Mbinu za kukabiliana na mbu

Mbinu za kukabiliana na mbu

Habari zenu wadau,

Leo tupeane mbinu mbalimbali unazotumia kukabiliana na mdudu msumbufu mbu.

Wengi wetu hutumia chandarua lakini zinaleta bad looking ya chumba chako. Pia si muda wote utakua kitandani ndio ujikinge na mbu.

Ukitumia spray nayo maharufu makali, ukifunga dirisha especially hizi aluminium windows wanapenya kama wote.

Basi tujuzane njia nzuri unayotumia ili nasi itusaidie.

Wasalaam.
Nawaachia kidogo wakishiba naanza kuwaua, wanakua hawawezi kukimbia tena! Kwahio kesho huwezi kukuta mbu tena
 
Panda kivumbasi (holy basil) eneo ulilopo, mbu hawatazaliana hovyo, pia uwe unachoma majani yake kidogo chumbani, moshi ule na mbu havipatani.

Pia ni mmea mzuri wa kufukuza roho chafu na mambo ya giza, wahindi wanauheshimu sana huu mmea, nyumba nyingi lazima utaukuta hata ndani
Ungekuja na pacha yake mkuu
 
1. Twanga vitunguu swaumu, then weka karibu yako au kwenye kona za room ile harufu watakimbia,
2. Kuna dawa zipo karakoram sokoni ( kule gorofani )
zinachomwa kwa umeme zinauzwa elfu 5.. ( haswa duka la madawa ya kilimo)
3. Kuna kiwanda cha kuuwa vilui lui via mbu, kipo kule kibaha wana dawa zao ni nzuri ina zinataka maturities ya kaya kuanzia 3 au 4. Zenyewe zinawekwa kwenye mazalia ya mbu na zinaua kweli....
 
Aisee kumbe utajiri umejificha hapo tu, kwetu yapo na tunayaita hivyo MALUMBA…. mara nyingi tulipenda kutumia mbegu zake ikiwa mtu anaumwa macho.

Hebu niambie, kuhusu utajiri nifanyeje?[emoji1614][emoji39]
Na huwa tunaweka madirishani pia ili kuzuia mbu kuingia ndani, kutoa uchafu ulioingia kwenye jicho kwa kuweka mbegu zake ambazo huenda kukusanya uchafu wote na kuutoa pamoja na tongotongo
 
Back
Top Bottom