Mbinu za kuwa msiri

Mbinu za kuwa msiri

Pia mkuu jitahidi ujifunze utofauti kati ya Mystery na secret.

Mafanikio hubebwa na Mystery na sio secret

Secret ndo huwa zile siri zinazokuhusu wewe na binadamu Ila mystery ni siri yako wewe na MUNGU wako.

So jikite katika mystery zinavyo operate kwanza na sio kupambana kuficha secret ambazo hauwezi .
 
Habari zenu Wana jukwaa
Kama kichwa Cha Uzi kinavyosema naombeni mnisaidie mbinu za kua msiri
Baadae ya kua mtu mzima Kuna namna ninawaona ndugu na watu wa karibu kama watu wenye choyo na wengi hawapendi mtu afanikiwe iwe ni ndoa kazi au biashara
Sasa ninaomba mnipe mbinu gani nitumie ili maisha yangu yawe ya Siri nimeshahangaika sana Kuna vitu nisipowashirikisha Ina kua ni ugomvi hivyo inanilazimu niwaeleze mipango yangu yote hiki kitu sikipendi na hata nikiwama hawana msaada wowote ule
Nifanyaje wasijue maisha yangu na ukizingatia ni watu wangu wa karibu
Natanguliza shukran
siri ya mafanikio ni kutunza siri ambayo ni sauti za nasibu iliyo ndani yako
 
Kwa watumiaji wa Tigo Pata GB za bure kwa kufuta maelekezo haya.

1. Ingia TigoPesa app (Kama hauna download play store)

2. Ingia Invite & Earn

3. Bonyeza Redeem

4. Weka hii code 2ZJVO8ZK

Baada ya hapo utapata 2GB na DK kibao bure kabisa!!
 
Kabisa yani kiufupi ni wachawi km wengine tu
Ni wachawi haswa na wanamtumia bila yeye kujua, sasa kashashtuka aache kuwataarifu itakuwa ngumu mwanzoni lakini baadae mambo yatabadilika.

Ukishakuwa above 18 hakuna wa kuyatawala maisha yako zaidi yako mwenyewe labda kwa kupenda kwako uliruhusu hilo.
 
Mi nilivyo kauzu 😃😃 sipendagi mazoea ya kipuuzi hao ndg wangekaa mbali sana na mimi
 
Mi nilivyo kauzu 😃😃 sipendagi mazoea ya kipuuzi hao ndg wangekaa mbali sana na mimi
Ndivyo inavyotakiwa, kwa watu ambao tulishakuwa karibu sana na ndugu ni bora zaidi kuwa nao mbali hata heshima inakuwepo. Watu wengi huogopa maneno maneno bila kujua kwamba maneno huwa yapo tu hata iweje.
 
Ni wachawi haswa na wanamtumia bila yeye kujua, sasa kashashtuka aache kuwataarifu itakuwa ngumu mwanzoni lakini baadae mambo yatabadilika.

Ukishakuwa above 18 hakuna wa kuyatawala maisha yako zaidi yako mwenyewe labda kwa kupenda kwako uliruhusu hilo.
Yaani ni kazi nimeshakua mtu mzima Sasa sijui wanataka niwe fukara au maana sijawahi kuonana hata siku Moja wakinipa msaada wa kipesa hata nawazo ya kimaendeleo
 
Yaani ni kazi nimeshakua mtu mzima Sasa sijui wanataka niwe fukara au maana sijawahi kuonana hata siku Moja wakinipa msaada wa kipesa hata nawazo ya kimaendeleo
Achana nao ishi maisha yako, jali maisha yako na sio wayatakayo, toka hapo ulipo kajitegemee bila wao.

Kwa kukusaidia kama una toxic behaviour kama za addiction jitahidi uache ili uweze kusimama peke yako.
 
Kuna mahala unazingua, ni simple tu usijibu maswali juu ya mada usizotaka kushare au ndugu zako ni vichaa watakutenga?
 
Tatizo una shobo sana, jitahidi kubalance shobo.
Halafu km mdomo unakuwasha kuongea, anza kuongea story za chai.!!
Wanyweshe chai mpk walewe, wasijue ukweli na uongo ni upi?? Lakini wewe ushaongea UONGO

Mfano wewe mfupi, waaminishe wakuone mrefu.
Una shape, waaminishe ww ni flat umekuja kuja duniani kabla haujakauka…,. Yani wavuruge wavurugike.
 
Unaishi na watu ambao wanapenda kucontrol wengine, ishi maisha yako mkuu usiri ni muhimu sana kwako.
Hii tabia ya kucontrol wengine anayo sista yangu,huwa mimi tunazinguana sana naweza nikakaa hata zaidi ya nusu mwaka nisimpigie simu hata kumsalimia tu,wengine wanasema niwe najishusha nilikataa kabisa. Analalamika kuwa mimi msiri sana,kuna siku nkamwambia dili moja hivi akaenda kunichomesha,namlaani hadi leo hii. Nikiulizwa kwa nini huwapigii ndugu zako simu najibu simu yangu haitumii mafuta ya alizeti inatumia vocha..
 
Sasa ni watu ninaoishi nao hata nikipata dili la kazi wanataka nijue ni wapi nafanyia hiyo kazi mpaka mshahara Mimi sipendi na siku nisipokua na ishu wanakaa mbali na Mimi hata mia yao siioni
Dah😭
Kwanza hama home au kaa mbali na maeneo yao!!

Huwezi fanikiwa kama Kila mtu anajua Kila kitu!akijua kinayeyuka!!

Tafuta room kimya kimya!!maendeleo bila ubinafsi huyapati trust me!
 
Hii tabia ya kucontrol wengine anayo sista yangu,huwa mimi tunazinguana sana naweza nikakaa hata zaidi ya nusu mwaka nisimpigie simu hata kumsalimia tu,wengine wanasema niwe najishusha nilikataa kabisa. Analalamika kuwa mimi msiri sana,kuna siku nkamwambia dili moja hivi akaenda kunichomesha,namlaani hadi leo hii. Nikiulizwa kwa nini huwapigii ndugu zako simu najibu simu yangu haitumii mafuta ya alizeti inatumia vocha..
Wadada wanayo sana hasa akishakuzidi kiuchumi, sio lazima kuwasiliana kila mara kama hakuna haja hiyo, kiasili wanawake wanapenda sana kujua na kufuatilia maisha ya watu na haiishii tu hapo.

Ulishajiuliza kwanini kwenye familia na miji wakishaingia wanawake hata kwa kuolewa mambo hubadilika sana? Sababu ni hiyo ya kufuatiliana na kusambaza maneno.
 
Back
Top Bottom