Mbinu ya kujiwekea uwezekano mkubwa wa kupata unachokitaka

Mbinu ya kujiwekea uwezekano mkubwa wa kupata unachokitaka

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,177
Reaction score
734
Chochote unachokitaka kwenye hii dunia unaweza kukipata kutoka kwa watu. Kiwe kikubwa, kiwe kidogo; iwe watu wengi, au watu wachache. Cha muhimu ni kujenga mazingira yatakayofanya wakupe “wewe” na/au waendelee kukupa tena na tena.

Kwa miaka yote niliyofanya kazi katika taasisi kubwa za serikali na binafsi nimekuwa aidha muhusika mkuu wa manunuzi au mtu ambaye nina mchango katika maamuzi ya zoezi la manunuzi. Wauzaji wa bidhaa za taasisi zetu walikuwa ni wengi sana, zaidi ya 100; ila mar azote tulikuwa tunaishia kununua kutoka kwa wauzaji 5 mpaka 10 tu. Wauzaji hawa wengi walikuwa wahindi, na walijua kutupa sababu muhimu zaidi za sisi kuwapa wao biashara. Wao walipata biashara, na sisi tulipata mahitaji yetu plus (Mahitaji +).

Faida.jpg


Unaweza kupata au kukosa unachotaka (kazi, mtaji, biashara, pesa nk) kwa kutumia vitu saba:
1. Potential yako (Una lipi kubwa? Unaweza kufanikisha nini?)
2. Network yako (Watu unaojuana nao; Watu wanaoweza kukusaidia)
3. Upekee wako
4. Kujulikana kwako
5. Kupendwa kwako
6. Kuaminika kwako
7. Kuwasilisha kwako

Kabla ya kuanza kuhangaika na dunia na walimwengu basi anza kuhangaika na hivyo vitu kwanza. Pia usitumie nguvu nyingi kuhangaika peke yako kutokea nje, bali tumia watu waliomo ndani wakusaidie kukuhangaikia pia. Tazama mazingira ya watu wanavyopata mikopo benki – wameenda benki, wana dhamana zilizokubalika na benki, wamewashawishi vizuri maafisa wa mikopo.

Kwa sasa tuna tatizo la uwingi wa watu wanaotafuta ajira na uchache wa nafasi za ajira. Ila bado watu ambao wana ujuzi/uzoefu/maarifa yanayohitajika sana kuzuia upotevu au kuongeza uzalishaji katika taasisi/makampuni/ofisi zingine wanapata kazi. Watu hawa wana potential; ni assets.

Unaweza kuanza biashara bila mtaji kwa kuwa na uwezo wa kuwapatika watu mahitaji yao muhimu na kuwataka walipie kwanza ndipo uwatengenezee au uwaagizie kisha uwapatie. Mwaka 2018 nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye alinunua kiwanda kwa mkopo. Ni bahati mbaya sana aliunderestimate operations za kiwanda na mara tu akajikuta hana kabisa pesa za kununulia malighafi kutengenezea bidhaa, ila ikaja bahati nzuri sana maana viwanda vya bidhaa yake ni vichache nay eye bidhaa zake zilikuwa zinaaminika na bei yake ilikuwa ndogo. Wasambazaji wa bidhaa zile na maduka makubwa ya jumla wakamfuata rafiki yangu kama mmiliki mpya na kumuomba awatengenezee bidhaa zile huku wao wakilipia kabla. So anakusanya Tsh 30,000,000 ananunua malighafi na kulipia gharama zingine kwa Tsh 21,000,000 kisha kuwatengenezea na kuwapelekea wale wateja bidhaa zao ndani ya siku 3 tu! Alikuwa na Potential (uwezo wa kuwatimizia wasambazaji wake mahitaji ya bidhaa), Upekee (bei zake zilikuwa ndogo kiasi), Kuamikika (Kiwanda kilikuwa kizima, vibali vipo hai na document zote zilikuwa safi) na Kujulikana (Kumbuka kwamba wateja walikuwa wanamfuata yeye alipo).

