Mbivu mbichi Vita vya Ukraine; Je, Urusi akishinda dunia itakuwa kwenye hali gani?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,344
Reaction score
12,472
Habarini za muda huu,
Kumekuwa na Vita nchini Ukraine ambapo majeshi ya Ukraine yanalinda nchi Yao dhidi ya uvamizi wa Rassia katika nchi Yao.

Dhamira ya nje ya Ukraine ni kujilinda dhidi ya uonevu wa Rassia.

Dhamira ya nje ya Rassia ni kuwalinda wa Ukraine wanaonewa na serikali yao wenyewe pia kulinda maslahi Yao ya kiulinzi dhidi ya madola makubwa ya Magharibi ikiwemo USA.

Sabubu zingine zikitajwa ikiwemo uwepo wa Bomba la Nord stream II ambalo limekuwa haliifurahishi marekani na Uingereza.

Tufahamu
Hivi Vita bado vipo kwenye phase ya pili endapo vikikomaa na kufika phase zingine ambapo tutashuhudia uwepo wa majeshi ya kigeni ya kiisaidia Ukraine na labda madola mengine yakaisaidia Rassia ni wazi itakuwa ni Vita vya tatu vya dunia.Vita vya 3 vya dunia sio kitu kirahisi na sio kitu Cha kutamani kukishuhudia hasa kwa uwepo wa masilaha ya nyukilia kila pembe ya dunia.

Endapo vitatokea Vita vya tatu vya dunia na Rassia na washirika wake wakashinda Western block (NATO) ni lazima kutakuwa na mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji dunia na labda wengi wa waTanzania wangependa US ianguke Ila hawajui athari za US kuanguka ghafla hasa kutokana na Vita.

Naomba nije na baadhi ya athari za dunia kutoakana na Kubadilika kwa Super power national

Siasa
Mfumo wa siasa katika nchi nyingi za dunia ya 2 na 3 utabadilika Sana na pengine tutashuhudia madikteta wakiongezeka kwa Kasi , uwepo wa mapinduzi mengi ya kijeshi katika nchi hizo kunakotokana na kukosekana kwa udhibiti wa mifumo ya upatikanaji uongozi.

Hili linatokana na ukweli kuwa mfumo wa demokrasia na pengine mfumo wa upatikanaji uongozi unaratibiwa na marekani na washirika wake hasa ufaransa na Uk kupitia Common wealth na Francophone hivyo kuanguka kwa NATO kutasababisha kuzorota kwa taasisi hizo hivyo viongozi wengi,nchi nyingi na makundi mengi yataona ndio wakati wakujinasua kwenye makucha ya dhuluma.

Pia Rassia atataka kuja na mfumo wake na kujaribu kuweka alama zake ili awatambue waliofika "Qualifications" za kuwa washirika wake

Siasa za kikanda
Duniani Kuna Kanda kadhaa ,lakini hapa ningependa kutoa maoni yangu juu ya siasa za Kanda Kama 5 hiivi zitakavyokuwa endapo US ataanguka

Ulaya
Kitendo tu chakutokea Vita vya 3 vya dunia vikihusisha Rassia ni kitu ambacho umoja wa ulaya hukitaki na sababu kubwa ni kuwa athari atakazopata Rassia ni sawa na watakazopata wao.

Ukanda huu sio rahisi kuona ongezeko la madikteta ama mapinduzi lakini tutashuhudia vyama vikongwe Kama CdU , Labour etc vikikosa mvuto na kuibuka makundi mapya ya wahafidhina amayo yatakuwa tayari kuwekeza zaidi jeshini zaidi ya miundo mwingine ya uchumi.

Umoja wa ulaya utavunjika na badala yake wataunda chombo kipya.

America na Carrebian Islands
Ukanda huu tutashuhudia mengi
1.kudharaulika kwa US
2.Ubabe wa Cuba, Ecuador ,Bolivia na Venezuela
3.Kukua kwa ujamaa
4.Ongezeko la madawa ya kulevya
5.Mapinduzi na udikteta

3.Kanda ya Afrika
Hapa Kuna shida toka mwanzo Ila tutarajie yafuatayo
1.kufa kwa makundi ya kigaidi Alshabab,Bokhoharam etc
2.Kukoma kwa vurugu Nigeria,DRC na Libya
3.mapinduzi, udikteta na mabadiliko ya lazima kiuongozi
4.vyama vikongwe vya kisiasa kugeuka kuwa makundi ya uasi eg ANC,FDDSDD ,Ccm etc
5.kubadilika kwa mfumo wa maisha kabisa ya wananchi.
6 .Kuundwa kwa African Army

4.Kanda ya Asia ya mbali na pasifiki
1,Tarajia madikteta wengi
2,kuanguka kwa madola makubwa ya Korea kusini, Japan nazinginezo
3.Vurugu na ukimbizi mwingi
4.Vita visivyoisha vikihusisha China
5.kukua kwa biashara ya "human trafficking"

5.Kanda ya Mashariki ya Kati
Kanda hii ni muhimu Sana duniani kwakuwa kwanza ndio chimboko la ustaarabu hasa dini pendwa na pia uzalishaji wa nishati
1.Kuanguka kwa dola za Kuwait, Bahrain, Saudi Arabia na E.A.U
2.Kukua kwa dola za Israel na Qatar
3.Migogoro ya Afughanstan na pia Palestine itabaki vile vile
4.Hofu ya ugaidi itapungua
5.Ongezeko la madikteta
6. Hali ya sirya itatengemaa
7.Wakurd watatawanywa kabisa
8.Turkey itagawanywa vipande viwili

Asanteni kwa leo
 
Asante sana
 
Mawazo yako tu mkuu,ila hakuna kitu kama hicho.

U.s.a ni mjanja sana,ataishambulia Ile Russia kwa dk chache na atakuwa ameingamiza.

Ni mjanja na anajua na ana akili kuliko mawazo yako
 
Ukiangalia kwa ndani zaidi nilivyoandika sio kwamba natarajia but nimewaza tu endapo itatokea US akaanguka ghafla itakuwa ni sawa na kumuondoa paka penye panya wengi
 
Hakuna cha Vita ya Tatu wala ya Saba,
Wanapasha tu Mitambo yao baadae wafunge zipu Maisha yaendelee,

Usiwaze sana, kula mlo kamili, fanya mazoezi, pumzika kwa wakati.
 
"Wanapashana tu Kitambo Yao baadae wafunge zipu maisha yaendelee"
 
Mkuu ningependa kujua ...wewe unasimama na upande gani?
Russia au Ukraine?
Neutral kwasababu
1.kama mkisto Safi nisingependa kuona damu za watu zikimwagika hovyo
2.Ni athari za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na Vita zitakuwa kubwa Sana
3. Mimi ukiachana na Simba sc ,Mimi sishabikiagi vitu vingine vyote huwa natazama tuu

Japo najua Rassia atampiga Ukraine Ila yeye atapigwa kwa fimbo ya mbali ya USA (kiuchumi)
 
Back
Top Bottom