Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
UTANGULIZI
Lugha ya kigeni niile lugha ambayo haipatikani katika jamii ya mjifunzaji na kuwa hawezi kujifunza lugha hiyo bila kufundisha. Niukweli usiopingika kuwa na ufahamu wa lugha nyinginezo za kigeni zaidi ya Ile lugha yako Kuna faida kubwa katika ulimwengu huu wa kitandawazi. Faida zilizopo za kujua lugha ya kigeni ni pamoja na
1. Biashara, unapokuwa na uelewa wa lugha Fulani ya kigeni kwamfano kichina, itakusaidia katika mawasiliano ya kibiashara na kufanya biashara yako na mzungumzaji wa lugha hiyo ya kigeni kwenda sawa. Hivyo tunaweza kusema kuwa kufahamu lugha yakigeni Kuna faida kubwa kiuchumi.
2. Elimu, kwa nchi za kiafrika asilimia kubwa hutolea elimu kwa kutumia lugha za kigeni katika ngazi mbalimbali za kielimu. Hivyo kufahamu kwako kingereza kutakusaidia kuwa na uelewa wa unayofundishwa. Aidha yapo maarifa mbalimbali yaliyo katika lugha za kigeni Kama vile kichina, kijerumani na kigiriki, katika vitabu na mitandao mbalimbali, hivyo kufahamu kwako lugha hiyo ya kigeni kutakusaidia kuyapata maarifa hayo. Pamoja na faida hizo na nyingine lukuki kami vile kupata fursa za udhamini wa masomo miongoni mwa fursa nyinginezo. Unaweza kusikiliza fursa nyinginezo kwa kusikiliza makala ya DW kiswahili (2018) katika kiungo hiki >Umuhimu wa kujifunza lugha za kigeni | DW | 19.04.2018
KOSA LINALOFANYWA KATIKA UFUNZAJI WA LUGHA YA KIGENI HAPA TANZANIA
Lipo kosa kubwa linalofanywa katika ufunzaji wa lugha ya kigeni hasa ufundishaji wa lugha ya kingereza, na kusabaisha watu wengi kutoifahamu lugha hii bali kuwa na misamiati kadhaa ya kingereza, na ndiposa ukiwasikiliza watanzania wengi wajiongea lugha ya kingereza huongea kingereza Cha kitabuni. Hii hutokana na ukweli kuwa kingereza hufundishwa kama somo badala ya kufundisha kama kozi ya lugha ya kigeni, Yani kuzingatia stadi na taratibu zote za ufunzaji wa lugha ya pili.
ZIFUATAZO NI MBINU ZITAKAZO RAHISISHA UFUNDISHAJI NA UFAHAMU WA LUGHA YA KIGENI,
Kwanza, Lugha za kigeni Kama vile kingereza zifundishiwe kwa watanzania kama kozi ya lugha ya kigeni na sii kama somo la kawaida kama ilivyo sasa, Zipo taratibu na kanuni za ufundishaji wa lugha ya pili au ya kigeni ambazo zisipozingatiwa Jambo la ujifunzaji wa lugha ya kigeni hukwama. Mambo hayo ni pamoja na kuzingatia viwango vya wajifunzaji wa lugha husika, malengo, pamoja na kuzingatia ufundishaji wa stadi nne za lugha ambazo ni kusikiliza kuzungumza, kusoma na kuandika, miongoni mwa taratibu nyingine. Mambo haya hayazingatiwi kwakuwa hata wafunzaji hawana weledi na maarifa ya kufunza lugha ya kigeni. Hivyo ni muhimu mitaala ya elimu ikafanyiwa marekebisho, pia waalimu wa lugha za kigeni Kama vile kingereza wakapatiwa mafunzo ya namna ya kufunza lugha ya kigeni.
Pili, Lugha za kigeni k
ama vile kingereza zifunziwe kwa mkabala wa kimawasiliano, Ufundishaji wa lugha kimawasiliano huzingatia kuwa lengo kuu la kujifunza lugha ni mawasiliano. Aidha wafunzaji waache kufunza sarufi na kuikaririsha kwa wanafunzi bila kujali mawasiliano. Vile vile mazoezi mbalimbali yanayotolewa kupima uelewaji yazingatie kuchochea utendaji kwa mjifunzaji. Pia wanafunzi au wajifunzaji walugha wanaweza kupelekwa katika mazingira husika kulingana na mada ya siku hiyo, kwamfano mfunzaji huweza kuwapeleka wajifunzaji sokoni kufanya manunuzi kwa lugha husika wajifunzayo. Mazingira halisi huboresha kumbukumbu kwa kile walichojifunza.
Tatu, Matumizi ya media mbalimbali katika kufunzia lugha, matumizi ya media kama vile video, picha, magazeti na media nyinginezo za kisasa husaidia kurahisisha katika kujifunza lugha ya kigeni. Tafiti mbalimbali zilizofanywa kuhusu ujifunzaji wa lugha ya pili au ya kigeni zikionesha matokeo chanya pale ambapo mfunzaji wa lugha alitumia media mbalimbali katika kufundishia lugha. Hii ni kutokana na ukweli kuwa matumizi ya media katika kufundishia lugha huchochea uelewaji wa haraka wa lugha kwani huhusisaha milango mingi ya fahamu ya mjifunzaji wa lugha ya pili au ya kigeni.
Nne, Matumizi ya motisha, Mjifunzaji wa lugha yeyote wa kigeni nikama mtoto mdogo hivyo huhitaji motisha Kama vile mazingira mazuri ya kujifunzia pamoja na zawadi nyingine ndogo ndogo kama vile kupongezwa pale anapofanya vizuri na kutiwa moyo pale anapofanya vibaya. Hivi vinapokosekana katika kujifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili huenda ugumu ukajitokeza kwani mfundishaji atakuwa anafundisha darasa lisilochangamka vilevile utoaji wa motisha kwa wajifunzaji huwafanya wapende kujifunza na kupenda somo kwa ujumla.
Tano, Darasa moja halitakiwi kuwa na wanafunzi wengi. Kuwa na wanafunzi wengi katika darasa la wajifunzaji lugha ya kigeni ni kikwazo kikubwa cha kuzuia wanafunzi wasiielewe lugha husika, kwani wanafunzi au wajifunzaji lugha huwa na uwezo tofauti wa uelewa, kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi humsaidia mfunzaji kumfikia kila mjifunzaji na kumsaidia pale apatapo changamoto. Ili kuwezesha hili ni kuwekeza katika elimu, ambapo madarasa ya kutosha yatajengwa pamoja na kuzalisha wataalamu wakutosha wakufundisha lugha za kigeni Kama vile kingereza na kichina.
Sita, Wakufunzi walugha ya lugha za kigeni wapewe mafunzo maalumu yakufindisha lugha ya pili Kama vile kingereza, Hii itasaidia kwa wele wafundishaji kuwa na stadi na maarifa Muhimu katika kufundisha lugha. Aidha vitabu vya kufundisha lugha vitungwe kwa kuzingatia ubora, taratibu na kanuni za kufundishia lugha za kigeni.
Zaidi ya yote, ikiwa hayo yatazingatiwa yataweza kuchochea ufahamu wa lugha za kigeni kwa Watanzania na hata ikiwa kingereza hakitatumika kutolea elimu kwa masomo mengine bado watanzania wataimudu lugha hii kuliko ilivyo sasa. Nakuweza kupata fursa zile zitokanazo na ujuzi wa lugha ya pili au ya kigeni
Upvote
68