Kwa sasa ni ngumu sana kupata kazi kwa kusambaza CV, application letter na copy za vyeti maofisi mbalimbali na kusubiria kuitwa kazini. Ofisi tayari ina applications zaidi ya 50 kama zako. Utatumia muda mrefu, nguvu nyingi na gharama kubwa. Bora uhangaike kunetwork na waajiriwa wa ofisi unazowazia kuajiriwa, maafisa waajiri (HRs), wamiliki, mabosi na kadhalika. Ufanye mawasiliano nao ya hapa na pale, uwakumbushe kukiwa na nafasi popote wakushtue, wakumbushe mabosi kwamba unaweza “kuwafanyia maajabu” katika kampuni yao na kadhalika. Julikana na watu, Pendeka, Aminika. Ukiitwa mahali kikazi fanya presentation (wasilisha maboresho, fursa, ziba mapengo na madhaifu) ya kufa na kupona!

Ukiweza kufanya kitu kinachoonekana na kuthibitisha bila shaka nini unaweza kuzalisha zaidi basi unaweza kufanikiwa kupata kazi, mtaji, biashara au pesa unazohitaji. Matapeli wengi wanaendelea kutapeli watu kwa sababu wamemaster vizuri zoezi zima la uwasilishaji (presentation)! Tapeli anakuonesha mkoba halisi wa Gucci unaridhika nao. Unajua bei yake halisi ni Tsh 300,000; ila tapeli amekutajia atakuuzia kwa Tsh 40,000 tu maana ameuiba kwa muhindi so anauuza fasta apate hela ya kula. So na wewe unajaa unabargain tena akupunguzie bei unampa Tsh 30,000. Tapeli anakubali kwa shingo upande anakuambia haya toa hela huku yeye anatafuta mfuko wa kukuwekea mkoba wako wa Gucci. Unalipia Tsh 30,000 unaondoka na mfuko wako, kufika nyumbani hakuna mkoba na tapeli alikuuzia njiani tu so hata ukirudi haumkuti.

Tuishie hapa jamani. Jua tu kwamba kila kitu ni biashara, wewe unatoa na mwenzako anatoa. Wewe unapokea na mwenzako anapokea. Hakikisha una kikubwa cha kutoa na unakutana na watu sahihi wenye uwezo wa kukupa unachotaka.

Mwaka 2010 nilihitaji mkopo kutoka benki kwa ajili ya kuanzishia biashara. Sikutosheleza vigezo vilivyoainishwa na benki, ila yule afisa mikopo aliniambia anaweza kuipitisha kunisaidia nipate mkopo “at his own risk” ila mkopo ukitoka tu nimpoze Tsh 200,000. Tulikubaliana kufanya hivyo na baada ya siku 3 mkopo ukaingia kwenye akaunti yangu na mimi nikampa Tsh 200,000 yake.

Dunia ndivyo ilivyo. Si wewe, si mimi.
 
Hii mbinu inahitaji mtu ambae ana akili za asili, sio akili za darasani
Na Mwenye akili hizo hawekezi nguvu nyingi kwenye kuajiriwa (utumwani)
 
Mkuu umechambua vizuri sana, hiyo no mbili naitumia vizuri sana, kufaamiana na watu na kuwa mwaminifu hivo vitu viwili vinaweza kukupa unachotaka, friendship is more than talent.
 
Nilikwenda kukopa World Bank nikiwa na umri wa miaka25 tu!!.jopo la maafisa mikopo ile waliponiona tu! Kwenye inter view!! walicheka sana!! Wajatamka mbele yangu dogo kachanganyikiwa huyu.....wakaniuliza natoka nchi gani?? Km kawaida Bongo!!! Ndo kabisaaa hawana mbavu!!!...mbaya zaidi wazo hata la biashara sina!!!

Ila akatokea mmoja tu mwenye ushawishi pale......akanidhamini na kunipa wazo kuwa kuna taasisi pamoja na wao wanahitaji mask!!ivo niwatengenezee!! Wao Wakanipa akili ya kutafuta mashine ya kutengenezea...kweli nikaipata dakika sifuri.... Basiii .nikakomaa mwenyewe na mpenzi wangu.Maria..

Tukazalisha faster tena tukakidhi mahitaji kuzidi walivotarajia...ee banawee!! Zikamiminika kazi hizo na miradi mingine miiingi....ndo nikawa tajiri mpaka leo. Ni chuma cha pua...
 
Back
Top Bottom