Mbona ghafla matamko dhidi ya Heche yamekuwa mengi?

ufisadi ni dhambi ya fedheha sana gentleman ndio maana kila jamii inakemea hiyo nonsense kwa matamko 🐒
Mkata viuno kwenye kiwango Cha uboera Sana KILA tred inayohusu chadema mitako pwa pwa pwa hata aibu kiduchu huna nakustua CCM wamefisasi KILA kitu tupo hoi Kama nchi Ila maviongozi ya CCM yanaukwasi wa hataki.
 
Naona ghafla matamko dhidi ya John Heche makamu mwenyekiti wa chama kikubwa nchini, yamekuwa mengi.

Unajua ni kwa nini? Mtambo wa propaganda wa CCM umeishiwa mbinu za kuishambulia CHADEMA.

Alipokuwa Dr. Slaa ana nguvu walisema ni chama cha wakatoliki. Mbowe naye alipowashika pabaya wakasema ni chama cha wachaga.

Sasa ile propaganda ya uchaga na ukatoliki haiwezi kufanya kazi kwa Heche. Heche ni mkurya halafu ni msabato.

Sasa njia pekee ni kuonesha kuwa hata wazee wa kimila wa Tarime hawafurahishwi na Heche. Hii nchi si tulishakubaliana mambo ya ukabila yasiingizwe kwenye siasa zetu?

Inakuwaje wazee hao wa kimila wa Tarime watoe tamko dhidi ya Heche kama vile Heche anawakilisha kabila lao kwenye mambo ya siasa!

Aliyewaambia hao wazee wa Tarime kuwa Heche yupo CHADEMA kuwakilisna kabila na koo zao ni nani?

Wanachadema hawakumchagua Heche kwa kuwa ni mtu wa kutoka kwenye kabila ama koo zao. CHADEMA walimchagua Heche afanye hicho anachofanya ambacho wao wanakipinga.

Vijana wa Tarime waelimisheni wazee wenu kuwa wao wana mamlaka na Heche kama mtoto wao lakini si kama kiongozi wa chama cha siasa.

Mbona hawajataja hayo matusi wanayodai Heche anatukana. Halafu wanaposema anatukana viongozi wa kitaifa hawaoni kuwa pia yeye ni kiongozi wa kitaifa?

Sasa wao ujasiri wa kumkemea kiongozi wa kitaifa wameutoa wapi?
Waseme tu wamelishwa mlungula gani na nani?
 
Kuhusu wazee wa kikurya, ningewaelewa kama ingekuea miaka ya tisini ambako huko, kwa mtazamo wao anefanya kasa.

Kosa hilo ni kitendo cha kwenda mjini halafu hajajiubga ja Geshi,. Hana Buti. Hana kombati, hata V moja hana, hapo huyu mtoto wamzee Heche angefanya kosa.

Yaani unarudi nyumbani likizo baada ya miaka kadhaa huko mjini, na watu hawajyoni umevaa buti! Unaulizwa unasema; nafanya TENESCO, huna hat V, eti ubacheo cha supervisor, hapo hata mke hupati. Umeharibika.

Sasa tuwe makini. Awali nilidharau hii kitu na nikajizuia kuisemea,lakini inavyoebdelea, wajinga hawa wanaenda kufanikiwa kwenye suala la muda.

Hawa jamaa wanahitaji sana muda ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili,Chadema na hasa Heche ni kikwazo kwao kufikia malengo yao, kwa muda mchache (kumbuka Jumuiya ta Madola) wanaoutaka ili kurekebisha mambo..

Sasa, limeibuliwa hili, CDM na wafuasi wake wameondoka kwenye reli na kutumia nguvu na muda mwingi kujadili " sijui wizi, sijui ubadhirifu" tena wa vichenchi vya mboga na kuacha kumkimbiza mwizi aliyechoka tayari kwa mipini anayopigwa kutoka kwa wana nzengo.

