Tinov 1998
New Member
- Aug 26, 2022
- 3
- 4
Kutokana na ukuaji wa shughuli za binadamu za uzalishaji kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira Hali inayopelekea kubadilika kwa tabia ya nchi. Aidha shughuli za kibinadamu Kama vile ukataji miti, viwanda, kilimo na usafirishaji vimepelekea mabadiliko hayo kwa wingi.
Baadhi ya madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi ni pamoja na kubadilika kwa misimu, joto kuongezeka, ukame, mafuriko, kuhama au kutoweka kwa baadhi ya mimea na wanyama.
Kutokana na teknolojia ya umwagiliaji kuwa mdogo katika kilimo nchini wengi tunategemea mvua za misimu kwa uzalishaji. Kukosekana kwa mvua za kutosha kwa wakati hupelekea uzalishaji kuwa chini ya wastani.
Pamoja na hayo kumekuwa na hali ya kutoweka au kudhoofika kwa baadhi ya mimea kutokana na kushindwa kustahimili mabadiliko hayo.
Kwa ujumla madhara yote hayo hupelekea kukosekana kwa chakula cha kutosha (food insecurity), ubora mdogo wa mazao, upatikanaji hafifu, na mfumuko wa Bei za vyakula
Aidha zifuatazo ni baadhi ya mbinu zinazoweza kuleta matokeo chanya kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchini katika kilimo nchini:
Mosi, kuhamasisha utunzaji wa mazingira, hii ni pamoja na kutoa elimu kupitia wadau na sekta binafsi kuhusu upandaji miti, na utunzaji wa mazingira kwa ujumla ili kuepukana na mabadiliko hayo.
Pili, kuepukana na matumizi yasiyokuwa sahihi ya kemikali katika kilimo, baadhi ya kemikali na viatilifu katika kilimo hupelekea kuongezeka kwa gesi za nitrojeni monoxide, kabondaoksaidi, kloroflorokarboni (greenhouse gases) na menginezo ambazo huharibu ozoni ( ozone layer depletion) Hali inayopelekea miale kupita duniani kirahisi na joto kuongezeka. Kemikali hizo ni pamoja na mbolea za viwandani na viuagugu na wadudu.
Tatu, kubuni aina za mimea (Varieties) ambazo zinauwezo mkubwa wa kustahimili mabadiliko ya tabia ya nchi (drought resistant Varieties).
Nne, kuwekeza katika kilimo Cha umwagiliaji ili kuendeleza uzalishaji hata mvua zisiponyesha.
Tano, kuimarisha viwanda vya uchakataji na uongezwaji thamani za mazao ( Value addition) ili kuwa na uhakika wa chakula bora wakati uzalishaji ukiwa mdogo.
Sita, kutumia njia za oganiki ( Organic farming technique) ambayo haihusishi matumizi ya kemikali za viwandani.
Saba, Kuboresha uzalishaji katika mazingira Kama vitalu nyumba ( controlled environment farming)
Mwisho, kubuni njia mbadala za nishati ili kupunguza matumizi ya mkaa ambayo hupelekea ukataji miti na kusababisha mvua kuwa chache ( climate smart agriculture).
By Tinov 1998
0688503442.

Upvote
1