Wacha niwe mchambuzi ma maswala ya Kisiasa Kwa Dakika Moja
Hakuna Shaka yoyote kwamba kuondoka kwa Mzee Edward Lowasa Kule Upinzani(chadema) na kuelekea Kule CCM kumeitingisha Chadema na kuiacha Mahututi, hata hivyo Ikumbukwe kwamba Mh. Lowasa Kule upinzani alifuata Uraisi,na kwa mtu yeyote mwenye utashi walau kidogo tu hapaswi kushangazwa na uamuzi WA kurudi.
Hata kwenye Maisha ya kawaida mtu anapoenda nchi ya mbali kutafuta ufanisi kimaisha anapokosa au umri wake umesonga Sana hatimaye huamua kurudi nyumbani alikozaliwa ili aishi na watu WA karibu na hatimaye kufa kifo tulivu katika ardhi ya nyumbani. Ndivyo ilivyotukia kwa Lowasa, ametumia utashi wake kutambua Hali zinavyoenda,kesho ya familia yake,uzee wake, kupoteza marafiki wa karibu,kutendewa kwa hila na wapinzani wake WA Kisiasa, na pia ushawishi WA viongozi wakuu WA CCM.Na kufanya uamuzi WA kurudi ambao Nazani haukuwa mgumu Sana kwake ukilinganishwa na ule WA kukihama chama chake CCM mwaka WA 2015,na Kama umekuwa ukifuatilia nyendo zake utang'amua kwamba Mzee alikuwa makini Sana kuhusu Kauli zake,kuvaa mavazi ya chama(chadema), Kufanya uwana harakati, uamuzi wa familia yake kwa kijana wake kutogombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema Kule jimboni kwake Licha ya kudaiwa kwamba wananchi walimsihi agombee, Mikutano yake kadhaa na mwenyekiti WA CCM.
Tukirudi kwa Hawa CCM,kwa ufahamu wangu WA Hali zilivyokuwa mwaka 2015,kupatikana kwa mgombea wao kulikuwa busara za wazee kunusuru chama kwa kuepusha mpasuko mkubwa ambao hata hivyo ulitokea kwa kadiri Fulani, baada ya Lowasa kukihama chama chake ili kutafuta nafasi nyingine ya kutimiza ndoto yake maishani na ya muda mrefu ya kuwa Rais.
Licha ya kwamba Lowasa ameshapoteza mwelekeo,Heshima kubwa aliyokuwa nayo ndani ya CCM na Chadema Ikumbukwe pia hata ndani ya CCM huenda bado kuna wingu kubwa la watu wangali wanapaaza sauti mioyoni mwao wakisema "Tuna Imani naye(Lowasa)".Kwa hiyo huenda ukaonekana ushindi WA Kisiasa dhidi ya upinzani ila mpasuko ungali unaunguruma ndani ya chama hiyo machachari nchini Tanzania.
Hitimisho:
Usiweke moyo wako kwa mwanasiasa Fulani au mtu mwingine ili Siku akiondoka au kuanguka nawe unabaki Mahututi Kama ilivyo kwa upinzani nchini Tanzania.