Mbona ghafla matamko dhidi ya Heche yamekuwa mengi?

Mbona ghafla matamko dhidi ya Heche yamekuwa mengi?

Hata kama Heche kazipiga kweli mbona Mwamba alipozipiga hatukusikia hizi kelele zote?

CDM ishapata hadi hati za ukaguzi zenye mashaka kutoka kwa CAG na hatukuwasikia hawa watu!

Sasa hivi ndiyo wana uchungu sana na pesa za chama?

Huu ni mradi tu unasukwa na muda si mrefu lengo lake litakuwa wazi C& P.
 
Mmeelewa sasa kwanini mikutano ilizuiliwa?

Laiti mikutano ingekuwa inaendelea Heche anatandika bakora jukwaani majambazi ya CCM hivyo vipress uchwara wala usingevisikia maana watu wangekua busy kusikiliza kwenye rally Heche kaongea nini.

Ila bado naona hii project kama ya wakatoliki wale wa kuchaji haina maisha marefu maana inaratibiwa na mazezeta.
 
Kuna clip inazunguka ya Sheikh mmoja akimshawishi BAWACHA wa kanda ya kati . Huu ni ushahidi mzuri tu kuwa watu wanalipwa. Ukitaka kujua ni kwanini , jiulize kwanini hakuna anayekuja na ushahidi hata mmoja!
Wote wanatoa tuhuma hatujaona ushahidi

Katibu mkuu kasema yeye ndiye anatunza kwa maana ya kupokea na kuidhinisha matumizi. Hakuna anayemuuliza bali wanamwandama Heche

Siri ni kwamba wakati wa ''Maridhiano ya CCM na Mbowe'' , Heche na Lissu walikuwa mwiba mkali. Hawakukubali mambo yaende tu. Hilo likawaudhi sana CCM

Kwasasa wanataka kumuondoa waweke kibaraka wapige picha za kupeleka commonwealth na kwenye balozi waseme kuna maridhiano.

Wakiulizwa maridhiano ni kuhusu nini na kati ya nani na nani hawana jina

Jiulize kwanini CCM ndio wanakewrwa '' na ufisadi'' wa CHADEMA na si ufisadi ule wa Dodoma wa watu kujiteua?
kwanini hawakemei pesa za uniform za Polisi katika mabilioni!
Kwanini hawaulizi Bilioni 70 zilizopelekwa Mwanza zilikuwa za nani na nini
Kwanini hawakerwi na pesa alizosema SSH kwamba zimepelekwa China
Kwanini hawakerwi na pesa za bargaining tusizojua hadi leo
Kwanini hawakerwi na mikataba
Kwanini hawana uchungu na Trilioni 1 ya kunywa chai na mikate Ofisini
Kwanini hawakerwi na viongozi wa Umma kumiliki magari ya Milioni 600
 
Naona ghafla matamko dhidi ya John Heche makamu mwenyekiti wa chama kikubwa nchini, yamekuwa mengi.

Unajua ni kwa nini? Mtambo wa propaganda wa CCM umeishiwa mbinu za kuishambulia CHADEMA.

Alipokuwa Dr. Slaa ana nguvu walisema ni chama cha wakatoliki. Mbowe naye alipowashika pabaya wakasema ni chama cha wachaga.

Sasa ile propaganda ya uchaga na ukatoliki haiwezi kufanya kazi kwa Heche. Heche ni mkurya halafu ni msabato.

Sasa njia pekee ni kuonesha kuwa hata wazee wa kimila wa Tarime hawafurahishwi na Heche. Hii nchi si tulishakubaliana mambo ya ukabila yasiingizwe kwenye siasa zetu?

Inakuwaje wazee hao wa kimila wa Tarime watoe tamko dhidi ya Heche kama vile Heche anawakilisha kabila lao kwenye mambo ya siasa!

Aliyewaambia hao wazee wa Tarime kuwa Heche yupo CHADEMA kuwakilisna kabila na koo zao ni nani?

Wanachadema hawakumchagua Heche kwa kuwa ni mtu wa kutoka kwenye kabila ama koo zao. CHADEMA walimchagua Heche afanye hicho anachofanya ambacho wao wanakipinga.

Vijana wa Tarime waelimisheni wazee wenu kuwa wao wana mamlaka na Heche kama mtoto wao lakini si kama kiongozi wa chama cha siasa.

Mbona hawajataja hayo matusi wanayodai Heche anatukana. Halafu wanaposema anatukana viongozi wa kitaifa hawaoni kuwa pia yeye ni kiongozi wa kitaifa?

Sasa wao ujasiri wa kumkemea kiongozi wa kitaifa wameutoa wapi?
Ukiona hivyo juu huo mpango ni uratibu wa mtu au kikundi fulani,haiwekani wote wasome script moja halafu ni kama wanaokotwa tu majalalni na kuvalishwa fulana, mboga mboga ni wahuni na wanamhofia Heche, wangekuwa wa maana wangehoji mabilioni waliyochangiwa na mabwenyenye siku ile je wanajua hayo mabilioni yalikoenda ?hata TRA walifyata sikuoni wakidai asilimia yoyote.
 
Wazee wa kimila wanahitaji kutahiriwa ufahamu wao wakifa kabla ya kuzikwa vijinga vya moto vinawahusu mikunduni mwao ili wengine wajifunze kuacha unafiki, uzandiki, uchawa, fitina na uchonganishi.
 
Endeleeni kujitekenya na kujichekesha Mwenyewe kama zuzu
Ukiandika sentensi usichanganye wingi na Umoja kwenye sentensi moja maana unaiparaganyisha.

Ulipoandika " Endeleeni kujitekenya" halafu tena ukaandika "na kujichekesha mwenyewe..." Hapo sentensi yako haina muwala.

Hapo Lumumba hamjui kiswahili vizuri?
 
Ukiandika sentensi usichanganye wingi na Umoja kwenye sentensi moja maana unaiparaganyisha.

Ulipoandika " Endeleeni kujitekenya" halafu tena ukaandika "na kujichekesha mwenyewe..." Hapo sentensi yako haina muwala.

Hapo Lumumba hamjui kiswahili vizuri?
CHADEMA kwa sasa mmepoteza Dira na muelekeo kabisa
 
Hata hili nalo litashindwa tu, Watz waleo sio wale wa 70s elimu ipo ya kutosha.
 
Yaani hiyo hela ndio unaona nyingi?
Hiyo ndio maana yana TONE TONE wewe chawa wa buku 7!

Ulifikiri hilo ni bomba la mamiliioni ya wakwepa kodi na narco cartels?
Yaani mnazidiwa ushawishi hadi na Upendo Nkone Ambaye pesa yake ilipatikana kwa muda mfupi
Umehamia kwa Upendo Nkone tena?

Kesho utasema hizo pesa mumeo anakusanya kwa muda mfupi.

Wewe si ndio ulisema CHADEMA haina ushawishi haiwezi kuchangiwa hata senti!

Pole kidampa wa buku 7 nayaelewa maumivu unayoyapitia kwa kuona unachotamani hakiwi, simamia misimamo yako usiyumbe !
 
Back
Top Bottom