Mbona hizi dini zinachanganya?

Mbona hizi dini zinachanganya?

Kwa nini?
Kiranga hauamini uwepo wa Mungu hata nikikujibu "Kwa nini" Papa Francis alimjibu hivyo,bado utabisha,na mimi huwa sipendelei kubishana,halafu sijui kubishana,mimi majibu yangu huwa ni "Yes" au "No" halafu naweka nukta.

Hapo Papa Francis ni kama alikuwa ana muambia huyo binti asimlilie Yesu bali binti ajililie nafsi yake.Kuelewa hili inahitajika hekima au akili ya hali ya juu kama ambavyo kuelewa Luka 23:27 ina mhitaji mtu kuwa philosopher ili aelewe.

Luka 23:27 Yesu akawageukia akasema,Enyi binti za Yerusalemu(zinaweza kuwa binti za mahali popote,binti za Bukoba,binti za Geita,binti za Mwanza,binti za Dar es Salaam n.k),msinililie mimi ( Yesu anasema wasimlilie yeye maana anajua anaenda kutimiza mission yake aliyotumwa na Mungu kuja kumkomboa mwanadamu) , bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Binti ajililie nafsi yake ili na yeye siku moja aweze kutimiza mission ya roho yake aliyopewa na Mungu kuja kuikamilisha duniani,awe mtakatifu.
 
Sijawahi kutumia internet ya bando mkuu. Labda nikija likizo Tanzania ambako nako nina option ya mitandao ya Kimarekani.

Mimi natumia unlimited internet. Halafu nina unlimited internet nyingine ya WiFi.

Bando hata mnavyoweka sijui.
Dah! Mungu amekujaalia sana
 
jambo la kwanza ni kupigania UHAI WAKO KWA GHARAMA YOYOTE

jambo la pili kuipigania AFYA yako kwa namna yoyote ile

jambo la tatu kuliangaikia tumbo lako

hvyo ndivyo kila binadamua anatakiwa afany kila siku bila kujari kam utaenda peponi au motoni

ukidhulumu uhai wako(kujiua) ni dhambi na unaenda motoni

ukilifanyia ubahili tumbo lako na afya yako ni dhambi pia

wewe hapa duniani pambana tu iwe jua uwe mvua pambana mpk tone la mwisho

kufa utakufa tu huwezi kukimbia KIFO
ukitaka uishi maisha marefu yasiyo na shaka yaani uenjoy hapa duniani usiogope KIFO wewe yaogope matendo yako au yafurahie matendo yako hakika hautaofia kifo 7bu unajua una deni kwa muumba wako

enjoy kila dakika katika maisha yako Uumbaji haujirudii hakuna FELAKUTI mwingine na hatotokea tena hata wa kufanana nae pale NIGERIA imebaki LEGANCY yake kula maisha mwanangu
ila kumbuka SWALA NA KAZI mfungo kama hij wa ramadhani au kwa resima funga kujenga AFYA na kupuunguza dhambi
Exactly 💯
 
Km ndivyo, basi watu wasingekuwa wanaenda hospitali au kutumia dawa. Na walioacha kwenda hospitali kwa kigezo cha Imani yao wamekufa.

"Zakuambiwa changanya na zako". Jk's voice.
 
Kiranga hauamini uwepo wa Mungu hata nikikujibu "Kwa nini" Papa Francis alimjibu hivyo,bado utabisha,na mimi huwa sipendelei kubishana,halafu sijui kubishana,mimi majibu yangu huwa ni "Yes" au "No" halafu naweka nukta.

Hapo Papa Francis ni kama alikuwa ana muambia huyo binti asimlilie Yesu bali binti ajililie nafsi yake.Kuelewa hili inahitajika hekima au akili ya hali ya juu kama ambavyo kuelewa Luka 23:27 ina mhitaji mtu kuwa philosopher ili aelewe.

Luka 23:27 Yesu akawageukia akasema,Enyi binti za Yerusalemu(zinaweza kuwa binti za mahali popote,binti za Bukoba,binti za Geita,binti za Mwanza,binti za Dar es Salaam n.k),msinililie mimi ( Yesu anasema wasimlilie yeye maana anajua anaenda kutimiza mission yake aliyotumwa na Mungu kuja kumkomboa mwanadamu) , bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Binti ajililie nafsi yake ili na yeye siku moja aweze kutimiza mission ya roho yake aliyopewa na Mungu kuja kuikamilisha duniani,awe mtakatifu.
Unahubiri dini wakati mimi natafuta jibu la kimantiki, hatuwezi kuelewana.

Papa hakujibu swali, alipiga danadana za kisiasa ya dini.

Ambazo na wewe unaendeleza hapa.

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya?

Hakuna aliyejibu swali hili.

Epicurus aliyezaliwa miaka 341 kabla ya Yesu aliuliza hili swali siku hizo. Mpaka leo halijajibiwa.

Na hata Papa mwenyewe kakubali hana majibu ya swali hili.

Kwa sababu si mtu ambaye halijui swali hili na ugumu wake.

Papa kasoma falsafa na theolojia. Anajua ugumu wa swali hili. Anajua halina jibu la kimantiki.

Ndiyo maana akabaki kuhubiri longolongo.

Binti analilia nafsi yake kwa kuulizia the problem of evil halafu wewe unamwambia aililie nafsi yake?

Aililie nafsi yake mara ngapi?
 
Dah! Mungu amekujaalia sana
Mungu hayupo mkuu.

Angekuwapo watu wasingeijua internet ya bando ikoje.

Kila mtu angekuwa anagonga unlimited ya kampuni ya simu na unlimited ya WiFi kama mimi tu.

Kama yupo, kwa nini anipendelee mimi nisiyemuamini halafu wanaomuamini wengine wawe wananuka umasikini hata bando wapate kwa manati na wengine wana viswaswadu vimepasukapasuka vioo ni hatari kwa afya zao lakini wanadunda navyo tu?
 
Back
Top Bottom