Pre GE2025 Mbinu za wizi wa kura zinazotumiwa na CCM zabainika; ni hizi hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ccm haijawai kuiba kula Sku zote Ccm anashinda ushindi wa kihalari kitu msichokijua Ccm iko mbele kiakili kimawazo na kimbinu na ndo jaja ya ushindi wake

Kuna vitu km viwili niwewai vishuhudua moja
Sku moja au ile sku ya uchaguzi ccm utumia watu kununua wapiga kula yan mtu anatoka kwake kwenda kupiga kula njian anakutana na Ccm wanampa pesa mwananchi anabadili mawazo hapo hapo anaenda kuwapigia kula

Lakin pia kuna tabia ya vijana weng especially bodaboda na wale vijana wasojitambua huwa wanauza kadi zao za kupigia kula so mwisho wa sku sku ya kupiga kula hawaendi sabu washauza vitambulisho vyao vya kupigia kula

Na hii njia yakununua kadi za wapiga kula hutumika sana
Unaweza enda mkutano wa chadema ukakuta vijana kibao wanaimba na kusukuma gari la mgombea wai kumbe yameshauza kadi zao za kupigia kula Ccm., viongozi wa chadema wanaona tunavijana weng sana tutashinda uchaguzi kumbe vijana hao hawana kadi zote zishauzwa zko kwa mgombea wa Ccm zimetunzwa ad uchaguzi ukiisha ndo wanarudishiwa
 
Ku
Kula ndo nini
Jifunze kuandika kwanza
 
Wewe ni mpuuzi sana ujue mkuu. Mwaka 2020 kulikuwa na uchaguzi?
 
Jana nimeongea na mtu mmoja aliyekuwa akijihusisha na kuorodhesha wapigakura akaniambia CCM walimletea orodha ndefu ya wapigakura kweny daftari na kumtaka ataingize kwenye daftari. Kumbe hawa jamaa wana mbinu nyingi za wizi wa kura.
 
Je mtu anateuba kura ataogopa kuibamali za umma?
 
Mzee wa bao la mkono aliweka kila kitu wazi. Huenda tangu vyama vingi vianze CCM "haijawahi kushinda " angalia wakati wa Mrema. Alishinda Mrema sema tu nae ni mtu wa system.
 
Safari hii patachimbika
Kwenye hizi chaguzi kuna kitu kikubwa sana kinakosekana na sijawahi kuona watu wakipiga kelele kukidai na ndio hicho Chama A wanakitumia kuwapigia Chama B natamani niitoboe hii Siri ila ngoja subiri niushirikishe Ubongo nikidakwa na kuvushwa mkoa mpaka mkoa nitakua pekeyangu ngoja nile buyu tu kwanza ila TEHAMA imewekwa kando kura zinahesabiwa na watu kwa mikono na watu wana uwezo wa kuongeza au kupunguza ila Mashine hua haifanyi huo ujinga km ni 10 itaonyesha 10 km ni 100 itaonekana 100
 
CCM hawajawahi kushindwa kuchezea hata mashine iongeze kura. Tazama jinsi wanavyochezea mashine za EFD na kuiba pesa za umma kwa manufaa ya matumbo yao makubwa kama mapakacha yasiyowahi kushiba hata siku moja. Wapuuzi sana hawa.
 
CCM hawajawahi kushindwa kuchezea hata mashine iongeze kura. Tazama jinsi wanavyochezea mashine za EFD na kuiba pesa za umma kwa manufaa ya matumbo yao makubwa kama mapakacha yasiyowahi kushiba hata siku moja. Wapuuzi sana hawa.
Mashine zisiwe chini ya Chama A wasimamizi kutoka Nchi za mbali ndio wawe wasimamizi wa Mashine hizo au hilo pia linashindikana kufanyika mnaogopa Chama A watagoma au nyinyi ndio mtagoma wasimamizi wa kutoka Nchi za mbali kusimamia Mashine nao wataiba kura? Na hilo pia hamtaki sasa mnataka nini? Maana hilo ndilo ambalo Chama A wanaliogopa kuliko jambo lolote lile kwenye hii dunia likitokea tu kwesha habari yao Mashine haiongopi fingerprints zako James haziwezi kusoma fingerprints za John hata ufanyaje
 
Hili kwenye utawala wa CCM ni vigumu kukubali upigaji kura wa aina hii
 
Hili kwenye utawala wa CCM ni vigumu kukubali upigaji kura wa aina hii
Na ndio Siri ambayo wengi hawaijui na hawajisumbui kuifanyia kazi likiletwa Mashine linachukua kura 1 ya kila mpiga kura na utambulisho wake na hio Mashine wasikabidhiwe Chama A waichekeche km kuikagua ikaguliwe ikiwa wote wapo yaan wale wanaokuja kusimamia ndio wawe wanakuja kuisimamia na Mashine iwekwe kwenye uangalizi mkali, Mashine haidanganyi 1 itasema 1 haiwezi kua 1 Mashine ikasoma 1000
 
Shaurini vijana wenu waache kuuza vitambulisho vya kupigia kura uwo ndo wizi wa kwanza
Labda huu uchaguzi mdg ndo akuna vitambulisho ila zile chaguzi kubwa vijana wenu wanauza sana kadi za mpiga kura mwisho wa sku awapigi kura

Unakutana na vijana 50 wanapiga kelele mtaani people power kumbe katika hao 50 ni vijana 30 ndo wanakadi wengne wote washauza kadi zao
 
Mbinu inayo tumika kwa sasa ni ya kuwatumia sana Polisi kwenye kufanikisha wizi kura, Polisi wana play part kubwa sana kwa kushrikiana na wana CCM.

Police walishirikiana vilivyo na wana CCM kufanikisha wizi na hii ni planed kutoka juu sio kwamba ni bahati mbaya.

Kuna maadai baadhi ya maeneo gari za polisi ndizo zilizo kuwa zinatumika kusambaza kura feki.

Sehemu zingine ilipo kuwa inatokea Upinzani wanawawekea CCM ngumu kuingiza kura feki waliamuwa kuwaita polisi na wakifika wao ni kukamata hadi mawakala na kutokomea nao kusiko jilikana au kupiga mabom ya machozi.

Kule Karatu huwezi amini Green guard walikuwa wanazunguka na gari za polisi kwenye vituo vya kupikura.

Adui mkubwa anaweza
akawa CCM ila Back up yao kubwa sana iko Polisi, polisi wanawapa sapoti kubwa sana CCM kwenye kufanikisha wizi wa kura.

Hii ni mbinu imeanza awamu ya Magufuri.
Polisi ni adui mkubwa sana wa Demos huenda kuliko hata CCM wenyewe.
 
Polisi na ccm ni samaki na maji. Huwezi kutaja kimoja bila kuhusisha kingine. Ndo maana umuhimu wa katiba mpya upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…