Mbona internet ya Dodoma ni Vodacom tu?

Mbona internet ya Dodoma ni Vodacom tu?

Mimi ni mgeni Dodoma. Kwenye mitandao natumia zaidi Halotel na Tigo kutokana na unafuu wa gharama.

Nilipofika hapa internet inasumbua mno kiasi kwamba siwezi kustream na kuangalia video kwenye internet, wakati mwingine hata kuingia JF natakiwa kusubiri muda kidogo.

Awali nilijua simu imeharibika nikawa nafikiria kuidispose kabla ya kupata wazo la kujaribu Vodacom. Vodacom wana 4G kama Tigo lakini wako faster mno.

Nimeumia sana kwa sababu mimi sio mpenzi wa Vodacom kutokana na gharama zao. Kwa kweli Vodacom natumia M-Pesa tu.

Halotel na Tigo rekebisheni mapungufu haya, mnatuumiza wateja wenu.

Ni kweli, nikuwa Dodoma kwa wiki moja mwezi uliopita nilipata changamoto kwa internet airtel
 
Back
Top Bottom