Mbinu za kuwa msiri

Mbinu za kuwa msiri

Mtu hafundishwi kutunza siri.

Siri ni ile uijuayo wewe mwenyewe pasipo kumshirikisha mtu.
Sasa kama wao wanafahamu mambo yako unafikiri wameyajuaje pasipo wewe kuwaambia?
 
Acha kuweka kila kitu mtandaoni na uepuke kuzungumza sana mambo yanayo kuhusu stori zako Acha wasimuliane wao kwa wao ila we usiende kuprove
 
Habari zenu Wana jukwaa,

Kama kichwa Cha Uzi kinavyosema naombeni mnisaidie mbinu za kua msiri.

Baadae ya kuwa mtu mzima kKuna namna ninawaona ndugu na watu wa karibu kama watu wenye choyo na wengi hawapendi mtu afanikiwe iwe ni ndoa kazi au biashara.

Sasa ninaomba mnipe mbinu gani nitumie ili maisha yangu yawe ya Siri nimeshahangaika sana Kuna vitu nisipowashirikisha Ina kua ni ugomvi hivyo inanilazimu niwaeleze mipango yangu yote hiki kitu sikipendi na hata nikiwama hawana msaada wowote ule.

Nifanyaje wasijue maisha yangu na ukizingatia ni watu wangu wa karibu

Natanguliza shukran.
Bado hujakua

Ukianza kukua Tu utaanza kuwapozea na kutojali wanaongea nini juu ya mamabo yako.

Hao ni binadamu ambao wanautashi wao kwahiyo huwezi kuwazuia wasikuchukie ukianza kuficha mipango yako.
 
Kuna vitu nisipowashirikisha Ina kua ni ugomvi hivyo inanilazimu niwaeleze mipango yangu yote hiki kitu sikipendi na hata nikiwama hawana msaada wowote ule.

Nifanyaje wasijue maisha yangu na ukizingatia ni watu wangu wa karibu

Natanguliza shukran.
Broh ukweli ni kwamba kwasasa unapenda, kuna siku litakukuta jambo, hapo ndio utaacha kupenda kwa vitendo.

Ila naomba kujua, hao ni kina nani ambao ni lazima uwaelezee mipango yako yote? Hakuna mwenye kuweza kukulazimisha ufanye hivyo, labda mkeo kwavile ndio jukumu lako.
 
Broh ukweli ni kwamba kwasasa unapenda, kuna siku litakukuta jambo, hapo ndio utaacha kupenda kwa vitendo.

Ila naomba kujua, hao ni kina nani ambao ni lazima uwaelezee mipango yako yote? Hakuna mwenye kuweza kukulazimisha ufanye hivyo, labda mkeo kwavile ndio jukumu lako.
Mimi ni ke na Hawa ni walezi wangu
 
Ukitaka kusema, Meza mate mara tatu mfululizo bila kuhema, utakuwa ile siri yako umeimeza. 😎😎

Na waharibu au wapinga maendeleo yako ni wale wa karibu, hakuna anayependa mtu atoboe
 
Naishi nao Bado
Kama unaishi nao/chini yao, basi bado wana haki ya kukuuliza mipango yako. Japo vipo ambavyo kwa rika lako unaweza kuvifanya siri.

Waambie yale wanayotakiwa kuyajua. Siku utakayotoka hapo nyumbani (kuolewa, au kupata kazi sehemu ya mbali), hapo ndipo utaanza kujimiliki.
 
Natamani kutoka ila nawaagaje ndo shida 🤔🤔🤔
Aga wazazi wako tu inatosha sana, hao ndio wenye baraka kwako, kama hawapo aga yeyote. Fanya maamuzi magumu na usiogope lawama vinginevyo utaendelea kuupalilia umasikini wako na umri unasogea.

Alafu acha kuogopa watu, waheshimu. Wewe ni muoga muoga.
 
Back
Top Bottom