Ukitaka kuthibitisha hili, hii sinema itakuwa na episode nyingi sana ambazo CDM wanazimeza na kuacha kumkimbiza mwizi.

Watu hawa wanatumia media zote na hasa za kwenye mtandao ili kusambaza propaganda hizi. Ukifuatilia hizi taarifa, ukamkumbuka yule bingwa wa ufafanuzi, utasema maneno yote lakini kubwa katika uandidhi huu hakuna weledi na hata maswali ambayo yangeulizwa na mhitimu wa darasa la saba B, angeyabaini

Kwa mfano, taarifa za 30 kurekodiwa na ikaelezwa itarushwa lini, kesho yake Jambo Tv, wanakuja na kitu hicho, kama ilivyoelezwa. Naamini wanapewa na bahasha yenye maelezo ya kurusha kama ilivyo bila kuhaririwa.

Kipengele cha muhimu cha WAPI katika habari ni msingi wa taarifa ili kufahamika huyu amezungumza haya hakiwekwi, utaambiwa tu akizungumza. Imeishia hapo.haielezwi alikuwa na press, anahutubia. Kwenye mjadala nk, hakuna.

Ukiona habari zote hizo, CDM haipewi nafasi kujibu, "habari" inakusanywa na kurushwa, inaachwa hivyo.

Kuna wale wana CDM, wanaofungiwa vichochoroni na waandishi wanaitwa kuchukua habari. Ajabu ya uandishi huu, eti hakuna mwandishi anayeliona hilo na hata kuchomeka ndani ya para tu kuwa" akiongea katika stoo ya mahindi, mwanachama huyo anayetaka uwazi amesema...

Sijui kama tunapiga hatua au vipi historia itatuhukumu. Kapuya alikuwa waziri, kafanya madudu, waandishi wakamfuata, akagawa bahasha za kaki, kesho yake magazeti yakaibuka na kuchwa cha habari, Waziri agawa bahasha za kaki. Hawa wa siku hizi wanashindwa wapi?.

Kituko,kingine cha udhalilishaji na kinachostaajabisha ni ile bodi ya Ithibati ya wanahabari, imepotea kwenye issue hii au haina meno tena? Kuna "habari" moja kusambazwa ikiwa vilevile kwa "VYOMBO VYA HABARI". Hii imetoka jana kuhusu nyumba inayodaiwa kuhengwa na Heche, Mambo haya tuliyaona uchaguzi w 2000 ambapo, wapambe walikuwa wakiandika story anatafutwa mwandishi anapewa mshiko, anaambiwa nenda kaweke jina lako. Habari inatoka hivyo kwenye magazeti yote, hata kama kulikuwa na kosa la uandishi, inakwenda hivyo.

Tusisahau pia kuna tunaweza kuwa tunachezeshwa na issue ya mafuta.
 
Naona ghafla matamko dhidi ya John Heche makamu mwenyekiti wa chama kikubwa nchini, yamekuwa mengi.

Unajua ni kwa nini? Mtambo wa propaganda wa CCM umeishiwa mbinu za kuishambulia CHADEMA.

Alipokuwa Dr. Slaa ana nguvu walisema ni chama cha wakatoliki. Mbowe naye alipowashika pabaya wakasema ni chama cha wachaga.

Sasa ile propaganda ya uchaga na ukatoliki haiwezi kufanya kazi kwa Heche. Heche ni mkurya halafu ni msabato.

Sasa njia pekee ni kuonesha kuwa hata wazee wa kimila wa Tarime hawafurahishwi na Heche. Hii nchi si tulishakubaliana mambo ya ukabila yasiingizwe kwenye siasa zetu?

Inakuwaje wazee hao wa kimila wa Tarime watoe tamko dhidi ya Heche kama vile Heche anawakilisha kabila lao kwenye mambo ya siasa!

Aliyewaambia hao wazee wa Tarime kuwa Heche yupo CHADEMA kuwakilisna kabila na koo zao ni nani?

