Mbio za CHADEMA 334 (CHADEMA Marathon 334)Shiriki sasa! Hujachelewa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
CHADEMA Marathon 334 ninini?

CHADEMA Marathon 334 ni kampeni maalum ya kuchangisha fedha iliyozinduliwa na chama kikuu cha upinzani nchini Tanganyika.

Lengo kuu la kampeni hii ni kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 334 za Kitanzania ili kufanikisha shughuli mbalimbali za chama.

Fedha zitakazopatikana kwenye kampeni hii zitatumika kugharamia na kuandaa mkutano mkuu ujao wa chama unaojulikana kama Baraza Kuu la Umma.

Mkutano huu muhimu umepangwa kufanyika tarehe 15 Septemba 2026.

Ndani ya wiki ya kwanza tu tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii mnamo Julai 2026, chama kilifanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni 81 kutoka kwa wanachama, wapenzi, na wananchi kwa ujumla.

Kwa wadau na wafuasi wanaotaka kuchangia kampeni hii ya ukusanyaji wa fedha, chama kimetoa njia rasmi na salama za malipo.

Unaweza kutuma mchango wako kupitia M-Pesa kwenda namba 0744446969 (Jina la Akaunti: CHADEMA HQ) au kupitia Benki ya NMB kwa namba ya akaunti 22606600140 (Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo).

Kuwa sehemu ya mabadiliko.. Changia sasa🔥

Updates:

Mpaka leo, Julai 20, 2026 - tayari 145M🔥🔥🔥

Nimechangia mara mbili, kupitia bank na mpesa,nadhani jf members tuchangie, shilingi 100 waweza Iona ni ndogo lakini ni kubwa sana,hebu tujitoe kwa chochote
kwanini uchangia mara mbili gentleman?

kwani chama chenu kina wanachama wangapi hata ishindikane kuchangia elf moja tu miongoni mwenu kwa siku moja? kila moja wenu kwa siku moja tu?
 
Gentleman,
changamoto ni nini hasa hata kiasia hicho kidogo tu cha pesa kushindwa kuchangwa ndani ya siku moja?

ina maana wanachadema hawajui mpaka sasa juu ya mchango huo hata ionekane nguvu kubwa kiasia hiki ikitumika kuwalazimisha wachangie?
 
W

Ewe mkata viuno propaganda zenu zimebuma CHADEMA HIYOOOOOO INASONGA MPAKA INAKERAAAAAAAAAAA
 
why maneno maneno tu mitandaoni na vitendo ni zero? changamoto ni nini?
 
Gentleman,
changamoto ni nini hasa hata kiasia hicho kidogo tu cha pesa kushindwa kuchangwa ndani ya siku moja?

ina maana wanachadema hawajui mpaka sasa juu ya mchango huo hata ionekane nguvu kubwa kiasia hiki ikitumika kuwalazimisha wachangie?
Kulazimishana kuichangia issue za ndani ya chama zipo kwenu ccm, Hadi KUELEKEA kuswekwa ndani kisa hamjachangia chama chenu
 
Mkuu Asante kwa Uzi huu wa hamasa, ila ulipaswa kuwa na taarifa hadi ya leo kwenye huu Uzi wako. Hadi kufikia leo, update ya lisaa limoja lililopota, cdm wamefikisha shilingi 144.3m. Najivunja kuwa sehemu ya waliichanga hadi sasa. J3 au j4 naongeza mzigo tena.
 
Sahihi kabisa mkuu nimeongeza kipengele cha updates
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…