Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Utashi ni kipawa cha binadamu kinachomfanya aweze kutaka mwenyewe chochote. Kitu hicho kinaweza kuwa chema na hata kibaya, ingawaakili yake mwenyewe inaona zaidi wema fulani uliomo na ambao unamvuta. [Wikipedia]
Je unafahamu vitu kama afya njema, umbo la mwili wako na hata sura yako kwa kiasi fulani[tena kikubwa] inachangiwa na utashi wako binafsi? Ndiyo zipo sababu nyingine pia lakini hii hapa nayo ina nafasi yake.
Tuzungumzie suala moja tu la umbo la mwili wako, ikijumuisha ukimbaumbau na ukibonge na mengineyo.
Kwa tafsiri ya harakaharaka tuseme kuwa mwili wa mtu mwenye umbo kubwa una muelekeo wa kutunza nishati na rasilimali muhimu kwa wingi zaidi mwilini. Na huu muitikio wa kutunza nishati kwa ajili ya mapambano ni wa kibaiolojia, sema ni wa kizamani kwa sababu wakati huo hatari yoyote ilimaanisha kupigana au kukimbia. Yote yalikuwa ni matukio yanayohitaji nguvu. Hata sasa mwili huitikia vivyo hivyo hata kama tatizo ni la kufikirika tu kichwani. Mfano hauhitaji nguvu yoyote kupambana na baruapepe ya ‘deadline’ ya kazi kutoka kwa bosi. Lakini ikitumwa utashangaa moyo unaenda mbio, kijasho chembamba bila ‘action’ yoyote inayohitaji nguvu.
Mwili bado unaitikia ki-primitive hata kwa changamoto zetu za kisasa! Waliofanikiwa kuiondoa hofu kwa kiasi kikubwa katika miitikio yao, hawasumbuliwi sana na matukio ya kisasa yawe ya kimaisha, au kiafya. Ni jambo kila mmoja anaweza kujifunza na kuipata faida yake. Kubali tu kutumia akili vizuri zaidi. Outsmart your body!
Kwenye suala la mwili mtu anaweza kusema ooh! Mbona mimi similiki kampuni wala sina mawazo eti soko litayumba pesa zangu zitapotea. Kwanza naomba nikutoe wasiwasi ndugu. Hii bado ni nadharia tu. Lakini jikague zaidi; je unazitambua hatari ngapi duniani? Mfano ukipanda gari unakuwa makini na ajali? Au unapumzika kabisa na kutazama miti hapo nje dirishani? na kufurahia mwendokasi kwamba tunawahi kufika nikamkumbatie mama/baba/mpenzi wangu? Kwenye mahusiano je? Unajiachia kwa amani? Au ndio unatawala misemo kama ‘kikulacho ki nguoni mwako’, atanisaliti, haeleweki? Je unazifahamu kesi ngapi za kusalitiana, ngapi za kuishi kwa upendo hadi uzeeni. Je unahisi mahusiano ya aina ipi ndiyo mengi?
Unahisi huo wako utakuwa kundi gani? Kuhusu amani; unafahamu maisha kuijumla ni amani? au ni vita? Kuhusu uchumi; je unaionajeonaje hali ya uchumi? Je tunahitaji kujizatiti kiasi gani kiuchumi? Hali ya kisiasa, hali ya kiserikali; je unahisi ipojepoje; je ni ya kusapoti? Je ni ya kupigwa vita? Je katika mambo imayofanya asilimia ngapi unahisi ni ya maana? Asilimia ngapi unahisi hayafai? Katika dini uliyonayo je ipojepoje; je ni upendo na huruma? Je, ni ukali na hukumu? Je unahitajika kuipambania? Kwa njia zipi za amani au za namna gani? Naomba nisisitize hapa kwenye dini simaanishi historia zake, bali namaanisha ‘hivi sasa’ kulingana na unayoyajua hadi hivi sasa unahisi kipi ni kweli. Wewe binafsi bila kujali kundi ulilopo. Hata kama tuna makundi na akili ya makundi ipo, lakini kumbuka! nafasi ya akili yako binafsi ni kubwa sana. Ukiamua wewe ndiyo unaweza kujiruhusu kutumia akili ya kundi ulilopo lakini siyo yote.
Basi ndugu zangu yote hayo yanaijenga ‘will’ yako, yanaujenga utashi huru wako binafsi. Na kitu kikubwa kinachohusika hapo ni taarifa unazozijua na hasa unazozikubali kwamba ndio ukweli hadi muda huu hapa unapoamua. Na ndivyo utashi/will yako inavyoamua na kuamurisha mambo yaani ndiyo wewe ulivyo. Mtajitambua kwa matendo.
