Mbinu za Kuidhoofisha CCM

Post yangu inaomba michango ya watu, ungeweza tu kusema katiba mpya bila kusema nazuga watu.

Uzoefu unaonyesha machafuko tu ndio huleta mabadiliko ya kweli Afrika. La kwanza kwa sasa ni kuhakikisha watu wengi hawajitokezi kupiga kura, kisha kutumia matatizo yanayoshindwa kutatuliwa na serikali, ikiwemo na ugumu wa maisha kufanya vurugu ili kupata mabadiliko ya kweli. Pia kutokushirikiana na wanaccm kwenye misiba, sherehe, michezo nk. Njia hizi zitaleta muafaka taka wasitake.

Sasa hivi viongozi wa CCM wakiitisha mikutano ni watu wachache sana huhudhuria, inatakiwa watu wahamasishane kuwasusia huku ikitolewa elimu dhidi ya uwepo wa CCM madarakani na madhara yake. Vikao vya bunge zikiletwa mada zake ni kuziponda mwanzo mwisho ili bunge lizidi kudharaulika.
 
Hivyo vitu viwili huwezi kuvifanya wakati mmoja. Ukiidhoofisha CCM wakati vyama vya upinzani bado havijawa imara unatengeneza power vacuum kitu ambacho ni hatari kwa nchi na kinaondoa usalama. Huwezi kuimarisha vyama vya upinzani wakati CCM tayari iko imara. Itafanya kila mbinu kudhoofisha upinzani na kubaki madarakani. Ndiyo maana siasa za vyama vingi ni rahisi kuanza nchi ikiwa changa. Ukivileta baada ya chama kimoja kukaa madarakani miaka mingi ni vigumu kukitoa na ndiyo matatizo ya nchi nyingi za Afrika pamoja na Tanzania. Ilitakiwa wakati ule wa nchi za Afrika zinapata uhuru zianze na vyama vingi. Zingeweza, leo demokrasia ingekuwa imara sana Afrika.
 
Kipi ambacho hawajakipata na wapo tayari ni coalitions government ambayo ndio future ya new democracy.
Zanzibar walipata Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi tena inayojumuisha watu kutoka vyama vyote vya siasa.

Lakini mpaka leo hawajapata wanachokitaka pamoja na kuwa serious kuliko kawaida yenyewe.
 
Kipi ambacho hawajakipata na wapo tayari ni coalitions government ambayo ndio future ya new democracy.
Coalition Govt Haina future kwa watu wa kawaida.

Ni aina ya njia ya wanasiasa kugawana keki ya taifa Ili kuepusha kelele.

Ni sawa na Simba na Chui kuacha kugombania swala, na badala yake kukaa pamoja kula. The Berlin conference trick!!
 
Nimesoma mawazoyenu hakuna chama cha siasa kinaitwa ccm hiyo ni camouflage tu,ina trap watu wajue ni wanachama wa chama cha siasa kumbe ni washabiki wa dola.Ccm kitakuwa chama cha siasa wakitenganisha kofia mbili uenyekiti na urais.Bila huvyo kila kukibadika awamu kuna wanaccm wataumizwa.
 
tulipokosea ni pale ambapo mali na ukwasi wa CCM kipindi cha chama kimoja kuendelea kumilikiwa na CCM kipindi cha vyamaq vingi......
tulitakiwa mali za CCM ile zigawiwe kwa serikali au kwa vyama vyote kwa kipindi hicho...
kwa sasa chadema au act haiwezi kupambana na ccm kama vyama vyetu vya upinzani vilivyogubikwa na umasikini .....
 
Ni vyama vya upinzani kuweka mapandikizi ndani ya CCM

Upinzani ichochee kila mgogoro unaibuka ndani ya ccm na si kuwaunganisha,!

MF,

Kundi LA Magufuli lingepata uungwaji Mkubwa na upinzani ili kuhakikisha ccm inapasuka vipandevipande
 
 
Hapo mwisho bado si swali sahihi. Kabla umesema vizuri kabisa kwamba lengo ni kuweka level playing field kwa vyama vyote. Sasa tatizo au suala la kushughulikiwa ni kuondoa ukiritimba (monopoly) wa chama kimoja ambacho kina hadhi batili ya chama dola na sio kutafuta namna ya vyama vya upinzani kuishinda CCM. Isije kuwa tunaondoa CCM na kuweka chama dola kingine. Demokrasia inataka uwazi (transparency) na ushiriki wa wananchi katika kuondoa chama dola na kuweka level playing field; sio mbinu za “uchochoroni”.

Kinachoidumaza Tanzania hadi leo ni kuwa na chama na wanasiasa wenye guarantee ya uongozi wa nchi tangu uhuru. In a true democracy, political leaders have to be kept on their toes with the knowledge that they can be booted out of power and replaced any time - by the will of the people.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…