Mbinu zipi wamezitumia Wakinga kuwa wafalme Kariakoo?

hizi biashara zote ulizotaja hazifikii hata asilimia 2 za biashara za kariakoo mkuu.
 
Mkuu mimi sitabishana sana na wewe cos tunazidiana ujuaji kuna unayoyajua wewe mimi siyajui kuna ninayoyajua mimi lakini nakwambia kwa mfumo wanaoenda nao Wakinga wengi hawana guarantee ya kudumu sokoni miaka 10 labda kama wataamua kuwa wapiga winga.

Ninae rafiki yangu wa Kikinga ameukimbia mji na madeni juu kwa mambo haya haya ya kuweka faida 1,000/=,2,000/=,mtu unauza box umeinunua 62,000/= bila receipt yenye VAT unauza 64,000/= faida 2,000/= hujatoa receipt ya kueleweka anakutana na tra unaandikiwa penalty 3mill au rushwa 800K utegemee kudumu sokoni?

Uza vingi kwa bei ndogo kwa sababu umeviingiza mwenyewe siyo mtu ni vendor utake kushindana na ma-giant sokoni utang'atwa tu.
 
Kumbe ni rafiki yako moja tu mkuu, hio haiwezi wakilisha hata theluthi ya average, nikwambie tu hata kwa waarabu humkosi aliekimbia kwa madeni.

Wakinga wapo wengi tu tunaenda kugombania bidhaa zao kwa bei zao chee na wapo wandunda miaka na miaka.

Hayo mambo ya TRA yanakuogopesha lakini ni mambo yakawaida sana kwa wanaofanya biashara Kariakoo. Hapo Kariakoo ukiwaogopa TRA huwezi fanya biashara
 
Waeleze nafikiri mtoa mada amekuja Kariakoo jana Mchana
 
Kaahhh wee mfukunyuku balaaaa
 
Mkuu umemshushia gazeti hahah
 
Mods huu uzi ufungwe kijana kamaliza Kila. Kitu hapa k'njaro 7 Kinga 0
 
Asanteeeeee sana hii niliitafuta nikaikosa wakinga ni hopeless wanapewa nguvu na jina na watu wachache wenye mawe mjini ila bado hawajafika level za wachaga
Naona wanadanganywa na Vunja Bei ndo wanasema wote wana magorofa[emoji23][emoji23]
 
Nimekwambia naogopa TRA mimi?

Huyo ni kama sample tu maana ndiye niliyekuwa nimezoena nae ila ni wengi sana wanakimbia sokoni,shida nilichogundua wewe unataka debate naachana na wewe.
 
Kwa Tanzania ukitoa ngozi nyeupe zenye utajiri mkubwa yaani familia moja utajiri lukuki, wanaofuata kwa kumiliki uchumi ni wachaga, brothers wachaga stage ya uchuuzi walitoka muda mrefu kwa sasa wanamiliki makampuni, viwanda, uagent wa bidhaa mbalimbali na hata kwenye shule walisoma zamani sana na kila sehemu mchaga yupo na kila mkoa na wilaya huwezi kumkosa acha hapo kariakoo, wakinga wanakujakuja lakini sio level za wachaga bado sana ni vyema kuwapa heshima wakinga wanapambana sana kama hata waha wanavopambana lakini tusiwalinganishe hawa watu wako mbali zaidi
 
Ustaarabu wa makabila mengi kurudi kwao hasa kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka au kujenga kwao kijijini makabila mengi waliiga kutoka kwa wachaga na kidogo kwa wahaya, ukienda vijiji vya makete na Kilimanjaro ndio utaona utofauti wa civilization ya watu toka zamani,
 

Bila shaka wewe Ni Mkibosho Tena anaye penda sifa sio mbaya Ila siku Akiingia Kiongozi mwenye husda na kaskazini Ataanzia kwenye huu uzi wako.
Hivyo kwa nmna moja au nyingne umeanika watu Hapa bila kujua! Je umelipwa kwa kufanya hivi? Bila shaka hapana Ila huu Uzi Ni chanzo kizuri Cha info....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…