoni.


7. Si watu wa Maonyesho.
Unaweza kudhani ni stoo keeper na Winga ndo mwenye duka, mitandaoni wanapost nne au tano za familia tu


8. Wana Mfumo Mkali wa “Cash Rotation”

Wanahakikisha pesa haikai – wanapokea mzigo, wanauza haraka, na kurudisha tena pesa hiyo kwenye mzigo mpya. Hili huwapa mzunguko mkubwa wa bidhaa na faida kila siku, badala ya kusubiri faida ya mwezi /mwaka.


9. Wana Vibarua wa Kueleweka na Mfumo wa "Loyalty"

Wana timu ya watu wa kusambaza, kupakia, kufunga, hata kuuza kwa niaba yao. Hawa watu wanaaminika, wanahudumiwa vizuri, na mara nyingi wamejengewa utaratibu wa malipo unaowafanya wasihame hovyo hovyo.


10. Wanajifunza na Kufuatilia Trends za Kimataifa

Hata kama hawako kwenye mitandao, wana watu au familia wanaowasaidia kufuatilia bidhaa zinazo-trend duniani. Wakiona kuna bidhaa mpya ya moto Ulaya au China, wanaagiza kabla soko la Tanzania halijajua.
.
Ingawa unaweza kuwa huna mtaji kama wao ila kuna siri unaweza kuzitumia kupanga juu.
.
Katika siri hizi. Ni siri gani utaanza kuitumia
Wewe kwenye hizi umetumia ipi?
 
Back
Top Bottom