Mbona hizi dini zinachanganya?

Kwa nini?
Kiranga hauamini uwepo wa Mungu hata nikikujibu "Kwa nini" Papa Francis alimjibu hivyo,bado utabisha,na mimi huwa sipendelei kubishana,halafu sijui kubishana,mimi majibu yangu huwa ni "Yes" au "No" halafu naweka nukta.

Hapo Papa Francis ni kama alikuwa ana muambia huyo binti asimlilie Yesu bali binti ajililie nafsi yake.Kuelewa hili inahitajika hekima au akili ya hali ya juu kama ambavyo kuelewa Luka 23:27 ina mhitaji mtu kuwa philosopher ili aelewe.

Luka 23:27 Yesu akawageukia akasema,Enyi binti za Yerusalemu(zinaweza kuwa binti za mahali popote,binti za Bukoba,binti za Geita,binti za Mwanza,binti za Dar es Salaam n.k),msinililie mimi ( Yesu anasema wasimlilie yeye maana anajua anaenda kutimiza mission yake aliyotumwa na Mungu kuja kumkomboa mwanadamu) , bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Binti ajililie nafsi yake ili na yeye siku moja aweze kutimiza mission ya roho yake aliyopewa na Mungu kuja kuikamilisha duniani,awe mtakatifu.
 
Sijawahi kutumia internet ya bando mkuu. Labda nikija likizo Tanzania ambako nako nina option ya mitandao ya Kimarekani.

Mimi natumia unlimited internet. Halafu nina unlimited internet nyingine ya WiFi.

Bando hata mnavyoweka sijui.
Dah! Mungu amekujaalia sana
 
Exactly 💯
 
Km ndivyo, basi watu wasingekuwa wanaenda hospitali au kutumia dawa. Na walioacha kwenda hospitali kwa kigezo cha Imani yao wamekufa.

"Zakuambiwa changanya na zako". Jk's voice.
 
Unahubiri dini wakati mimi natafuta jibu la kimantiki, hatuwezi kuelewana.

Papa hakujibu swali, alipiga danadana za kisiasa ya dini.

Ambazo na wewe unaendeleza hapa.

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya?

Hakuna aliyejibu swali hili.

Epicurus aliyezaliwa miaka 341 kabla ya Yesu aliuliza hili swali siku hizo. Mpaka leo halijajibiwa.

Na hata Papa mwenyewe kakubali hana majibu ya swali hili.

Kwa sababu si mtu ambaye halijui swali hili na ugumu wake.

Papa kasoma falsafa na theolojia. Anajua ugumu wa swali hili. Anajua halina jibu la kimantiki.

Ndiyo maana akabaki kuhubiri longolongo.

Binti analilia nafsi yake kwa kuulizia the problem of evil halafu wewe unamwambia aililie nafsi yake?

Aililie nafsi yake mara ngapi?
 
Dah! Mungu amekujaalia sana
Mungu hayupo mkuu.

Angekuwapo watu wasingeijua internet ya bando ikoje.

Kila mtu angekuwa anagonga unlimited ya kampuni ya simu na unlimited ya WiFi kama mimi tu.

Kama yupo, kwa nini anipendelee mimi nisiyemuamini halafu wanaomuamini wengine wawe wananuka umasikini hata bando wapate kwa manati na wengine wana viswaswadu vimepasukapasuka vioo ni hatari kwa afya zao lakini wanadunda navyo tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…