So kadri unavyokuwa umejengwa na taarifa njema zaidi mwili wako hautajiandaa na mapambano. Na kadri unavyozidi kuwa na ufahamu na habari za kutisha na mbaya ndivyo ambavyo mwili utajiandaa zaidi kwa mapambano.
Pendekezo kwa watakaopenda kujiunda kuwa bora zaidi kadri siku zinavyoendelea. Kujitengenezea utashi mzuri [good will] unaweza kutumia mbinu nyingi ikiwamo hizi. Hii itajumuisha binafsi, kijamii, kitaifa hadi kidunia nzima kwa ujumla. Kwa kuanzia wanaweza kufanya hivi;
1. Jitahidi kutafuta na kupata taarifa nzuri kwa wingi zaidi: Tafuta taarifa nzuri kuwahusu watu wengine, taarifa nzuri kukuhusu wewe mwenyewe, taarifa nzuri kuihusu nchi yako na kuhusu mataifa mengine. Kuwa nazo nyingi maana zinakujengakuwa mtu mzuri zaidi. Mwenye will njema zaidi. Hata video zenye visa vyema vya upendo zinasaidiaga usipuuze hili. Angalia nyingi uwezavyo. Unadhani ni kwa nini wadada wanaoangalia ‘za-kikorea’ nyingi wanakuwaga na mahaba flani ivi amaizing.
2. Hakikisha kila taarifa unayosambaza ni habari njema: Hii itakujenga zaidi na itafanya uendelee kupokea taarifa njema pia. Kusambaza habari njema humfanya mtu kuwa mwema zaidi kwa sababu ya uhusiano. Chochote unachoamua kujihusianisha nacho jua kinakujenga hivyo. Jiulize tu kile kipindi nchi nzima ilikuwa inasambaza habari za maendeleo tu. Unakumbuka kila mwananchi alianza kujisikiaje? Yaas kimaendeleomaendeleo ndiyo. Vijana tuliongezeka katika kuwaza kuanzisha viwanda ukilinganisha na kuajiriwa. Kila raia akaanza kuwa na ile ‘mentality’ ya kujiamulia mambo yake kama yeye [akiiga nchi inachofanya] na kuuongoza uchumi wake kama yeye [akiiga pia nchi ilichokuwa inafanya] na hata kuuchukia uovu na kupiga vita uzembe na ufisadi kama tu nchi ilivyotuaminisha kuwa inafanya. Na matokeo kwa kweli yalikuwa mazuri nadhani wote ni mashahidi. Taarifa zinazozagaa zina mchango mkubwa sana katika akili zetu binafsi, jamii zetu na taifa kwa ujumla.
4. Usisambaze taarifa mbaya kwa kuisifia, tena usisambaze taarifa mbaya isiyokamilika. Kuna sababu vitabu vya hadithi za watoto wakieleza kuhusu mtu mbaya wanamalizia na baya alilopata. Mfano ukiona taarifa inasema ‘milioni mia tisa zatafunwa na kigogo wa serikali’ USISAMBAZE. Ila unaweza labda ukasambaza bora ile inayosema ‘Kigogo wa serikali atumbuliwa, afilisiwa baada ya ubadhirifu wa milioni mia tisa, pesa hizo zitapelekwa kwenye mradi uliosuasua kutokana na ubadhirifu huo’. Kwa kufanya hivyo[au kutofanya] unajisaidia wewe mwenyewe jamii yako, kizazi kijacho, taifa na dunia yote kwa ujumla.
Vizuri zaidi ni kuachana tu na habari zote mbovu, usizipe airtime, usisambaze viscreenshot [tena hivi ndo vibaya zaidi], wala usisifu masuala mabovu. Usiishie kusoma vichwa vya habari na kupokea ujinga, chimba zaidi. Na natoa wito kwa vyombo vya habari kuzikamilisha habari zao kabla ya kuzirusha hewani. Mhoji mtuhumuji mhoji mtuhumiwa wahoji wote wanaohusika ndio uturipotie, la sivyo kazi yako itakuwa mbovu. Ikibidi block watu walioamua kujihusisha na taarifa mbaya marakwamara.
3. Ukikutana na taarifa mbaya, usiamini tu moja kwa moja kuwa dunia ndivyo ilivyo. Ichuje. Nenda ndani zaidi katafute sababu ya jambo hilo baya kufanywa. Tafuta sababu za kuridhisha ili kuiridhisha nafsi yako mpya ambayo kutokana na taarifa nyingi nzuri ilizonazo; imeamini kwamba dunia na walimwengu ni wazuri ila kuna wakati sababu fulani fulani zinaweza kuwafanya wakatenda ubaya. Tafuta hizo sababu ili ujue namna ya kuepuka maovu na kubadilisha mambo yawe mema na matamu zaidi
4. Usitafute kuwasamehe wakosefu tafuta kuwaelewa. Tafuta zaidi kuelewa chanzo cha mtu kukosea. Hata mtu akija kukuomba msamaha usiseme tu nimekusamehe hapana. Mwambie kwanza ningependa kufahamu sababu zilizofanya ukafanya vile, what were you thinking at at a time. Ukimuelewa utashangaa vile utakavyosamehe kwa moyo mkunjufu kabisa. Na kwa kuongeza utakuwa umejua zababu za ‘otherwise a good person’.
