Mbio kuelekea 2025 machozi jasho na damu

Mbio kuelekea 2025 machozi jasho na damu

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Wakuu kumekua hali ya kawaida katika Nchi zote Duniani inapokaribia mwaka wa uchaguzi huwa na fukuto na joto la vyama na Wanasiasa kujiandaa kwajili ya uchaguzi husika hii tumekua tukisikia kila Kona ya Dunia Watu kushutumiana, kuchafuana, kuwekeana vikwazo na wakati mwingine hata kudhuriana ilimradi tu kuhakikisha kuwa anaweka Mambo sawa na njia inaliwa nyeupe kupata madaraka.

Uzi huu ni maalumu kwajili ya kuangazia matukio mbalimbali yanayotokea ikikaribia kipindi cha uchaguzi Mkuu hapa nitaanza kuorodhesha matukio mbalimbali niyakumbukayo yaliyojiri,nayaojiri yatakayojiri katika Nchi yetu kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za mitaa 2024 na ule wa 2025.
 
Kama unakusudia kuwatukana wanasiasa Kwa lugha za mafumbo nadhani haisaidii,ukitaka fungua code watu waporomoshe matusi Kwa wafu.
 
Kuna waziri mkuu mstaafu aliitwa nyampara anayeutaka urais huku akiwa na mashamba makubwa ya mahindi, waziri mkuu mwingine mstaafu naye alionjeshwa chungu na makada wenzake kuwa aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha masultan. Yupo pia waziri mkuu mwingine mstaafu yeye alichafuliwa mapema sana asiiufikie urais hata robo kwenye hatua za mtoano akiishia raundi ya kwanza akashupaza shingo kuutaka urais akaishia kuitwa fisadi mkubwa. Kuna waziri mkuu mstaafu mwingine yeye aliishia kutungiwa kitabu cha uongozi akakosa sifa ya kuteuliwa kugombea urais. Ni waziri mkuu mmoja tu ambaye hakuchafuliwa katika kuutaka urais ila hakuupata. Majimboni ni vituko na vitimbi ni vingi wanachafuana mpaka mpaka maisha binafsi kama elimu na mahusiano ya kimapenzi. Madiwani nao hawako nyuma kule mpaka michepuko na kupakua mizinga ya watu inatajwa. Serikali za mitaa nako mwendo ni uleule ndani na nje ya chama ni kurushia matope, ushuzi ili mradi tu mgombea achafuke na anuke. Hizi zote zinaitwa siasa za maji taka, kuchafuana kisiasa
 
Lukuvi walimtoa mapemaa, Sasa bado kipara na Madelu.
 
Back
Top Bottom