Mbona hayati mzee Kawawa na Dkt Omari wamesahaulika kabisa

Mbona hayati mzee Kawawa na Dkt Omari wamesahaulika kabisa

Tufanye kesho jumatatu tuwakumbuke wote tena iwe mapumziko na jumanne!
 
Kiongozi mkuu wa Jamhuri huwa ni Rais. Nyerere alijiuzulu na kumuachia Kawawa. Yeye akachukuwa Urais.
 
Wazo zuri pia au itengwe siku 1 yakuwakumbuka wote kama marekani wanavyofanya
hilo nalo ni wazo zuri kwani inaweza kuunganishwa kwa kumbukizi ya muasisi iwe inabeba wote...
 
Tanganyika ilipokuwa Jamuhuri waziri wake mkuu alikuwa JK Nyerere
Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru alikuwa J. K. Nyerere

Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika ni J. K. Nyerere

Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika ni R. M. Kawawa

Kabla ya kuundwa kwa Jamhuri ya Tanganyika, Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu akamwachia Kawawa, alirejea kama Rais baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri mnamo mwaka 1962.
 
Iko hivi

Watu wa Kaskazini hususan Wakristo huwa wana Desturi ya kuwakumbuka Wazee wao waliofanya mambo makubwa yaliyogusa maisha yao

Usishangae hata wazee wa kule walio hai huwa wanafanya mpaka Aniversary ya ndoa zao na wanakaribisha wageni wengi tu na chakula cha kutosha kinapikwa sembuse Mtu mkubwa kama Sokoine ambaye nusura awe Rais wa nchi hii?

Na hayo yote wanaofanya ni NDUGU na JAMAA na wanaalika wageni

Suala la Dr. Omary Ally Juma na Rashid Mfaume Kawawa kama hawakumbukwi waulize ndugu zake walio hai
 
Hatuna haja ya kukumbuka wafu,tunakabiliwa na mengi. hata hao uliowataja wanakumbukwa ni suala muda nao watasahaulika.
 
Iko hivi

Watu wa Kaskazini hususan Wakristo huwa wana Desturi ya kuwakumbuka Wazee wao waliofanya mambo makubwa yaliyogusa maisha yao

Usishangae hata wazee wa kule walio hai huwa wanafanya mpaka Aniversary ya ndoa zao na wanakaribisha wageni wengi tu na chakula cha kutosha kinapikwa sembuse Mtu mkubwa kama Sokoine ambaye nusura awe Rais wa nchi hii?

Na hayo yote wanaofanya ni NDUGU na JAMAA na wanaalika wageni

Suala la Dr. Omary Ally Juma na Rashid Mfaume Kawawa kama hawakumbukwi waulize ndugu zake walio hai
Kwani kumbu kumbu ya Nyerere huwa inaandaliwa na serikali au familia?
 
Back
Top Bottom