Natamani nisisitize zaidi kwenye habari njema, taarifa nzuri yaani sijui nisemaje. Okay labda motisha nyingine ni pale mtu anajua kuwa anachokifanya ni kujitolea kwa ajili ya wengine. Basi ndugu sambaza habari njema kama sehemu ya kusaidia masikini wa kimawazo na wengine. Sambaza habari njema za nchi kama sehemu ya kuitangaza nchi kiutalii ili watu wainuke kiuchumi. Sambaza habari njema za dunia kama sehemu ya kuiombea huruma ya Mwenyezi Mungu. Unakumbuka Ibrahimu alivyojitahidi kuleta wazo la kwamba watu wema bado wapowapo labda wema wanaishi. Wakati unafanya hivyo tambua kuwa wewe mwenyewe hausahauliki, mambo mema yanakujalia wewe kwanza, yanafurika halafu ndiyo yanabubujika na kuwafikia wote ambao habari zako njema zitawafikia. Yote hayo tunafanya ili kuwezesha amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema. Peace and good ‘will’ among men on earth. Peace
Kitu cha kutia moyo tu ni kwamba, ukishaweka uamuzi wa kuiendea njia fulani katika hili suala la will/utashi. Unakuwa ni kama tayari umeshafikia ila hatma unayoitamani hata kama bado upo unatembea katika njia ya kuielekea hiyo hatma. Huamini jiulize tu jinsi uzima, kweli na njia vinavyofanya kazi. Ni vitu ambavyo huwi navyo ‘having’ bali unakuwa hivyo ‘being’. Amua sasa kuwa wa upande wa mema, na mwema umeshakuwa kitakachobaki itakuwa tu ni kutembea katika wema. When your will is good, YOU are good. And that is good a good thing both in itself and outward!
NB: Mada hii ni ndefu imebidi kufupishwa kutoka katika blogu, ikiwa ungependa kufahamu saidi kuhusu utashi huru na baiolojia ya miili yetu waweza kuiona hapa Utetezi kwa Utashi Huru Binafsi [kibaiolojia zaidi]– An Appeal to Personal Free Will [mostly biological].
Nimekumbuka! Kipande muhimu nilichoruka ni kuwapa japo mfano mmoja. Wacha niuweke hapa isiwe lazima kuutafuta huko katika blogu; 'Ili kufikia majibu haraka tuangalie watu wawili. Rastaman, pamoja na bosi CEO wa kampuni kubwa ya madini.
Rastamani anachokijua hadi muda huu ni; Yeye ni mtu wa amani, watu wote ni kama ndugu zake na wako na amani naye, hapendi kuvunja sheria na kuwaumiza watu wengine na watu wengine pia wanarudisha wema huo. Hana vita na utulivu ndiyo hali ya kimaisha. Sasa huyu Rastamani hajiandai na vita yoyote, hivyo mwili wake ‘will’ yake haiamurishi kutunza chakula na maji mwilini anakuwa kimbaumbau. Suala la uzushi kwamba nywele zinakondesha limetokana na kuwatazama marasta wanaofuga nywele ndefu. Right observation! Wrong conclusion!
Tukirudi kwa CEO wa kampuni ya madini yeye anachokijua hadi wakati huu ni; Yeye ni mtu anayejitahidi kuwa na amani lakini kazi inambana, watu wote ni kama washindani wake kwa hiyo kuna kajiuadui fulani kamaendeleo lakini sio ka shari kihivyo, Sheria zipo na mapungufu ndiyo maana mda mwingine baadhi yake anaziepuka na anafahamu washindani wake pia hufanya vivyohivyo. Kuna vita ya kimaendeleo inaendelea na haijawahi kutokea kukawa na utulivu wa kudumu katika soko la dunia.
Sasa huyu kibosile yampasa kujiandaa na hii vita ya chinichini, hivyo ‘will’ yake itauamurisha mwili wake japo kuwa na akiba kiasi ya chakula na maji na ndiyo maana anakuwa boss-kitambi-meneja!. Suala la watu kuhusianisha wingi wa pesa na kitambi lipo sana tu. Hapa pia ndio tunasema right observation! Right association, conclusion awaiting scientific study.'