Wanachadema hawakumchagua Heche kwa kuwa ni mtu wa kutoka kwenye kabila ama koo zao. CHADEMA walimchagua Heche afanye hicho anachofanya ambacho wao wanakipinga.

Vijana wa Tarime waelimisheni wazee wenu kuwa wao wana mamlaka na Heche kama mtoto wao lakini si kama kiongozi wa chama cha siasa.

Mbona hawajataja hayo matusi wanayodai Heche anatukana. Halafu wanaposema anatukana viongozi wa kitaifa hawaoni kuwa pia yeye ni kiongozi wa kitaifa?

Sasa wao ujasiri wa kumkemea kiongozi wa kitaifa wameutoa wapi?
Tunapoeleza kwamba, CCM hakuna watu smarts,wabunifu,wanusa habari,wenye marejeo chanya,wasoma alama za nyakati na wakweli huwa tunamaanisha.Huwa hawajipi homeworks na kuyafanyia majaribio maigizo yao kupima matokeo tarajiwa.A bunch of heathens!
 
Ukiona hivyo ujue ni suala la muda kabla ya wazee wa kindengereko nao hawajatoa tamko, baadaye wazee wa kizaramo, Wazee wa kihaya , wa kichaga na n.k GAME PLAN.
Kwa namna hiyo ina maana CCM ni vipofu wa maarifa mema na sayansi ya siasa za kimikakati yenye tija.Wanajaribu kila njia itakayowaijia vichwani mwao kwa mwendo wa kukisia matokeo.Kwa ufupi,hawajiwezi katika mbongo zao.Dhoofu kabisa!
 
Naona ghafla matamko dhidi ya John Heche makamu mwenyekiti wa chama kikubwa nchini, yamekuwa mengi.

Unajua ni kwa nini? Mtambo wa propaganda wa CCM umeishiwa mbinu za kuishambulia CHADEMA.

Alipokuwa Dr. Slaa ana nguvu walisema ni chama cha wakatoliki. Mbowe naye alipowashika pabaya wakasema ni chama cha wachaga.

Sasa ile propaganda ya uchaga na ukatoliki haiwezi kufanya kazi kwa Heche. Heche ni mkurya halafu ni msabato.

Sasa njia pekee ni kuonesha kuwa hata wazee wa kimila wa Tarime hawafurahishwi na Heche. Hii nchi si tulishakubaliana mambo ya ukabila yasiingizwe kwenye siasa zetu?

Inakuwaje wazee hao wa kimila wa Tarime watoe tamko dhidi ya Heche kama vile Heche anawakilisha kabila lao kwenye mambo ya siasa!

Aliyewaambia hao wazee wa Tarime kuwa Heche yupo CHADEMA kuwakilisna kabila na koo zao ni nani?

Wanachadema hawakumchagua Heche kwa kuwa ni mtu wa kutoka kwenye kabila ama koo zao. CHADEMA walimchagua Heche afanye hicho anachofanya ambacho wao wanakipinga.

Vijana wa Tarime waelimisheni wazee wenu kuwa wao wana mamlaka na Heche kama mtoto wao lakini si kama kiongozi wa chama cha siasa.

Mbona hawajataja hayo matusi wanayodai Heche anatukana. Halafu wanaposema anatukana viongozi wa kitaifa hawaoni kuwa pia yeye ni kiongozi wa kitaifa?

Sasa wao ujasiri wa kumkemea kiongozi wa kitaifa wameutoa wapi?
Kumbe Wasabato siku hizi wanakunywa Konyagi?
 
Nina wasi wasi pia Gen Z wa kikurya wanaweza kwenda kuwasalimia hawa madingi wanoko wa kikurya😀
Hao wazee wakimila wanadhani tamko la kimila la Wakurya linawahusu pia na wandengereko wanaomuunga mkono Heche?
 
Back
Top Bottom